Wana-JamiiForums, karibuni tutajirike

Wana-JamiiForums, karibuni tutajirike

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,549
Kila mtu humu anataka pesa, wengine tayari wamefanikiwa kuzipata kiasi na wengi wetu bado tunatafuta. Sasa nimebuni njia rahisi na nyepesi kwa kila mtu kujipatia pesa kwa urahisi zaidi. Nataka wanachama tuwe 5000 na zaidi, na tucheze upatu, na kila mwanachama awe anachangia sh 500 tu kwa siku. Ina maana 5000 mara 500 = Tsh 2,500,000 kwa siku, wakipatikana wanachama 30,000 itakuwa 30,000 mara 500=Tsh 15,000,000 kwa siku,kwa mwaka ni sawa na sh bilioni 5.4 na tutakuwa tunagawana kila baada ya mwaka.

Tutatengeneza Katiba yetu, ambapo atakuwepo Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina na wanachama.

Karibuni ndugu zangu tuji organize, hili ni jambo serious katika kutoa umaskini uliokithiri miongoni mwetu, nina mawazo mengi sana mazuri zaidi ya hili. Kwa humu ndani, wanachama 30,000 ni rahisi sana kupata. Tutakuwa na ofisi yetu, na tutajisajili kisheria, na tutakuwa na Mwanasheria wetu.

Haya karibuni wadau tuchangie mawazo na tujue tunaanzaje..
 
Ni vizur, ILA tatizo la watanzania Ni ukosefu WA uaminifu sasa,
 
Nani ampe pesa mtu asiyemjua? Aisee hapo hujanishika kabisa.Unaweza kua na wazo zuri ila hao wanachama wengine je?
Ni ngumu kuamini fake ID's.
 
Katika vitu ambavyo sijawahi jaribu hii ni mojawapo.

Na kwa mtu ambae anajua kutunza na kuzungusha pesa simshauri hata siku moja kucheza upatu
 
Unadhani kutajirika huwa ni rahisi kiasi hiki...

Kujua magazijuto pekee haimaanishi unaweza kuwa tajiri kirahisi...
 
Atleast ungesema baada ya mwaka mfungue kampuni yenu lakini kuhusu kugawana bora niendelee na vikoba vyangu
 
Kila mtu humu anataka pesa, wengine tayari wamefanikiwa kuzipata kiasi na wengi wetu bado tunatafuta. Sasa nimebuni njia rahisi na nyepesi kwa kila mtu kujipatia pesa kwa urahisi zaidi. Nataka wanachama tuwe 5000 na zaidi, na tucheze upatu, na kila mwanachama awe anachangia sh 500 tu kwa siku. Ina maana 5000 mara 500 = Tsh 2,500,000 kwa siku, wakipatikana wanachama 30,000 itakuwa 30,000 mara 500=Tsh 15,000,000 kwa siku,kwa mwaka ni sawa na sh bilioni 5.4 na tutakuwa tunagawana kila baada ya mwaka.

Tutatengeneza Katiba yetu, ambapo atakuwepo Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina na wanachama.

Karibuni ndugu zangu tuji organize, hili ni jambo serious katika kutoa umaskini uliokithiri miongoni mwetu, nina mawazo mengi sana mazuri zaidi ya hili. Kwa humu ndani, wanachama 30,000 ni rahisi sana kupata. Tutakuwa na ofisi yetu, na tutajisajili kisheria, na tutakuwa na Mwanasheria wetu.

Haya karibuni wadau tuchangie mawazo na tujue tunaanzaje..

DECI part 2...utawapata tu kiongozi...coz watanzania wengi ni wavivu na wanapenda shortcut katika maisha...kazi kwenu wadau!
 
Back
Top Bottom