Uchaguzi 2020 Wana Kawe kataeni mateso mengine ya miaka 5

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
WANAKAWE KATAENI MATESO MENGINE YA MIAKA 5.

Leo ningependa kuongea kwa kifupi sana na wananchi wenzangu wa Tanzania wa pale jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam. Nimeona nitoe dukuduku na mtazamo wangu kuhusu mambo mbalimbali ya jimbo la Kawe hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili tushiriki kwa pamoja kuijenga Kawe na Tanzania yetu kwa ujumla.

Baada ya kufunika miaka mitano ya Ubunge wa jimbo la Kawe, hatimaye Mbunge aliyemaliza muda wake ndugu Halima Mdee amerudi kwa ngwe nyingine tena kuomba akitaka achaguliwe na aendelee kwenye nafasi ya Ubunge. Halima Mdee anarudi tena kugombea wakati akijua namna alivyowakosea wana Kawe kwa miaka 5 iliyopita. Naomba twende pamoja kwanza.

Wananchi kipindi hiki ni lazima tuambiane ukweli ili tuwe kwenye nafasi nzuri ya kwenda kufanya maamuzi yetu ifikapo Oktoba 28. Kipindi cha miaka mitano muliyompa ridhaa Halima Mdee tumeshuhudia mambo mengi sana ya aibu na ya kukatisha tamaa ambayo mwakilishi wenu huyu ameyafanya na kutukatisha tamaa sana, mambo ambayo sidhani kama ninyi watu wa Kawe mlimtuma. Sidhani kama yalikuwa makubaliano yenu nae wakati anasimama majukwaani kuomba kura mwaka 2015.

Tumeshuhudia kwa miaka mitano hii Mwakilishi wenu huyu ambae kimsingi alipaswa kupaza sauti kwa mambo ya Kawe, akigeuka mtuhumiwa wa kuripoti polisi kila juma kwa tabia zake za kutaka kushindana na sheria na taratibu za nchi. Alitumia muda mwingi wa Uwakilishi wake kama Mbunge pale Bungeni kusumbuana na polisi na kufukuzwa Bungeni tu.

Lini alisimama Bungeni kuongelea mambo ya Kawe wakati karibu nusu ya kipindi cha Ubunge alikitumia kutumikia vifungo vya kutimuliwa Bungeni na kuhudhuria kesi mahakamani.

Huyo si ndie aliyeshirikiana na Wabunge wenzake kususia bajeti katikati ya kuijadili pale Bungeni. Akasusa kwenda Bungeni kisa Corona. Kwake, yeye ni muhimu zaidi ya wana Kawe. Bajeti iliyopaswa kujadiliwa ili ilete pasu yenu kama wana Kawe akasusa kuijadili na kwenda kujifungia kwa maslahi yake binafsi badala ya maslahi ya wananchi nyinyi wa Kawe.

Amewakosea sana wana Kawe na kuvunja mkataba wenu mlioahidiana wa yeye kwenda kusema shida zenu badala yake aligeuka kituko na mtu wa kufukuzwa kila siku na kukwaruzana na polisi tu. Miaka mitano alikuwa na kesi zaidi ya 10 polisi na kufukuzwa Bungeni. Sasa unawezaje kujenga maendeleo kwa njia hii? Mbunge anayeharibu sheria makusudi ili apate mtaji wa kisiasa. Mara ngapi mmemshuhudia pale Bungeni.

Ni mtu ambaye habadiriki na wala hawezi kubadirika tena kamwe na hayupo kwa maslahi yenu. Mlimpa miaka mitano akafanya madudu, mkampa tena mitano mkidhani atabadirika lakini wapi mambo yalikuwa vilevile tu. Sasa basi achaneni nae, hawafai.

Miaka mitano ya ridhaa yenu kwake amelipa kwa utoro wa kutohudhuria vikao vya bunge na hata hivyo vichache alivyohudhuria pale Bungeni alikuwa mstari wa mbele kupinga kila kitu huku akishiriki pamoja na wabunge wenzake wa Chadema kukataa upitishwaji wa bajeti.

Sasa unawezaje kufanya mabadiriko na kuleta maendeleo wakati wewe ni mtu wa kupinga kila kitu na kukataa kila bajeti inayowasilishwa na Serikali ambayo ndio ilipaswa ije kwenu wana Kawe?

Ana machafu mengi sana wana Kawe ambayo tukisema tuyaseme hapa yote sidhani kama ukurasa huu utatosha lakini mimi niseme tu kwa lugha moja kwamba imetosha sasa. Wote mseme inatosha sasa udanganyifu.

Uchaguzi huu ukakomeshe siasa za kiharakati mlizochezewa kwa miaka 10 mfululizo. Mnahitaji mtu atayefanya siasa za maendeleo zinazogusa maisha yenu ya kila siku kwenye madawa, barabara, maji na mengine kuliko hizi siasa za mtu mnayemtuma kugeuka kituko na kushiriki kufanya harakati zisizosaidia wala kuwapeleka kokote wana Kawe.

Uchaguzi huu una maana kubwa sana kwa wana Kawe. Ni uchaguzi wa kuamua kuchagua maendeleo na kuepukana na hizi harakati na blabla ambazo haziwezi kulipeleka jimbo kokote kule. Ni uchaguzi wa kuamua kupeleka mwakilishi atakayesimama na kupambana kuhakikisha mambo yanafika Kawe kuliko hali ilivyokuwa huko nyuma.

Kazi ni kwenu kufanya maamuzi ya kumchangua mchungaji Josephat Gwajima, mtumishi wa Mungu aliyejipambanua mwenyewe kusaidia watu wa Kawe kabla hata hajawa Mbunge. Mtu mwenye uchungu na Kawe aliyekubali kuweka pembeni shughuli zake zote za kiroho na yote anayoyafanya kuwahudumia wana Kawe.

Tarehe 28 Oktoba mkazime na kumpa adabu huyu mama anayewachezea akili zenu kwa kuwafanya kama watoto miaka na miaka kwa kumchagua Mchungaji mpole, mwenye huruma, maono na aliyejitoa kuwasaidia.

Muda ni sasa na maamuzi ni yenu wana Kawe. Mnyimeni kura zote na mumtume sasa Baba Askofu Josephat Gwajima ambaye kwa namna alivyo mchamungu na chini ya Chama alicho hawezi kamwe kuwaangusha. Ahsateni!

Ni Mimi Kijana Wa Newala, Mtwara.
 
Kawe inahitaji pande la mtu ili iende kwa kasi ya Magufuli Na huyo si mwingine bali n Gwajima wananchi wakawe tusifanye makosa tumchague Gwajima kwa maendeleo ya kawe
 
Kufanya kosa ni sawa lakini mbaya zaidi ni kitendo cha kurudi kosa, wanakawe kwa muda mrefu tumeteseka changamoto zetu zote hazijafanyiwa kazi. Mwanzoni nilikuwa napenda chadema kwa sababu niliamini wataleta mabadiliko na maendeleo lakini imekuwa tofauti sana..kwa sasa sitarudi makosa ya mwanzo
 
Achana na hao wanatoa chuki zao sisi ndo wanakawe na miaka mitano n mingi kama tutampa mtu ambaye hataweza kutuletea maendeleo ni hasara kwetu ni Bora tumchague Gwajima haijalishi watu wanasema nin hayo maneno hata magufuli anasemwa lakin ona mambo aliyofanya hvyo tusimuukumu mtu bila kumpa kazi akafanya
 
Kwa kawaida Watu huwa wanapenda kupinga Halima amepewa nafasi kwa miaka 10 na bado anasema michakato inaendelea ooh mara Magufuli hatoi hela kwa majimbo ya wapinzani kitu ambacho sio kwel kabsa sasa tunataka maendeleo ya uhakika tumchague Gwajima kwa maendeleo ya kawe yetu
 
Back
Top Bottom