Wanachuo wa St. Joseph wagomea ongezeko la ada

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,186
79,368
2nd June 10
Wanachuo wa St. Joseph wagomea ongezeko la ada

Beatrice Shayo

Zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, wamegoma kuingia darasani kwa madai ya kupandishiwa ada ya masomo pasipo kushirikishwa.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi hao ambao wanasoma mafunzo ya Uhandisi, walisema kiasi kilichoongezwa na bodi kwa sasa hakitambuliki na badala yake serikali inatambua ada ya zamani.
Kutokana tafrani hiyo, wanafunzi walifanya fujo na kuanza kurusha mawe katika majengo ya chuo hicho huku wengine wakivunja vioo pamoja na kugonga milango.
Hali hiyo ilidumu kwa muda wa saa tatu ambapo walimu wao walilazimika kuingia kwenye ofisi zao.
Baadhi ya wanafunzi hao walisikika wakisema wamechoka kuonewa na uongozi wa chuo hicho.
Mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema kitendo cha kupandishiwa ada hakikubaliki.
Alisema awali walikuwa wakilipa ada ya masomo ya Sh. milioni 2.4 lakini sasa wameambiwa walipe Sh. 2,750,000. ikiwa ni ongezeko la Sh. 350,000.
Wanafunzi hao walisema wanakusudia kuyafikisha malalamiko yao kwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Vurugu za wanafunzi hao ziliufanya uongozi wa chuo kupiga simu kituo cha polisi cha Mbezi kutaka msaada.
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbezi, Milton Tandali, alifika eneo hilo ambapo aliwasihi wanafunzi hao kuacha fujo na badala yake waketi katika meza moja na uongozi wa chuo kwa ajili ya mazungumzo.


NIPASHE

Wanachuo wa St. Joseph wagomea ongezeko la ada
 
Back
Top Bottom