BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 5,149
- 14,205
Licha ya JamiiForums kuwa Home of Great Thinkers pia ni forum ambayo member wengi utoa ya moyoni. Wengi humu tunatumia ID ambazo sio rahisi kufahamiana kitu ambacho upelekea mtu kufunguka hata yale ambayo hawezi kuyanena mbele ya jamii iliyomzunguka.
Kwa observation yangu ya nyuzi nazozisoma humu JF na comments za baadhi ya members zinajieleza wazi kuwa kuna tatizo ambalo mhusika anapitia yaweza kuwa kiuchumi, kitaalamu, na hata pia kisaikolojia. Tusisubiri mpaka member mwenzetu akafika katika hatua mbaya ndo tuweze kumsaidia. Unaposoma uzi wa mtu na ukagundua ana changamoto ni vizuri kumsaidia sio lazima pesa hata mawazo yako yanaweza kumpa mwanga.
Usishangae kukuta kuna members humu nyuzi zao zilionyesha wanahitaji msaada wa kisaikolojia wakakosa na kufikia hatua ya kujiua. Mimi ningependa kukumbusha tu JF MEMBERS TUSAIDIANE humu kuna members ni waalimu, madaktari, wachumi, wanasaikolojia na wengine wengi wenye taalamu mbalimbali tusaidiane unapoana nyuzi inahitaji msaada usisite kuutoa.
Fanya dunia kuwa sehemu salama.