Wana JF tusaidiane

Wana JF tusaidiane

Mimi huwa sioni tabu kueleza shida popote ili mradi sivunji sheria. Mungu amenikutanisha na watu wengi humu jf ambao nisingewapatavkwingine. Pamoja na kuwa wapo wenye kejeli ila wakusaidia pia wapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na Mimi nakusupport kwa ujasiri huo wengi wanaona kuomba msaada ni kama kudharaulika wakati si kweli.
 
Na Mimi nakusupport kwa ujasiri huo wengi wanaona kuomba msaada ni kama kudharaulika wakati si kweli.
Ukichukulia kila jambo kwa negativity hauwezi kwenda mbele. Mimi hapa jf kuna watu niliwahi kufanya nao kazi. Wapo tuliofanikiwa na wengine hatukufanikiwa. Chakujifunza ni kwamba, %kubwa ya wanaowakatisha tamaa wenzao huwa hawawezi kutoa msaada wowote hata kama hoja zao zitajibiwa pasipokuacha shaka. Angalia mtu akija humu ana njaa ama abahitaji msaada wa kifedha, utasikia mara andika jina kamili, mara toa namba ya simu. Hata hivyo wakipewa majibu huwanwanaingia mitini.

Nina ushuhuda flani ambao huenda kama kila mtu angekuwa anawaza negatively nahisi nisingeikuwa hapa nilipo. Mwanzoni mwa 2017 nilitoa tangazo kuwa nauza program za computer na printer. Nilipata wateja wengi na wapo walioponda. Kuna mtu mmoja akahitaji software ambayo sikuwa nayo ila nikamwambia kuna mtu anayo. Tukaelewana bei, akatuma pesa yote (zaidi ya 100000). Baada ya hapo nabmimi nikamtumia huyo muuzaji 😲😲😲😲😲 jamaa akanitumia program yenye kuhitaji password+key+email iliyotumika kununua. Kumbe ile program ilikuwa itumike kwa pc si zaidi ya tatu na alikuwa ameishamaliza zote hizo. Kimbembe kikaja kazi imekwama na natakiwa kurudisha hela. Nikipingwa chenga hatari. Niliogopa hata kupokea simu ngeni maana nilijua ni jamaa anabadili namba. Nilikosa amani kabisa, ila nilimuomba jamaa anipe miezi miwil nimtafutie pesa yake wakati nahangaika na mshkaji. Baada ya huo muda kupita bado hali ilikuwa mbaya. Nilitegemea jaamaa atakuja kwenye uzi wangu kuelezea hali halisi ila ilikuwa kinyume. Alikuja kupotea hewani na nilimpata tena baada a kwenda PM. Pesa yake nilimlipa baada ya nusu mwaka ila hadi leo akihitaji software ananiuliza. Hii ilinifanya nipambane zaidi ili nisimuangushe tena mteja yyote. Jf ina members mbalimbali wenye mawazo tofauti. Kuna wanaoamini kisasi ni juu ya Mungu na wengine wanajua ni jino kwa jino. Wapo wasioamini katika umoja na kinyume chake. TUKISHIRIKIANA HAKIKA HATA KWA KUSAIDIANA MAWAZO TU, TUTAFIKA MBALI. Saidia kile unachoweza.
 
Nice
Licha ya JamiiForums kuwa Home of Great Thinkers pia ni forum ambayo member wengi utoa ya moyoni. Wengi humu tunatumia ID ambazo sio rahisi kufahamiana kitu ambacho upelekea mtu kufunguka hata yale ambayo hawezi kuyanena mbele ya jamii iliyomzunguka.

Kwa observation yangu ya nyuzi nazozisoma humu JF na comments za baadhi ya members zinajieleza wazi kuwa kuna tatizo ambalo mhusika anapitia yaweza kuwa kiuchumi, kitaalamu, na hata pia kisaikolojia. Tusisubiri mpaka member mwenzetu akafika katika hatua mbaya ndo tuweze kumsaidia. Unaposoma uzi wa mtu na ukagundua ana changamoto ni vizuri kumsaidia sio lazima pesa hata mawazo yako yanaweza kumpa mwanga.

Usishangae kukuta kuna members humu nyuzi zao zilionyesha wanahitaji msaada wa kisaikolojia wakakosa na kufikia hatua ya kujiua. Mimi ningependa kukumbusha tu JF MEMBERS TUSAIDIANE humu kuna members ni waalimu, madaktari, wachumi, wanasaikolojia na wengine wengi wenye taalamu mbalimbali tusaidiane unapoana nyuzi inahitaji msaada usisite kuutoa.

Fanya dunia kuwa sehemu salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utoto umekua mwingi, kipindi cha nyuma tuli saidiana sana. Members wengi wenye mchango mzuri wamebaki wasomaji tu. Watu wana tukana mods nao hovyo, mtu una amua tu kukaa kimya
 
Back
Top Bottom