Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 304
- 518
Njombe
Wanafunzi 11 wa shule ya sekondari Kidegembye iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wamepata ajali kwenye gari wakitoka kupakia kuni za mwalimu majira ya usiku.
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimefika katika hospitali ya mji wa Njombe (Kibena) ambako wanafunzi wanapatiwa matibabu na kutoa maelekezo kwa serikali kuandaa majibu juu ajali hiyo.
"Tumetoka kukagua utekelezaji wa Ilani na kupata taarifa kuwa kuna ajari wanafunzi wameumia Sasa madaktari wa zahanati pale Kidegembye wamekiri kupokea wanafunzi 11 lakini wengine walitibiwa na kuruhusiwa na sita waliletwa huku (Kibena)"amesema Julius Peter Katibu wa CCM mkoa wa Njombe
Aidha amesema kwa maelezo ya walimu,wanafunzi hao walipata ajari majira ya saa moja jioni wakiwa kwenye gari aina ya fuso wakati wakitoka kupakia kuni za mwalimu ambapo amesema wameielekeza serikali kutoa majibu ya hatua zinazoendelea dhidi ya aliyesababisha ajali.