Wanachokitaka upinzani si uchaguzi, bali vurugu. Serikali iwachunguze Vizuri

MwanaPekee

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
382
385
Upinzani wa Tanzania ni mgumu sana kuulewa maana hata hawaeleweki nini hasa wanakitaka. Wakati zoezi la kuandikisha wapiga kura lilipokuwa likiendelea, na serikali kutumia muda mwingi kuwaelimisha watu umuhimu wa wao kujiandikisha na kupiga kura, Upinzani ulishangilia na kuwaunga mkono wale ambao hawakujitokeza kujiandikisha.

Hata hivyo Serikali ilitumia juhudi kubwa kuhakikisha idadi kubwa ya watu inafikiwa. In short hakuna aliyelalamikia mchakato huo kwa upande wao kuwa ulikuwa na kasoro zozote za kikanuni, zaidi ya kuwaunga mkono wale ambao hawakujiandikisha.

Hatua ya pili ilikuwa ni kwa wagombea kuchukua forms na kuzijaza kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazoongoza uchaguzi wa Serikali za mitaa. Katika hatua hii ndipo malalamiko yalipoanzia hasa baada ya wagombea wao wengi kuonekana wakikiuka Sheria na Kanuni hizo na hivyo kuenguliwa kwenye mchakato wa kugombea uongozi kwa nafasi mbalimbali.

Serikali imesikiliza kilio chao na kuamua kuwaruhusu wagombea wao wote waliochukua na kurejesha kushiriki katika uchaguzi huo licha ya kukiuka baadhi ya Sheria na Kanuni hizo, lakini bado wamekuja na hitaji la “Kuanza mchakato upya, yaani kuanzia uandikishaji wa wapiga kura”, la sivyo hawatashiriki.

Najiuliza kwanini hawakulalamikia mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura toka mwanzo, na sasa wanataka turudi huko? Je, kwanini wanasema hawatashiriki hata baada ya malalamiko yao kusikilizwa? CCM, imepita bila kupingwa katika maeneo ambayo wao hawakuweka mgombea, sasa wao walitaka iwaje?

Ninachokiona mimi hapa ni kuwa hawa watu hawana shida na uchaguzi. Wao wanatengeneza mazingira ya kuonekana wanaonewa kila wakati. Itakuwa poa kama serikali itawachunguza watu wachache wanataka kuvuruga mchakato huo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Na kuhusu uchaguzi, hakuna haja ya kuwabembeleza, vyama vilivyotangaza kujiondoa ni vitatu tu, lakini kuna vyama vingi tu (Almost 10) ambavyo viko tayari kuendelea na mchakato.

Tuache Maneno, Tuchape Kazi, Tulijenge Taifa Letu.
 
MwanaPekee,
Kwa taarifa yako upinzani wanajua kilaaina ya hila zenu, wanajua mpaka idadi ya waliojiandikisha!

2015 ile misululu ya watu waliokuwa wanajiandikisha idadi kamili ilikuwa ni 19m na kwa jinsi mnavyosahau, eti kwa kulazimishwa kule na idadi ndogo kabisa ya waliojitokeza bado wamefikisha idadi ileile kama ya ile misululu mirefu!

Ubovu wa Chama chenu, Hata kama MTU yupo vzr upstairs akisilimishwa huko tuu anakuwa hamnazo!

Je watendaji kwanini walizizira ofisi zao? Na polepole kasema mlikodi mawakili 1200 na ushehe! Duu harafu walioenguliwa wamekosea sasa mnataka warudi kufanya nini na wamekosea?

Cha kufurahisha kuhusu mwanadamu ni Hata kwenye filamu ya mnyonyadamu, kuna wanaowaonea huruma wanyonywadamu lakini kuna wanaompenda mnyonyadamu where you certainly belong!
 
Anayetaka fujo CCM ?kwa nini asitoe form au kupokea form za opposition.Kwa nini wakatwe wote?nsitafute pa kufia ,hanzeni kujiapisha basi
 
Anayetaka fujo CCM ?kwa nini asitoe form au kupokea form za opposition.Kwa nini wakatwe wote?nsitafute pa kufia ,hanzeni kujiapisha basi
Mkuu ujue Tatizo CCM wamewadharau watanzania wanawaona ni wajinga sana kuliko wao, lakini kupitia sakata hili CCM wamejifunza mengi, wametambua kuwa kila Mtanzania wa sasa anajua maendeleo yanaletwa kwa kulipa kodi zao siyo Hisani wala pesa binafsi toka mfukoni mwa mtukufu magufuli, maendeleo ni haki ya msingi siyo ombi
 
Back
Top Bottom