Wanafunzi 1,800 Wanakalia Mawe madarasani Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 1,800 Wanakalia Mawe madarasani Kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jul 8, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,211
  Likes Received: 3,624
  Trophy Points: 280
  ZAIDI ya wanafunzi 1,800 wa shule za misingi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wanatumia mawe, magogo na mifuko ya plastiki maarufu kama ‘rambo’ kama viti vya kukalia wawapo madarasani kutokana na uhaba wa madawati unaozikabili shule hizo.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa, kati ya shule 47 za Manispaa ya Kigoma-Ujiji, takribani asilimia 55 tu ya wanafunzi wanapata fursa ya kutumia madawati wakati wa masomo hali inayochangia kushuka kwa elimu katika wilaya hiyo.

  Kwamba manispaa hiyo inakabiliwa na upungufu wa madawati 5,883 ili kukidhi haja ya wanafunzi kukalia madawati, hasa wakati wa masomo ambapo imefahamika kwa sasa kuna madawati 8,117 pekee.

  Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wadau wa elimu, akiwamo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwasenga, Jeremia Ntibashima, changamoto ya upungufu wa madawati mashuleni unachangia taaluma za wanafunzi kuwa duni.

  Mwalimu Ntibashima alifafanua kuwa, pamoja na majengo mazuri katika shule za manispaa, lakini bado suala la uhaba wa madawati ni la msingi katika kukuza na kuendeleza taaluma ya mwanafunzi shuleni.

  Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Tatala Mpangalukela alisema kuwa, moja ya njia ya haraka ya kuondokana na changamoto hiyo ni kwa wahisani na mashirika mbalimbali kusaidia misaada ya madawati.

  Mpangalukela alifafanua kuwa, misaada ya wahisani na mashirika kwa kiasi kikubwa imechangia kupunguza uhaba wa madawati kwani manispaa hiyo imeshapokea madawati zaidi ya 419 kutoka kwa Hifadhi ya Taifa (TANAPA).

  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongella alieleza kuwa, ongezeko la shule za msingi katika kila kijiji na kitongoji, ni moja ya changamoto ambazo zinaikabili serikali na wadau wa elimu na kuwataka kushirikiana kwa pamoja kupata suluhisho.

  Mongella alieleza kuwa, serikali imetatua tatizo kubwa la kukosa majengo kwa kujenga shule kila mahali, na sasa juhudi ni kuhakikisha kuwa madawati yanapatikana.
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,211
  Likes Received: 3,624
  Trophy Points: 280

  Saafi sana JK,Saafi sana Shein,Saafi sana Malecela,Saafi sana Pinda,na Saafi sana watz wote wenye mapenzi mema na nchi yetu kwa kizazi hiki cha Kigoma!Naam ni kweli kabisa kama wanavyosema wenyewe wenye nchi "tz yenye neema inawezekana,na hata sisi tupo kwenye era ya sayansi na technolojia"

  Kukaa kwenye mawe,magogo na hadi kutandika mifuko ya plastiki watoto wetu mashuleni wao haiwahusu,inachojali tu ni kumtuma Malecela na Mkuchika kusimamia chaguzi zao!Tungekuwa wapi kimaendelao kama wangemtuka Mama Sitta,au Ngelaja au Masha kushughulikia kero za wananchi??
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  a)Namshauri mkurugenzi kabla hajaomba msaada kwa wahisani "auze gari lake VX anunulie madawati watoto, DC auze VX annue madawati shame on you shame on CCM
  b) Mbunge wa jimbo atoe per diem yake bungeni anunue madawati
   
 4. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kikwete yuko wapi wakati haya yote yakitokea?
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huko si ndio kulisahauliwa na akina nyerere, mwinyi na nkapa, angalau wakati huu wa JMK tunaweza kujuwa nini kinaendelea ili kipatiwe ufumbuzi
   
 6. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Angalau? Haya yote yamejulikana sana wakati wote kuanzia uhuru unless kama hukukulia Tanzania. Kikwete ameingia madarakani akiyajua yote haya ila anaelekea kumaliza ngwe ya kwanza akiwa amenunua magari ya kifahari zaidi ya viongozi wote waliomtangulia.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inawezekana ikawa ni hivyo, kila mtu na uono wake, wangu unaniambia JMK anafanya kweli, kuliko wote waliomtangulia, tatizo ni sisi wenyewe, tunangoja tufanyiwe kila kitu, Jee wewe ulianya nini katika hilo badala ya kulaumu? ulisha towa japo kiti kimoja au kajamvi ukakapeleka kusikokuwa na viti? Kama hujawahi, nakushauri fanya hivyo. Mwenzako nimeshawahi, ingawa si kwa Kigoma.
   
 8. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na mimi nimetoa on top ya kodi zangu ninazolipa serikalini kila siku.

  Kama wananchi wakitoa kodi ili serikali itumie pesa hizo kufanya mambo kama haya, je kuna sababu ya wananchi tena kutoa pesa zao binafsi?

  Swali la nyongeza - pesa zilizolipwa Richmonduli (wakati wa utawala wa JK)zingeweza kujenga madawati mangapi?
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kodi zako hazitoshi, kutowa ni moyo.

  Zililipwa na nani na kwa nani na zilikuwa ngapi?

  Zilizonunuwa Rada jee? na zilizonunuwa ndege ya Rais, na zilizoporwa BOT ambazo JMK kaweza (kuzirudisha) angalau si zote. Na zilizojenga hekalu kule Lushoto? na zilizonunuwa Kiwira? na zilizonunuwa majumba Upanga, Jamhuri, Mtwara? na zilizo fungulia ofisi binafsi Ikulu? Na zilizo fanyia matibabu ya kujaribu kupunguza uzito, Switzerland, mbona zote hizo huzitaji?
   
 10. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa twaongea lugha moja. Haya yote yametokea Kikwete akiwa waziri wa serikali hiyo ya kifisadi ya Mkapa. Baada ya kufanikiwa kuupata uraisi kwa wizi wa BOT (ambao mpaka sasa hajasema kwa usahihi pesa zimerudi kiasi gani), ameendelea na ufisadi zaidi na kusahau kuwa pesa za serikali zinatakiwa kutumika kwenye vitu kama hivi - ununuzi wa madawati.

  Kwa sasa kikwete anahusika mara mbili - wakati akiwa waziri kwenye serikali ya kifisadi ya Mkapa, na sasa ambapo ufisadi unazidi kwa kasi ya ajabu huku naye akijenga mahekalu yake sehemu zaidi ya tatu ndani ya Tanzania.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuwa waziri hakumaanishi u-fisadi. Ingekuwa hatujaona JMK kuchukuwa action yeyote katika kipindi chake, tungemlaumu sana, leo kuna makesi kibao yanayohusisha huo ufisadi wa BOT na kwingine kwingi, tumeshaona mpaka waziri mkuu akiporomoka wakati wake (kitu ambacho hata kama kimetokea zamani basi kisingejulikana ni kwa nini).

  JMK anafanya kweli na ndio maana leo tunawajuwa mafisadi na tunaona hatuwa zinazochukuliwa.
   
 12. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mafisadi hao ni pamoja na Rostam Azizi, Manji, Andrew Chenge, nk?

  Kuwa waziri katika serikali ya kifisadi ya mkapa na ukaendelea kushiriki kipamoja na maamuzi ya serikali hiyo (collective responsibility) kunamfanya waziri kuwa equally fisadi.

  Unakumbuka miaka ambayo Kikwete alikuwa waziri wa madini? unajua kwa hakika ni mikataba kiasi gani ya madini ilisainiwa kifisadi?
   
Loading...