GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,697
- 109,125
ASIYE NA DHAMBI AWE WA KWANZA KURUSHA JIWE
Mwaka 2004, beki wa kushoto wa Simba, Ramazan Ramazan, raia wa Burundi, aliomba klabu yake imuache huru kwa sababu amepata timu Ubelgiji.
Simba kiroho safi kabisa wakampa barua yake ya kumuacha (release letter) na kumtakia kila la heri.
Viongozi wakatamba kwenye vyombo vya habari kwamba klabu yao ni bora na inafuatiliwa na vilabu vya Ulaya ndiyo maana wachezaji wao wanaonekana na kuhitajika huko.
Baada ya kupokea barua yake, Ramazan Ramazan akasaini Yanga. Hakwenda Ubelgiji wala Belgium....akaenda Jangwani. Kama siyo kurubuniwa ilikuwa nini?
Hebu tuyaache ya 2004, huko ni mbali sana, yawezekana huyu muongeaji hapa alikuwa hajaanza kujua mpira.
Mwaka 2017, Gadiel Michael aliomba klabu yake ya Azam imvunjie mkataba ili aende kutafuta changamoto mpya anakokutaka.
Klabu ikakataa kwa sababu mkataba haunjwi kwa maneno tu...afuate taratibu.
Akaandika kwenye Facebook kwamba Azam wanambania kwenda Yanga ambako ameshasaini pre contract.
Pata picha mchezaji wa timu fulani, na ana mkataba, lakini anapata jeuri ya kutoka hadharani na kusema ameshasaini makubaliano ya awali na klabu nyingine bila klabu yake kujua.
Kama siyo kurubuniwa ni nini?
Mwaka 2020, Sure Boy aliufuata uongozi wa Azam FC kuomba avunje mkataba wake aende kutafuta changamoto mpya.
Klabu ikaamua kumuweka sokoni. Yanga wakaja na ofa yao ndogo...klabu ikaikataa. Siku iliyofuata, yule mtu aliyetumwa na Yanga kuleta ofa, akaleta barua ya Sure eti anaomba kuvunjiwa mkataba.
Kama siyo kurubuniwa, ni nini?
Msimu uliopita, D Ambundo aliiaga klabu yake ya Dodoma Jiji kwamba amepata timu England hivyo wamuache.
Kiroho safi wakamuacha na kumtakia kila la heri...siku iliyofuata, akasaini Yanga.
Kama siyo kurubuniwa ni nini?
Hivi vilabu vyote ambavyo wachezaji wao walirubuniwa, navyo viliumia sana kwa sababu hawa wachezaji walikuwa muhimu kwao.
Ikitokea na Yanga wachezaji wanarubuniwa, wavumilie. maumivu ni yale yale.
Gadiel Michael ni mchezaji ambaye Azam iliwekeza kwake akiwa mtoto mdogo. Mnajua uchungu wake?
Mnalalamika kwa mchezaji ambaye hata hamkuwekeza? Mmemkuta ameshakuwa senior player...vipi mngemkuza nyinyi?
Chanzo: Shaffih Dauda
GENTAMYCINE naomba huyu Zaka za Kazi apewe Ulinzi na ajengewe Sanamu yake kwa Madini haya na Hoja zake hizi Kuntu.
Na kuna Uwezekano mkubwa huyu Zaka za Kazi akawa na Aklli kuliko wana Yanga SC wote walioko ndani na nje ya Tanzania.
Pongezi / Kongole nyingi mno Kwake.