MSIMISEKI SENIOR
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 459
- 287
Katika hali isiyo na usawa ni kile wanachotendewa wanafunzi wanao omba kujiunga Undergraduate katika mwaka wa masomo 2016/17 wakiwa na Diploma kama sifa za kuingilia (Equivalent). Huu uonevu nadhani kuna tatizo mahali fulani ambalo linafichwa na haliwekwi wazi sana kwani hii hali haikuwepo hapo nyuma.
Mimi ni graduate miaka 7 imepita. Bahati nzuri mimi wakati najiunga na chuo wakati ule nilijiunga nikiwa nina Diploma hivyo niliingia kama (Equivalent). Wakati ule tulikuwa tunaomba vyuoni moja kwa moja, kupata nafasi ilitegemea sana ufaulu wako na nature ya kozi uliyoomba.
Ninakubaliana na utaratibu mpya ulioanza mwaka juzi wa wanafunzi wote kuomba kupitia TCU na NACTE lakini sikubaliani na utaratibu (treatment) wanayopewa Equivalents mwaka huu. Ni vizuri wenye nafasi za kusimamia huo udahili wakatambua kuwa mtu kuwa na Diploma siyo dhambi wala siyo kigezo cha mtu kutokuwa na uwezo darasani. Leo hii mnatoa tu majina ya walioomba wakiwa na form six mnawaacha walioomba kama equivalents hii siyo haki hata kidogo.
Kutokana na hili mnatujengea picha kwamba anayestahili kwenda chuo kikuu ni lazima aingilie kama kidato cha sita moja kwa moja, wakati miongoni mwa equivalents wapo waliohitimu kidato cha sita wakajiunga na diploma leo wanatamani na wao kujiunga chuo kikuu.
kibaya zaidi, baada ya kukamilisha udahili wa Form 6 leo mmewapa nafasi ya kuchagua upya kozi, lakini hao equivalents hamjawapa nafasi hiyo zaidi wa kuruhusu wale tu ambao hawakuomba awamu ya kwanza ndiyo waombe. Sijui ikitokea huyu equivalent naye akakosa licha ya kuwa na sifa je atapewa nafasi ya kufikiria kufanya upya machaguo?
Haki lazima itendeke kwa wote au basi msiwashawishi vijana kujiunga na Diploma muwaache waende moja kwa moja 1st degree ili kuwaondolea usumbufu ambao wataupata pindi watakapokuwa tayari kujiunga hapo baadae.
Mwaka huu naona masharti yamekuwa magumu sana si TCU wala HESLB naona wote lengo lao linafanana kwa hawa equivalents. Ni wakati wa kuinua sauti na kulipigia hili kelele kwani siyo sahihi ni unyanyasaji. Naona kama kuna mpango wa kuwaacha vijana wengi wenye diploma na ushahidi huo upo wazi.
LEO UNAPOTANGAZA KUKAMILIKA KWA UDAHILI WA FORM 6 PEKEE NA KUWARUHUSU KURUDIA UPYA PASIPO KUTOA PIA MAJIBU YA HAO EQUIVALENT ILI NAO WAJUE KAMA MTU AMEKOSA AWAMU YA KWANZA MAANA YAKE UNATAKA BAADAE UMNYIME NAFASI HUYU EQUIVALENT KWA KISINGIZIO KWAMBA USHINDANI ULIKUWA MKUBWA
Vijana, wengine tulishapita lakini tunawaonea huruma sana. Jitokezeni kujenga hoja ya msingi juu ya hii haki yenu ili wanaohusika wote wachukulie suala lenu kwa uzito.