Wanachuo wa UDSM na 'timing' tamu kwa Serikali ya Rais Magufuli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Wanachuo wa UDSM,akiwemo kijana wangu,wamecheza kama Pele. Wamegoma muda muafaka na hivyo kusikilizwa kwa haraka. Kijana wangu ameniarifu kuwa wanachuo walikata shauri la kugoma muda mwema. Muda ambao UDSM inapaswa kuwa tulivu,safi na ya kuvutia.

Kesho,tarehe 2/6/2016,Rais John Pombe Magufuli atakuwa UDSM kuweka jiwe la msingi la Jengo la Maktaba ya Kimataifa inayojengwa chuoni hapo kwa msaada wa Serikali ya China. Rais asingependa,wala isingependeza,kukuta wanachuo wa UDSM wapo kwenye mgomo.

Mgomo wa jana ulihusu kucheleweshwa kwa fedha za kujikimu kwa wanachuo hao toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Nyaraka za kimalipo chuoni hapo zinaonesha kuwa wanachuo walianza kupewa stahiki zao jana na wengine leo. Timing tamu!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
 
Wanaogopa Kubanguliwa kama KOROSHO,Bado Tulia tu Mzee Wangu,Tufikishie Ombi hili kwamba yule aliyemteua anamuharibia badala ya kumsaidia
 
Back
Top Bottom