Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,057
- 1,868
Mimi ni mvulana wa miaka 27 ni mhitimu wa chuo cha kilimo.Mwaka jana niliingia katika urafiki wa mapenzi na binti mmoja.kwa kweli yule bint moja ya sababu iliyonifanya nimpende ni msimamo wake.Alisema tusifanye mapenzi mpaka tufunge ndoa.Pili hakuwa kama dada zetu wengine swala la pesa kwake halikuwa ndo mapenzi kwake yaani ukitaka kumpa pesa mpaka uanze kumbembeleza mpaka azipokee.Kwa kweli niliona kwa dunia ya leo niliona huyu alifaa kabisa mke wangu wa ndoa.Kwa kuwa alikuwa na msimamo niliogopa kutangazia umma kwamba nina bint yule.aliyekuwa anajua mahusiano yetu ni rafiki yangu wa karibu na mama mwenye nyumba tu.Pia nilimwambia mama yangu kuwa ikifika mwaka 2014 mapema natarajia kufunga ndoa kwa kweli alifurahi si unajua wakina mama tena harafu ndo mtoto wa kwanza kiume ingawa sikumwambia nafunga ndo na nani.Ilipofika mwezi wa saba alianza kupunguza mawasiliano simu nikimpigia kupokea mpaka atake mwenyewe.Baadae nikagundua kwamba mama mwenye nyumba wangu alimshawishi aolewe na ndugu yake.Je nifanyaje?.