Wanachotendewa Equivalent students na TCU hakina usawa

MSIMISEKI SENIOR

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
459
287
Katika hali isiyo na usawa ni kile wanachotendewa wanafunzi wanao omba kujiunga Undergraduate katika mwaka wa masomo 2016/17 wakiwa na Diploma kama sifa za kuingilia (Equivalent). Huu uonevu nadhani kuna tatizo mahali fulani ambalo linafichwa na haliwekwi wazi sana kwani hii hali haikuwepo hapo nyuma.

Mimi ni graduate miaka 7 imepita. Bahati nzuri mimi wakati najiunga na chuo wakati ule nilijiunga nikiwa nina Diploma hivyo niliingia kama (Equivalent). Wakati ule tulikuwa tunaomba vyuoni moja kwa moja, kupata nafasi ilitegemea sana ufaulu wako na nature ya kozi uliyoomba.
Ninakubaliana na utaratibu mpya ulioanza mwaka juzi wa wanafunzi wote kuomba kupitia TCU na NACTE lakini sikubaliani na utaratibu (treatment) wanayopewa Equivalents mwaka huu. Ni vizuri wenye nafasi za kusimamia huo udahili wakatambua kuwa mtu kuwa na Diploma siyo dhambi wala siyo kigezo cha mtu kutokuwa na uwezo darasani. Leo hii mnatoa tu majina ya walioomba wakiwa na form six mnawaacha walioomba kama equivalents hii siyo haki hata kidogo.

Kutokana na hili mnatujengea picha kwamba anayestahili kwenda chuo kikuu ni lazima aingilie kama kidato cha sita moja kwa moja, wakati miongoni mwa equivalents wapo waliohitimu kidato cha sita wakajiunga na diploma leo wanatamani na wao kujiunga chuo kikuu.

kibaya zaidi, baada ya kukamilisha udahili wa Form 6 leo mmewapa nafasi ya kuchagua upya kozi, lakini hao equivalents hamjawapa nafasi hiyo zaidi wa kuruhusu wale tu ambao hawakuomba awamu ya kwanza ndiyo waombe. Sijui ikitokea huyu equivalent naye akakosa licha ya kuwa na sifa je atapewa nafasi ya kufikiria kufanya upya machaguo?
Haki lazima itendeke kwa wote au basi msiwashawishi vijana kujiunga na Diploma muwaache waende moja kwa moja 1st degree ili kuwaondolea usumbufu ambao wataupata pindi watakapokuwa tayari kujiunga hapo baadae.

Mwaka huu naona masharti yamekuwa magumu sana si TCU wala HESLB naona wote lengo lao linafanana kwa hawa equivalents. Ni wakati wa kuinua sauti na kulipigia hili kelele kwani siyo sahihi ni unyanyasaji. Naona kama kuna mpango wa kuwaacha vijana wengi wenye diploma na ushahidi huo upo wazi.

LEO UNAPOTANGAZA KUKAMILIKA KWA UDAHILI WA FORM 6 PEKEE NA KUWARUHUSU KURUDIA UPYA PASIPO KUTOA PIA MAJIBU YA HAO EQUIVALENT ILI NAO WAJUE KAMA MTU AMEKOSA AWAMU YA KWANZA MAANA YAKE UNATAKA BAADAE UMNYIME NAFASI HUYU EQUIVALENT KWA KISINGIZIO KWAMBA USHINDANI ULIKUWA MKUBWA

Vijana, wengine tulishapita lakini tunawaonea huruma sana. Jitokezeni kujenga hoja ya msingi juu ya hii haki yenu ili wanaohusika wote wachukulie suala lenu kwa uzito.
 
Ni kweli kaka,unajua hata ishu ya uombaji mikopo kwa dip.holders haijatulia sana na uhakika ni mdogo,yaani unaomba mkopo ukiwa hauna hata matokeo ya dip.pia kuna suala la muda wa uombaji kujiunga na vyuo vikuu.
 
Kaka dah kwa hilo umejenga hoja safi kiukweli inaboa kuona mwenzio Wa form six kachaguliwa na kupewa nafasi wakat we we hujui chochote bro wew acha yani nakesha katikq profile language hata angalau niione wakinambia niombe second round
 
Tupo kama nchi ya kusadikika tunawekwa nyuma muda wote profile muda wote bize wakifungua hakuna kitu sasa sielewi wakifungua hiyo tarehe 23 na mtu ukikosa sijui kama wataongeza muda to much tired na mfumo huu.
 
Iman yao ni kwamba wenye diploma walifeli shule sasa chakushangaza wametoa wa form six wanaenda degree mwaka huu na wanajipongeza kwa kaz nzur ambazo wamezifanya juu ya form six, cjui sis wa diploma degree zetu ni za vyuo vingine haiji akilin kila kitu tunakua wa mwisho afu Hakuna taarifa zozote je tuliokua tumeapply mwanzon tukiwa na hizo jpa tukikosa vyuo kuna second apply tena hakuna jibu, hakuna haki hapo
 
Iman yao ni kwamba wenye diploma walifeli shule sasa chakushangaza wametoa wa form six wanaenda degree mwaka huu na wanajipongeza kwa kaz nzur ambazo wamezifanya juu ya form six, cjui sis wa diploma degree zetu ni za vyuo vingine haiji akilin kila kitu tunakua wa mwisho afu Hakuna taarifa zozote je tuliokua tumeapply mwanzon tukiwa na hizo jpa tukikosa vyuo kuna second apply tena hakuna jibu, hakuna haki hapo
"Yatupasa kusali na kuswali sana maana tcu ni shedwaaaaaaaaa"
 
Wadau..
Kuna kitu mnaweza mkawa hamjafuatilia..
Kibaya wanachofanya ni kimoja tu kuchelewesha na nikotokana na mwaka mfumo kuhama toka kusimamiwa na nacte kwenda tcu..
Ila swala la nafasi za diploma zipo pale pale..
Kila chuo kina nafas za kwa diploma na form 6..
So hawa madogo majibu kutoka si kuwa nafas za diploma wamechukua hapana ila kibaya ni kuchelewesha ukizingatia kuna diploma wameomba toka april..
Watatoa, ila ishu ni system ya nacte ilikuwa weak sana. .. Mm nina ushahid mtu ana gpa ya 2.5 na alipata chuo mwaka jana.. Walikuwa hawana accuracy kabisa so kuamia tcu kuwa system moja.ina wamonitor hop mwakan itakuwa poa japo mwaka huu wameathirika na kuhama huku
 
Kusema ukweli na uchunguzi watanzania wengi bado wanajua mtu mwenye elimu ni yule wa form six na degree na sio diploma hata mtu ukiwa mtaani ukasema wewe unasoma diploma mtu anakuchulia poa poa tu ko mimi naona hiki kitu ndo bado kiko vichwank mwa watu wengi
[HASHTAG]#God[/HASHTAG] will do something, mimi naamini degree lazima twende tu
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom