Wanachama wa CCM Kuweni Macho Itafika Wakati Chama Kitaongozwa na Familia

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wandugu,
Tangu jk aingie madarakani kumekuwa na kasi kwa kiwango cha kutilia shaka ya watoto na ndugu na jamaa wa vigogo kuingia kwenye siasa. Kimsingi, siyo vibaya watoto au ndugu wa kigogo fulani kuingia kwenye siasa. Kinachotia shaka hapa ni kasi ya watoto na ndugu na jamaa hao kuingia kwenye ngazi kubwa za uongozi wakati hawana uzoefu kabisa. Mfano mzuri ni maneno yanayoongelewa sasa kwamba miongoni mwa majina yanayotajwa kuwepo kwenye balaza la mawaziri ni Januari Makama.

Wanachama wa ccm kaeni macho, chama chenu kitaishia kuongozwa na familia. Tabia hiyo lazima ikemewe. Vinginevyo, kila atakayepata fursa ya uongozi nae atapachika ndugu zake.
 
Back
Top Bottom