Wanadodoma kuweni makini na wahudumu wa royal village ni wezi sana

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,363
Habarini wanajamvini wakazi Wa Dodoma.
Aisee kuna hii sehemu nzuri Sana ya kula bata, vinywaji na starehe za hotel, swiming etc

Ni sehemu nzuri ya kukaa na kutulia, tatizo lao ni moja tu wahudumu Wa pale ni wezi Sana, yani ukienda we mgeni na hujui bei unachomekewa bei iliyojuu. Kuanzia kaunta mpaka wahudumu.

Chakushangaza wahudumu huwa wanajisifia wakikaa wao kwa wao kuwa, Leo nimeingiza laki mbili, Leo kuna mtu nimempiga kvant 20000 badala ya 13000.

Sasa wananchi kuweni makini, ikibidi mkienda pale muulizie mpewe menu iliyokuwa signed na mkurugenzi inayoonesha bei halisi ya kila kinywaji.

Nawashauri hawa wahudumu hasa wadada wafanye mkakati Wa kumwibia boss wao, na sio raia wema.

Bosi wao si tajiri, tena ndugu yake ni mbunge hapa dodoma na tajari anaemiliki mabasi na mahoteli, waibieni hao, sio sisi
 
Mkuu ndugu wa bosi wao ni mbunge Nlogolo huko....sio Dodoma. Hata hivyo kwa namna yoyote ile wizi haukubaliki,sio kwa mteja wala kwa muajiri....kesho na keshokutwa tutalalamika ajira kwa wahindi &wakenya kwasababu ya uaminifu wao
 
Hilo neno hatari
 
Habarini wanajamvini wakazi Wa Dodoma.
Aisee kuna hii sehemu nzuri Sana ya kula bata, vinywaji na starehe za hotel, swiming etc

Ni sehemu nzuri ya kukaa na kutulia, tatizo lao ni moja tu wahudumu Wa pale ni wezi Sana, yani ukienda we mgeni na hujui bei unachomekewa bei iliyojuu. Kuanzia kaunta mpaka wahudumu.

Chakushangaza wahudumu huwa wanajisifia wakikaa wao kwa wao kuwa, Leo nimeingiza laki mbili, Leo kuna mtu nimempiga kvant 20000 badala ya 13000.

Sasa wananchi kuweni makini, ikibidi mkienda pale muulizie mpewe menu iliyokuwa signed na mkurugenzi inayoonesha bei halisi ya kila kinywaji.

Nawashauri hawa wahudumu hasa wadada wafanye mkakati Wa kumwibia boss wao, na sio raia wema.

Bosi wao si tajiri, tena ndugu yake ni mbunge hapa dodoma na tajari anaemiliki mabasi na mahoteli, waibieni hao, sio sisi
Kila mtu anakula ofsn kwake
 
Mkuu ungeenda African Dreams jirani na hapo
kaka mmpongeze kwanza kwa kuripoti hili la royal village kabla ya kum direct aende sehemu nyingine.

asante sana mleta mada.
next week ninatarajia kuja dodoma na mimi ni mtu wa kupenda kula bata maeneo mazuri kama hapo ulipopataja. nitachukua tahadhari.
 
Nitafanya hivo siku nyingine
Huu wizi umeenea sehemu nyingi sana. Pole sana kama ndiyo unaugundua leo. Kama Dar Es Salaan ndiyo nyumbani kwake. Karibu kila Bar na sehemu za makulaji utakazoenda unatakumbana na hii kadhia. Wale walionza kuiba mwanzoni wengine walijenga hata nyumba. Ukiagiza chochote wakiona wewe ni mgeni mgeni au umekaa kitajiri tajiri au kutojali jali ni lazima wakulime. iwe bia, soda au chakula. Ni tabia sugu kabisa. Kuepuka hii tabia ilitakiwa wenye sehemu za huduma kuweka menu kwenye kila meza na mabango ya bei kwenye kila kona! Na kwa taarifa yako huiba kwa kushirikiana na hao wanaoitwa ''mameneja'' au wasimamizi wa sehemu husika. Dawa yao ni wewe kuwa active na kwenda kuuliza bei mwenyewe kbla ya kuagiza. Na kuna njemba nyingine zinatowa onyo kwanza kabla ya kuagiza kuwa wakimbambikia bei hapatakalika. Basi wakiona mtu wa aina hiyo huwa wanachukia kweli kweli.
 
Back
Top Bottom