Geza Ulole
Platinum Member
- Oct 31, 2009
- 75,731
- 107,175
2nd June 10
Wanachuo wa St. Joseph wagomea ongezeko la ada
Beatrice Shayo
Zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, wamegoma kuingia darasani kwa madai ya kupandishiwa ada ya masomo pasipo kushirikishwa.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi hao ambao wanasoma mafunzo ya Uhandisi, walisema kiasi kilichoongezwa na bodi kwa sasa hakitambuliki na badala yake serikali inatambua ada ya zamani.
Kutokana tafrani hiyo, wanafunzi walifanya fujo na kuanza kurusha mawe katika majengo ya chuo hicho huku wengine wakivunja vioo pamoja na kugonga milango.
Hali hiyo ilidumu kwa muda wa saa tatu ambapo walimu wao walilazimika kuingia kwenye ofisi zao.
Baadhi ya wanafunzi hao walisikika wakisema wamechoka kuonewa na uongozi wa chuo hicho.
Mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema kitendo cha kupandishiwa ada hakikubaliki.
Alisema awali walikuwa wakilipa ada ya masomo ya Sh. milioni 2.4 lakini sasa wameambiwa walipe Sh. 2,750,000. ikiwa ni ongezeko la Sh. 350,000.
Wanafunzi hao walisema wanakusudia kuyafikisha malalamiko yao kwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Vurugu za wanafunzi hao ziliufanya uongozi wa chuo kupiga simu kituo cha polisi cha Mbezi kutaka msaada.
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbezi, Milton Tandali, alifika eneo hilo ambapo aliwasihi wanafunzi hao kuacha fujo na badala yake waketi katika meza moja na uongozi wa chuo kwa ajili ya mazungumzo.
NIPASHE

My take:
Jamani mi siafiki huu uhuni wa wanavyuo kuharibu mali za vyuo binafsi kwa kisingizio ati wanaonewa, jamani tujiulize wa kurushiwa mawe hapa ni chuo au serikali ya CCM chini ya Mbayuwayu na Mkulo ambao wamekataa kupunguza matumizi ya serikali yao na wakaona bora wachukue mkopo bila kututangazia wataliapa vp na kwa riba kiasi gani? au hizi taasisi zinazojiendesha kwa shida na kujaribu kumudu gharama za uendeshaji?
Hivi nani asiyejua hivi vyuo vya kini ni Non-Profitable Organizations vingi vyao vikijengwa na sadaka na misaada ya taasisi ndugu za nchi zilizoendelea? Hivi lini tutaondoa matongotongo na kujua hivi vyuo ni binafsi na vina haki ya kumudu gharama za uendeshaji? nashangaa eti hawa wanafunzi walioharibu mali ati wanasema wanaenda kukishitaki chuo kwa Waziri Mkuu (mtoto wa Mkulima) hii inachekesha badala ya kuandamani kupinga mfumuko wa bei za bidhaa yaani uchumi kudorora na hela yatu kuporomoka hawa wanafunzi wenye mtindio wa ubongo wanafanya fujo!
Hivi hawajui kwamba hata hizo taasisi kuamua kuanzisha vyuoi kazi yao ila ni kwa kuona jinsi serikali inavyoshindwa kutoa huduma! Kwanini kama mtu hamudu hizo gharama asiende kumlilia Prof. Maghembe awape mikopo? au kwanini wasisome vyuo vya serikali ka chuo kenyewe kana wanafunzi 500 sasa lini katakuwa na wanafunzi 5000 katika matakwa ya hawa wanavyuo? au lini kule Kantalamba au Kigoma watapelekewa huduma? hivi si hawa wanavyuo baadaye mwaka huu tutawaona wamevaa Tshirt za Njano na kijani wakikampeni CCM irudi madarakani?
Hivi jamani tunajisahau hizi taasisi zina majukumu pia ya kulipa wafanyakazi nakuongeza huduma kama vifaa vya kufundishia na kutoa elimu bora! Ninachoshwa na ujinga wa Wadanganyika wakiambiwa wagome wanaogopa kuwa Mbayuwayu na ndezi! hivi lini tutajua thamani ya kura zetu? I am out of here!