Elections 2010 Wana JF Jiaandaeni Kuchukua Majimbo 2015

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Kwa udhaifu wanaouonyesha wabunge wa chama cha magamba hakika, wasitarajie kurudi tena mjengoni, nalileta hili kwa wale wote wanaopenda kuwawakilisha wapiga kura majimboni mwao wanakotoka, tiketi ipo wazi kama utagombea kupitia chama makini. Nafikiri hapo wanajamvi mnanipata kuwa chama makini ni CDM pekee .

Mimi nalitamani jimbo la Kyela maana mbunge aliyekuwa anaaminika kama mbunge machachari , mchapa kazi mh. Mwakyembe kwisha habari yake, unajua siku hizi simuelewielewi anachofanya ! ni kama yupo hayupo vile !
 
Mimi nataka jimbo la Mufindi kusini maana wananchi ni kama hawana mwakilishi kabisa ila wana jini linalowawakilisha mjengoni!!
Mniunge mkono!

Wana jf tuendelee kugawana majimbo tafadhari!!!!
 
Mimi nilijua hili kuwa humu jamvini kuna vichwa , na ninauhakika vikivamia hayo majimbo halitasalia jimbo labda kwa maana ya uwakilishi na upizani bungeni chama cha Magamba tukiachie majimbo 3 tu, hapo mnasemaje ? tutakuwa tumewaachia mengi au yatawatosha ?
 
2015 Jimbo langu ni Bukoba Vijijini; Tangu Kinyondo afariki dunia Jimbo hilo alijawai kupata Mbunge imara wa kuleta maendeleo ktk jimbo hilo. si Karamagi wala nani kila Mbunge anaeingia ni kushangaashangaa tu.
 
Ni mwendo wa kugawana majimbo tu, na si muda mrefu watapiga kelele hoo ! tumeanza kupokonywa majimbo, eeeh ! tutayatwaa yote. Enzi za magamba kwisha habari yake
 
Mie kwetu Mbinga magharibi nataka kumpiga rapa lile libunge linalosinziaga mjengoni (Capt. John Komba)
 
Duh! Mwisho wa uchaguzi ndiyo mwanzo wa Uchaguzi mwingine.Fanyeni utafiti kwenye hayo majimbo,ili muda ukifika wananchi wapate wawakilishi wa kweli.
 
mimi sitogombea lakini nitatoa support ya kufa mtu kwa yeyote makini atakaye mzava SOKWE hapo bunda ana maana kabisa
 
Hii ya Bunda nimeipenda, VIKWAZO atatoa support ya kufa mtu ili kumuondoa "SOKWE" Big Up VIKWAZO
 
Napita tu, naona mmeamua kujifariji baada ya msongo wa mawazo mliokuwa nao mnanagawana majimbo kama njugu
 
Yote kwa yote tukubaliane kuwa na itikadi moja na filosofi moja, hii itasaidia upashanaji wa habari zenye mwelekeo wa kimageuzi! Naamini na nitaendelea kuamini kuwa kamwe ukiwa ccm huwezi kuwa mwanamageuzi na chama halisi chenye sera thabiti za mageuzi na haki ni CHADEMA!!
 
mimi jimbo la nkenge bk nataka kumpiga chini asunta mshana,nimesha andaa silaha za maangamizi za kumaliza nazo.
 
Hapa si suala la kuamua kugawana majimbo kama "njugu" hivi kwa akili yako unafikiri ukimchukua "Great Thinker" humu jamvini anaweza ashindwe kuyapasua maboga yale ya CCM. Lets wait you will understand later the basis of our discussions

Usikurupuke siasa zinajengwa kwa hoja, unajitathmin then wapiga kura wakikuamini unachukua jimbo, mimi naamini kwa wale waigizaji waliopo pale bungeni kupitia tiketi ya CCM zaidi ya asilimia 70 au 80% hawatarudi, pale wanasinzia kwa mara ya mwisho kipindi hiki maana kazi waliotumwa pale ni kusinzia na mipasho tu
 
Back
Top Bottom