Wanaccm msitake kutufanya watanzania wote hamnazo

Wanaccm msitake kutufanya watanzania wote hamnazo

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,864
Hii ni aibu kwa watanzania, wanaccm sasa hivi wanahoji kampuni binafsi za uwakili kuwakilisha watu/kampuni dhidi ya serikali, wanaccm hao wanasema kwa kufanya hivyo ni kukosa uzalendo, jamani hii ni aibu kwa, kwa hoja za dhaifu za hivi zinatufanya watanzania wote tuonekane hamnazo.

Hivi kweli mtu anahoji mawakili binafsi kuwatetea wateja wao kwamba sio uzalendo huyo mtu anakuwa na akili sawasawa kweli, hao mawakili Wakikataa kuwakilisha hao watu mnawaona ni majizi ilihali waliwasainisha mikataba wenyewe mtawalipa mishahara nyie?

Hivi kwa hoja dhaifu kama hizi wenzetu wanatuonaje?
 
Ukifikiria sana CCM unaweza pata stroke. CCM kwa sasa ni cancer ya hili taifa, imemaliza rasilimali zetu zote za maliasili sasa imeanza kula rasilimali watu kwa kuharibu ubongo wa vijana wetu
 
ungeweka na mifano na wahusika ili ijulikane unaongelea nini.
naona unaharaka na CCM kuliko hoja yako kwa sababu tu unauhakika utapata wafuasi wa kukutia moyo
 
ungeweka na mifano na wahusika ili ijulikane unaongelea nini.
naona unaharaka na CCM kuliko hoja yako kwa sababu tu unauhakika utapata wafuasi wa kukutia moyo
Wahusika mnajijua mnaosema mawakili kuwatetea Acacia sio wazalendo wakati hao acacia mmewaleta wenyewe.
 
Back
Top Bottom