akatanyukuile
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 314
- 308
Mimi ni mhitimu wa chuo fani ya ualimu. Nilimaliza mwaka 2015 kwa mchepuo wa arts. Hivo mimi ni mhanga wa ajira mpya.
Nilivoona maisha yamekwama kijijini nililazimika kujitosa jijin Dar es Salaam kusaka maisha. Nilibahatika kupata kazi ya kufundisha shule moja ya binafsi, baada ya miaka miwili figisu zilikuwa nyingi nikaamua kuachana nao.
Ila kwa muda huo wote nimebahatika kupanga vyumba vyangu viwili na kuhakikisha nimeweka kila kitu kinachotakiwa, na pia nilikuwa ninasevu kapesa kidogo kidogo ambapo kwasasa nina milion 3 benki.
Changamoto inakuja nifanye nini na hizo milioni tatu. Nilinunua pikipiki ikaibwa hivyo sitaki kurudi kwenye maumivu ya pikipiki
Tafadhari mwenye uelewa wa biashara anisaidie nifungue nini ili niweze endeleza kapesa hako ambako ninako. Kwasasa sina kazi nipo tu ninawaza cha kufanya. Nipo Tegeta kwa ndevu hapa.
Msaada tafadhali.