Mgejua kuhusi haki msingemchezea fitna yule Dr wenu
Mgejua kuhusu mizani ya hadaa msingewahadaa Watanzania kwa uchafu wa mtu mwenye followers wachafu
Swala la kupendelea utajijibu mwenyewe mkuu.
Umesema vyema sawa na unavyohisi sawa sawa na wengine kadhaa.
Kwanza ni vizuri Mkajua kwa hakika kua tunaposema Tunataka Mabadiliko tunamaanisha nini sisi Watanzania.
Kumbukeni kua Mungu alituwekea Utarabibu wa Mipaka kati ya Nchi na Nchi. Na utarabibu wa kua na Viongozi ili kuongoza wengine ........Kwa Maslahi ya Wote waliopo na Vizazi vyao Wote bila kua na Upendeleo ili kudumisha Amani nk.
Na ndani ya hizo Nchi akaweka Rasilimali kwa ajili ya Vizazi vyote vitakavyoishi ktk Nchi husika.
Sasa kuhusu Nchi yetu kwa wale wanaojua Rasilimali tulizonazo na namna zinavyotumika, tunaona kuna haja ya kua na Mabadiliko ya Viongozi ili kunusuru Rasilimali zilizobaki tuone namna ya kuziamishia kwenye Elimu Bora,
Afya Maji nk kwa Ustawi wa Vizazi vyetu,
Maana mpaka sasa Rasilimali zilizotumika Haziendani na Maendeleo tulionayo sasa.
Tena kibaya zaidi tunadaiwa Matrilioni ya Shilingi. Kifupi.
Kwahiyo Haki imekua ikivunjwa kwa kiasi Kikubwa sana na Viongozi waliopo Madarakani.
Huyo Dr na wengine kadhaa unaohisi hawakutendewa Haki,
Sivyo unavyofikiri wewe pamoja na wengine kadhaa wanavyohisi.
Ila kilichotokea na kitakacho endelea kutokea ni Mbinu, Maarifa, nk zilitumika, na zitaendelea kutumika ili kuwezesha kushinda "Vita" vya kutaka Mabadiliko.
Na kwa bahati mbaya sana huyo Dr unaenzungunzia Hakukubali Mbinu ya kujishusha ili kufikia Malengo ndipo Mambo mengine yaendelee niwazavyo mimi.
Tena ilikua ni moja kati ya Mbinu bora sana kama huyo Dr angeelewa na kujishusha na kuungana na wenzake na kwenda mbele, leo tungeongea mengine.
Hatakama kulikua na shutuma za Ufisadi ambazo hazikua na Ushahidi wa hakika, maana Hakuna asiekosea. Tena Viongozi hawa wanastahili pongezi kubwa sana=
Freeman Mbowe, James Mbatia,
Emmanuel, Lipumba ingawa hakukamilisha na wengine waliokua Nyuma yao. Ukawa kwa ujumla wao.
Huu ni Mchakato sio kitu cha siku moja.
Pia kumbukeni kua sisi Watanzania hatuwachukii Viongozi waliopo Madarakani, ila tunachukizwa na namna wanavyo-ongoza na namna wanavyotumia Rasilimali zetu na kuwanufaisha Watu wachache na Wageni, huku Watanzania Wakikosa Elimu Bora, Huduma bora za Afya nk, huku wakiteseka kwa Umaskini wa kutisha.
Wakati wanajua kua Mungu amewapa Nchi kubwa yenye Madini ya kila aina, Bandari za kutosha, Ardhi kubwa yenye Rutuba, Mbuga za Wanyama za kutosha, Maziwa yakutosha, Samaki, Wanyama, Milima mikubwa na midogo.
Amani na Umoja ndani ya Nchi nk.
Mungu wangu!!! Nchi imejaa vitu Feki, Madawa ya Binaadam na ya Mifugo Feki, Hospital hazina Madawa, Vyakula, Vinywaji, Madawa nk vilivyoisha muda wa kutumika,
Akinamama wanaambiwa waende na Vifaa vya Kujifungulia.
Tumezungukwa na Maji hadi Ardhini
Lakini akina Mama wanazunguka kutafuta na Watoto Mgongoni mchana kutwa kutafuta Maji.
Wanafunzi wamejaa mabarabarani wamerudishwa kwa ajili ya Ada, Shule hazina Vyoo stahiki,
Shule hazina Vifaa stahiki vya kufundishia, Maabara Hakuna,
Waalimu wengi hawakidhi viwango vya kufundisha.
Vyanzo vyote vya Maji vimeharibiwa, Mipaka yetu yote Wageni Wanaingia na kutoka watakavyo, nk, nk, nk.
Alafu Viongozi hao hao wanakuja na kibwagizo eti HAPA KAZI TU.
Na Watu wanashangilia tu kwa sababu wamenyimwa kujua Haki zao, hivyo hawajitambui.
Tanzania tunahitaji Viongozi Makini haraka iwezekanavyo.
Mwisho napenda kukufahamisha kua kwa sababu nilizojaribu kwa Uchache kuzielezea hapo juu,
Mabadiliko yako palepale pamoja na Mazingira mnayoyaona.
Hakika Mungu Alieziumba Mbingu na Nchi Hatanyamaza hadi atakapotupa Haja ya Mioyo yetu sisi Watanzania tunaoelewa kinachoendelea kwa niaba ya wenzetu walio na "Udhaifu" wa kuelewa kinachoendelea.
HAKI HUINUA TAIFA.
NA PASIPO MAONO WATU HUANGAMIA.
MIZANI YA HADAA NI CHUKIZO MBELE ZA MUNGU.
OLE WA TAIFA AMBALO VIONGOZI WAKE HUDANGANYWA NA KUTAWALIWA KWA SIRI NA VIONGOZI WA MATAIFA MENGINE.
AMANI IWE NA TANZANIA HADI MWISHO WA VIZAZI VYETU. AMEN.