WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Hali ya siasa nchini ipo katika kipimo cha Def Cond 003, hii inamaana kuwa tungelitazama katika mizani ya hali ya Taifa, rais angelishatangaza hali ya hatari isiyozidi wala kupungua siku 28 kwamjibu wa katiba ya nchi hii.

Siasa ni mchezo mzuri sana, hakika kwa waamini wa siasa hufarijika wakiwa katika ulingo wa siasa hasa siasa safi, ninatamani sana kuiona Tanzania ikiishi katika siasa safi na ikitumia raslimali watu katika siasa hizo bila tone la damu lakini tamaa yangu inajaribiwa na siasa msonge na za kiimla za wanasiasa wetu nchini.

Kuendesha siasa Afrika ni ngumu, tena ni ngumu kuliko kujitwisha gunia la misumari, ndio ni ngumu kwakuwa vyombo vya dola ambavyo vipo kwamjibu wa katiba na sheria na ambavyo uwepo wake hutokana na kodi za wananchi wa vyama vyote hugeuko vitengo mhimu vya chama kilicho madarakani,

Moja ya mapungufu yaliyomo kwenye sheria zilizozaa vyombo vyetu vya dola ni pale sheria inaposisitiza kuwa ni lazima vyombo hivyo VIAPE kuwa VITAILINDA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI kwa utii na uaminifu.
Hili nimelieleza ili wale wenzangu wanaolalamika kuwa Polisi,TISS, JWTZ nk wanaisaidia CCM, Ukweli ni kuwa wanatimiza kazi yao kwamjibu wa sheria iliyoviunda vyombo hivyo (Invisible Act)

Chama kikuu cha upinzani nchini Chadema kimepita mapito mengi na magumu sana kuanzia mwaka 2005 mpaka hii leo, na majaribu yote yalilenga dhidi ya kifo kamili kwa Chadema, lakini Mungu alivyo si mnafiki chama kiliyashinda majaribu yote hata yale ya alama za damu.

Mwaka 2010 chama kilipata jaribu kuu ambalo kama si umahiri wa Mwenyekiti na timu yake ni dhahiri kuwa leo kingekuwa ni historia tu ya vyama vilivyowahi kuwepo Tanzania, hii ilitokana na KUPORWA ushindi wa uchaguzi wa URAIS na kufuatia wabunge wake kufunguliwa kesi zaidi ya 24 za kupinga matokeo ya uchaguzi wao.
Hayo yote yalitokea chini ya uratibu wa chama tawala kikitumia vyombo vyake vya dola ambavyo mimi wewe na wale tunavilipia kodi zetu.

Matukio yamauaji na utekaji yanayofanywa na CCM kwakutumia vyombo vya dola ambavyo kikatiba na kisheria ni vyauma na kisha kujaribu kuyageuza kuwa ni CHADEMA, ni dalili tosha na ya mwisho kwakuukaribia ushindi na ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi CCM ambae kwa hakika ni mbaya kuliko mkoloni mweupe wa leo.

Huu ni wakati mwafaka kwa wanachadema kutulia na kuonyesha mshikamano wetu, propaganda za ccm zisitunyime usingizi kwakuwa nasi ni wataamu wa propaganda tena za kisasa. Tujipange na kisha tuwakabili kwa propaganda murua na za kisomi bila kuvunja katiba ya nchi wala sheria za nchi.

Katika kipindi hiki ambacho mfumo wa chama unafanya kazi usiku na mchana kuwakabili maadui zetu wa NDANI na nje, ndicho kipindi mwafaka kwetu kukabiliana na propaganda za kitoto za vijana ngumbalo wa ccm waliojazana humu mitandaoni wakijaribu kuganga njaa kwakueneza uongo na uzushi dhidi ya CHADEMA.

Ninawahakikishia kuwa Chadema imezishinda hila zote za CCM za kuifarakanisha na umma, na sasa wanaweweseka tu,
Madiwani wasaliti tuliwapiga chini bila kuangalia sura zao, Masali Tumewapiga chini bila kuangalia sura zao, na sasa VIdeo yao ya Lwakatare imewafia mikononi sasa wanahaha pakutokea hawajui hata sababu yakumshitaki huyo Lwakatare,

Wakati ccm wao wapo bize na Video, Wanachadema tulieni tujikite kwenye ishu zinazowahusu wananchi moja kwa moja, fichueni ubadhirifu, rushwa, na matattizo ya kila sekta nchini,

Chadema iandae vijana wasomi wazuri kisha iwapeleke kwenye wizara zote nchini, wanaweza kupeleka kila wizara vijana 5 tu, hao kazi yao kuu iwe kufichua maovu na matatizo yaliyokwenye wizara hizo, vilevile waweze kupendekeza nini chakufanya ili kuondoa matatizo hayo.

MFAN0: Timu ya vijana hao iyafichue matatizo yaliyo kwenye Elimu, Uchumi, Afya, Ulinzi, Maji,Chakula, Nishati, Miundombinu na kisha viongozi wa Kitaifa waende katika majukwaa ya kiisiasa na waatangazie wananchi hali ya sekta hizo nchini na hatua za haraka za kuchukua. Tukifanya hayo ninaamini ndani ya siku 60 tu CCM itaangushwa na umma wa Watanzania.

PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZZ!!!!! ...................................!!!!
 
Napenda jinsi ambavyo chadema hujipanga na ku-deal na issues. Mfano wakati magamba wakilipua bomu la Rwakatare bado mambo mengine yaliendelea bila kusimama...Mwenyekiti na timu yake walikuwa katika uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki na kazi ilifanyika kwa ufanisi mkubwa. Na hayo ya Rwakatare nayo yalishughulikiwa accordingly. Ni jambo jema sana kuweza ku-deal na multi-tasks. Na hii pia ni tofauti kati ya chadema na magamba.

Mungu Ibariki Chadema.
 
Hakuna mabadiriko yanayopatikana kwa mteremko Mbowe ameshasema mara nyingi kuwa akifa tukanyage maiti yake tusonge mbele mpaka tutakaiona Tanzania yetu mpya,tunajua bado yatakuja makubwa lakini yote yatapanguliwa tu kwa msaada wa mwenyezi mungu maana ndie aliyalika uwepo wa chadema ili kukiponya kizazi cha Tanzania na rasilimali zake
 
Yes, hii ndiyo tofauti kubwa na inayowapa matumaini watanzania kuwa Chadema ndio mkombozi wao pekee.
 
Hakuna mabadiriko yanayopatikana kwa mteremko Mbowe ameshasema mara nyingi kuwa akifa tukanyage maiti yake tusonge mbele mpaka tutakaiona Tanzania yetu mpya,tunajua bado yatakuja makubwa lakini yote yatapanguliwa tu kwa msaada wa mwenyezi mungu maana ndie aliyalika uwepo wa chadema ili kukiponya kizazi cha Tanzania na rasilimali zake

Tutafika katika kilele cha ukombozi bila kukoma wala kuchoka
 
pipooooooooooooooooooooooooooooooooooooz

Tunasonga wakati maccm hawalali.
 
Hili sokomoko lote la Lwakatare ni fedheha kubwa kwa mwafrika na hakika kwa Mtanzania. Nchi ambayo watu wake wanakunywa uji na mchicha pori, watoto wanasomea kwenye sakafu, wajawazito wanajifungulia chini, maji hakuna, watu lukuki wanaishi kwenye mbavu za mbwa, yooote hayo hawaoni badala yake wanajikita kwenye video za kitoto!

Muda na nguvu iliyotumika kuandaa hii video ya kipuuzi ungetumika kutafuta suluhu ya matatizo yanayoikabili nchi- tungekuwa mbali. Ni aibu na jambo la kujutiwa kwamba tuna watu wazima wanaojiita viongozi wanatumia kodi za walalahoi kwa mambo ya kipuuzi.

Ukiangalia nchi jirani, utaona ni kwa jinsi gani Tanzania tunaongozwa na akili za Kijima! Hakuna nchi hata moja ndani ya Afrika Mashariki yenye hata nusu ya utajiri tulionao, lakini hebu angalia progress yetu! Hebu sikiliza wale tuliowapa madaraka.

Na kama wananchi- wa kawaida hawakuanza kukataa mtindo huu wa siasa za maji taka, tutaendelea kushindia uji na mchicha pori. Ifike mahali tuwaambie wanasiasa tunataka kusikia na kuona wanafanya mambo yenye tija na sio kupoteza muda kuandaa video za kitoto. Upuuzi mtupu.
 
Mkuu hili linasikitisha sana, hakika tunahitaji mapinduzi ya kiraia.
 
Of coz.. huwa naamini tatizo la leo ni dogo kuliko la kesho,so hutakiwi kutishwa na hili wala ksho
 
"Ukweli una tabia moja,huwa haupendi kupuuzwa"

RIP Mwl Nyerere the true son of Africa!
 
asante mkuu huku mtaani kwangu manzese sokoni walikata tamaa...asante kwa kutupatia glucos....
 
Safi sana Yericko Nyerere,Watanzania tumeshajua udhaifu wa serikali iliyoko madarakani,Tumeshajua udhaifu wa chama kinachotawala,Kitu cha msingi ni kuandaa mikakati mpaka vijijini ili tuweze kulinda kura zetu na hatimae Mkoloni Mweusi aweze kuondoka na kutuachia nchi yetu Tanzania tuliyopewa na Mwenyezi MUNGU!..........Tusikubali kurudia mkosa tuliyofanya mwaka 2010 tuliporuhusu kuibiwa kura kwa kutokuwa na mawakala!......Tupige vita kwa nguvu zote amri za kipumbavu kama ile iliyotumika kuzuia matokeo ya Urais kutangazwa vituoni na badala yake kutangazwa na Tume pekee tena makao makuu!....Watengeneze sana video lakini lengo letu wanachadema na WATANZANIA kwa ujumla ni Kuiondoa CCM madarakani ifikapo 2015!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom