ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Ninaposema wanaccm si maanishi mwanaccm anayeishi kijijini anayetembea bila ndala, si maanishi wanaccm wanaotembelea baiskeli. Ninamaanisha wana ccm wenye chama chao.
Kundi la wanaccm waliokosa vyeo ( uwaziri ) na ubunge ( wa kuteuliwa) . wapo wabunge waliojua fika lazima wapate uwaziri kutokana na kujiamini kwamba lazima wawepo, lakini baada ya uteuzi wa awamu ya kwanza kupita wakajipa moyo kwamba kwa kuwa uteuzi bado huenda wakaingia awamu ya pili, lakini baada ya awamu pili nayo kupita kuona hawapo wameanza vikao vya mikakati.
Lakini vilevile lipo kundi jingine lililojipa moyo kwamba wangepata ubunge wa kuteuliwa lakini mpaka sasa raisi kashateua nafasi 6 na bado nne hivyo wameshakata tamaa kupata hizo nafasi nne zilizosalia na kuamua kuungana na kundi la kwanza kuanza figisu figisu.
Lakini kundi la tatu ni lile la wabunge wa kawaida ambao wao hawakuwa na mategemeo ya kupata ubunge wao wanamwona kama magufuri ni mtu asiyetaka maridhiano na wabunge na wanamwona magufuri kama mtu anayejiona amepita kwa nguvu zake wakati wao ndio waliofanya kazi ya kupiga magoti kwa wananchi ili kuwaombea kura madiwani na raisi tena kwa gharama zao binafsi kuna baadhi ya majimbo hawakupata fedha ya chama kabisa , kundi hili linalalamikia kitendo cha boss kuwateua watu ubunge na kuwapa uwaziri watu ambao hawakufanya lolote wakati wa kampeni na kuwaacha watu waliojitoa usiku na mchana kukisaidia chama kushinda.
Tutegemee kuanza kujengeka kwa makundi makundi ndani ya ccm wakati kundi lenye nguvu kiasi kikubwa lipo nje, na kundi lililopo ndani halina nguvu ukimwacha nchemba , januari na Nape lakini wengine wote hawana nguvu ndani ya ccm . Makundi hayo yatajenga mpasuko ndani ya ccm . Kitendo cha kuzuia ziara za nje kwa wabunge na kitendawili kinachosubiri jibu cha kukopeshwa fedha za usafiri kwa wabunge kitaongeza msuguano mkubwa kama raisi atakataa kuwapa fedha walizoomba milioni 150