wanachama wa CCM wataka Makamba aondoke kukinusuru chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanachama wa CCM wataka Makamba aondoke kukinusuru chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 2, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Source: Raia Mwema page 3.
  "taarifa zaidi zinaeleza kuwa vikao kadhaa rasmi vya chama hicho, vikiwamo vilivyohusisha baadhi ya makatibu makini wa mikoa na wilaya vimebainisha kuwa uongozi wa chama hicho ni mzigo katika kukikwamua chama na bila kusita, vimependekeza Makamba ang'oke."

  "Sababu kadhaa zinatajwa kuhusu haja ya mabadiliko hayo, miongoni mwake ni kukidunga sindano ya uhai mpya chama hicho, ikizingatiwa mtokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita, kwa kuwa baadhi ya viongozi hawakutoa mchango wowote katika kusaidia ushindi wa chama hicho na badala yake walikua kwa matamshi yao na matendo wakisaidia kuporomosha umaaru wa chama hicho."

  Wanaopendekezwa kumata wadhifa huo ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Jaka Mwambi, Abdulrahaman Kinana,Steven Wassira, Chiligati na kama inawezekana kumrudisha Philip Mangula ambaye hakubaliani na mambo kadhaa katika uendashaji wa CCM ya sasa aliyomwachia Makamba
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Jaka mwambi labda..lakini kwa jinsi Mangula alivyokuwa firm kumpinga JK kwenye mbio za urais 2005 hawezi kufanya naye kazi ofisi moja hata iweje
   
 3. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wavunje chama tu,,,ili wafanye mapinduze ndani ya chama kama wanavyojiita "chama cha mapinduzi" la sivyo mwisho wao umefika!!!1
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tatizoo sio kupata katibu mkuu wa chama,shida ipo kupata mtu wa aina ya kuweza kufanya kazi na Mkitii.....makamba wanaiva vema sana na mkiti..
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  CCM wanatakiwa wafahamu kuwa hawatoweza kuitawala hii nchi milele.
  wakubaliane na mwisho wao ndio huu na wameyataka wenyewe.
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Maamuzi ya chama yanafanywa na vikao, bahati mbaya sana katibu si mwenyekiti wa vikao. Naamini matamshi ya Katibu Mkuu si maamuzi binafsi bali ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya vikao halali vya Chama. Kukinusuru chama cha Mapinduzi inatakiwa Kamati Kuu yote ing'olewe na waingie Wanachama wenye uzalendo wa kweli bila kuangalia uwezo wao wa kifedha
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hilo lichama lijifie tu. Lishakuwa kama ugonjwa wa saratani iliyofikia ngazi ya nne, ambayo haina njia nyingine ila kuondoka na uhai tu!
   
Loading...