Wanachama 381 wa CHADEMA Geita wahamia CCM wakabidhi kadi za CHADEMA kwa Upendo Peneza mkutano hadhara Geita

Waambieni wahamie tu chama cha mkoloni mweusi, umeme ukikatika tunakatiwa wote na bei ya sukari ikizidi kupanda tutaathirika wote.
 
Wanachama 381 wa Chadema Geita wahamia CCM wakabidhi kadi za Chadema kwa Upendo Peneza mkutano hadhara Geita

Source: Taarifa ya saa moja Habari Channel 10
Tanu+ccm=1954~2024 70 years old Bado siasa za kugombea wanachama na vyama vya 1992 duh
 
Hakuna ajabu vyama vya Siasa vimekuwa Platform ya kutafuta Kura ili kwenda Kula; Practically Ideologically havina tofauti
 
Tutajua huko mbeleni.

Hesabu hizi zinawezakana zikabadilika kabisa huko 2024-2025

381+19=

Yaani na baada ya 255, baada ya marathon na rides zote zile? Kweli?
 
Kishindo Cha Upendo Peneza kimeendelea kutikisa baada ya Wanachama zaidi ya 380 wa Chadema kukikacha chama hicho kilichopoyeza muelekea na kuhamia Chama Cha CCM chini ya Mwenyekiti shupavu Rais Samia.

My Take: Tuseme Ukiwa na akili timamu huwezi Baki Chadema maana ni mradi wa familia ya Sultan Mbowe na wachaga tena Walutheri Wacha kipukutike,hiyo ni trailer tu.

=========

WANACHAMA 381 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Geita wametangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Uamuzi huo unakuja ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita kupitia Chadema, Upendo Peneza ambaye tayari ameshahamia CCM.

Wanachama hao wamepokelewa rasmi juzi kwenye mkutano ulioandaliwa na CCM mkoa kwa ajili ya kumpokea rasmi Peneza, uliofanyika katika viwanja vya Nyankumbu mjini Geita. Akizungumzia suala hilo, Peneza alisema yote hayo ni matokeo ya serikali iliyopo madarakani kusimamia ukweli na haki na yeye amechagua kuwa mkweli ndio maana amehamia CCM.

“Mimi sikutafutwa na mtu kuingia CCM, nimeomba mwenyewe kuwa mwanachama, kwa hiyo tangu taarifa nilipoitoa kwa viongozi wa CCM wamenipa heshima kubwa sana. “Rais Samia Suluhu Hassan anataka haki, mheshimiwa anataka kila mtu atendewe haki, ndiyo maana baada ya kuingia madarakani aliwatafuta ndugu zetu wa vyama vya upinzani.

“Anataka watu wahudumie watu kwa haki, wananchi wasionewe, kwa sababu huo ndio msingi wa uongozi wake, na kwa sababu hiyo na mimi nitajitahidi kutoa mchango wangu,” alisema.

Daily News
Mmcheppuko....
 
Wanachama 381 wa Chadema Geita wahamia CCM wakabidhi kadi za Chadema kwa Upendo Peneza mkutano hadhara Geita

Source: Taarifa ya saa moja Habari Channel 10
Mfumo wa chadema una shida kubwa kubeba watu smart

Unahitaji marekebisho

Tusibaki tu kulaumu wanachama
Kwanini watu wengi smart inakuwa ngumu kukaa chadema


Naona Mfumo wa chadema una udhaifu mkubwa kubeba /handle smart People
Jambo jema ambalo Mbowe anaweza kufanya cdm ni kuacha mfumo Bora
Mwl Nyerere alikuja kugundua too late kwamba Mfumo alioucha wa chama kimoja ulikuwa dhaifu na ikamlazimu kupambana kuupanua akiwa nje ya nafasi
Akasahau Mfumo mama katiba ilikuwa dhaifu pia

Hili ni kosa naona chadema kutengeneza watu badala ya mifumo imara na itatugharimu baadae Kama Mbowe hataweza kubadili sasa
 
mkuu mirror01 ,jee unanfahamu zaidi ya humu jf, kujua what I do kuendesha maisha yangu?.
P
Pascal Mayalla ...Mkuu achakunionea bure kwasababu tuliitwa wanyonge...hata na mimi huyajuwi maisha yangu njee ya JF.ila wewe tunakujuwa JF kama wanahabari wakujitegemea pia Shadow alio pigwa chini na mtu chamungu Gwajima.Mbona Magufuli wakati amekuita wewe ni njaa hakutoka povu hivo ? Acha kujibu hoja Kwa kubagua huyu ni rais au mnyonge.Kama nimekukosea nisamehe mkuu.
 
Pascal Mayalla ...Mkuu achakunionea kwasababu tuliitwa wanyonge...mbona Magufuli wakati amekuita wewe ni njaa hakutoka povu hivo ? Acha kujibu hoja Kwa kubagua hiyo ni rais au mnyonge.Kama nimekukosea nisamehe mkuu.
Nimekusamehe, peace and love, kuna watu humu ni ma Sherifu, ukimsema tuu mtu vibaya, akikasirika... unakwenda na maji!.
P
 
Back
Top Bottom