Wana JF tukutane mahakamani.

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,788
2,000
Nawaomba Sana wote Kwa umoja wetu kesho asubuhi tukutane mahakamani wakati shujaa wetu Max atakuwa akifikishwa mahakamani Kwa makosa ya uonevu kabisa.
Tuungane tumpe moyo ndugu yetu, mimi nipo mororogo Kwa sasa nilileta biashara hapa jioni ya leo naondoka kuja Dar.
Hata Kama hatutajuana haina shida, ila tuonyeshe solidarity dhidi ya ndugu yetu.
Inashangaza Sana serikali inayojipambanua kupiga Vita rushwa lakini ndo serikali hiyo hiyo inataka imeanza kuvunja Uhuru wa habari, sasa ni chombo gani kitaisaidia serikali kupiga Vita rushwa?
Nayaona mafisadi yakifurahia ujio wa giza la habari ili yaibe vizuri.
Ni vyema rais Magufuli akatambua kwamba, wasaidizi wake hawawezi wote kuwa waaminifu na kumwambia ukweli.
Vyombo vya habari pote duniani husaidia Sana serikali ktk kufichua maovu, ndo maana ktk mataifa yaliyoendelea vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa taifa.
Kutuweka gizani, tukose Uhuru wa kupashana na kupeana habari Kama Korea kaskazini kuna malengo gani nyuma ya pazia?
Ktk historia ya dunia, utawala wa mkono wa chuma haujawahi kufanikiwa popote zaidi ya kuleta vuguvugu la vurugu na kufanya shughuli za kiuchumi kulala.
Palipo na haki pana ustawi na palipo na dhuluma pana chuki na visasi.
Taifa la watu mil 50 hapawezi kuwa na kundi la watu wachache tu wakitaka wabinye maslahi ya walio wengi.
Hiyo Haiwezekani na haijawahi kutokea, ili rais atambue uozo wa watumishi wa serikali ni lazima pawepo na vyombo huru vya habari ambavyo havipo Kwa ajili ya propaganda za chama.
Leo hii magazeti ya serikali hayawezi kuandika habari za waziri X kula mabilioni ya pesa, hiyo ni kazi ya mitandao huru ya kijamii na Magazeti huru.
[HASHTAG]#Free[/HASHTAG] Maxence Melo
[HASHTAG]#Free[/HASHTAG] mind of speech
[HASHTAG]#Free[/HASHTAG] Lema
[HASHTAG]#Bring[/HASHTAG] back Saanane alive
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom