Wana iringa wanahoji ni wapi mama mbega alikopata kura 16,916?


mnyikungu

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2009
Messages
1,779
Likes
1,630
Points
280
mnyikungu

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2009
1,779 1,630 280
Ndugu zanguni wana JF uchaguzi wa mwaka huu kilichotokea ni kama mazingaobwe, na isingekuwa nguvu ya umma ya kudai matokeo basi nadhani ndo yangechakachuliwa zaidi ya hapa.
ndugu zangu wana JF leo IRINGA watu kila kijiwe walikuwa wanaongea mengi kuhusu uchaguzi ulivyoenda, lakini kubwa lililotawala mijadala ya wengi je ni wapi mama mbega amepata kura 16,916 yaani matokeo mazima eti kati ya watu 35,614 mgombea wa CHADEMA kapata kura 17,748 wakiachana na tofauti ya kura 832. uchache wa kura alizoachwa mgombea wa si si m ni chache sana ukilinganisha na ushindani ulivyokuwepo. yafuatayo ni baadhi ya matokeo ya vituoni ambayo yatakuonyesha namna huyu mama wa ccm alivyokuwa hakubaliki lakini mwisho wa siku alikataa kusaini matokeo huku baadhi ya kura zikichakachuriwa kwa kumuuongezea ili kuficha aibu yake
Kituo ca stendi kuu-​
Ubunge mgombea wa CCM Monica Mbega (36) ,mgombea wa Chadema,Mchungaji Peter Msigwa (97) na mgombea wa NCCR-Mageuzi Mariam Mwakingwe ( 1)​
Kituo cha Ngome namba moja mgombea ubunge wa CCM Mbega ( 39)Msigwa wa Chadema( 90) na Mwakingwe wa NCCR-Mageuzi ( 5)​
Kituo cha Umati namba moja) ubunge Mbega ( 82) Msigwa ( 120) Mwakingwe ( 5),​
Kituo namba 2 umati huku ubunge Mbega ( 73),Msigwa (114) Mwakingwe(8) na kituo cha umati namba 3 ubunge CCM( 58) Chadema( 64) NCCR-mageuzi(1).​
Kituo cha FFU namba 1 huku ubunge CCM(36) Chadema(68),NCCR-Mageuzi (3) na kituo cha FFU namba 2 ubunge CCM(58)Chadema( 64) na NCCR-Mageuzi (3).​
Kituo cha IDYDC namba 1 nafasi ya ubunge CCM ( 46) Chadema(84) na NCCR-mageuzi (5) na kituo cha IDYDC namba 2Ubunge CCM( 67) Chadema(78) na NCCR mageuzi (7).​
Kituo cha THB na ubunge CCM(75) Chadema(159) na NCCR-Mageuzi (2) kituo cha kituo namba 2 ubunge CCM (87) Chadema(106) NCCR-Mageuzi (8) kituo cha soko la Kitanzini namba 1 ubunge CCM( 70) Chadema(82) na NCCR Mageuzi (1) kituo cha Makorongoni ofisi ya mtendaji kata CCM CCM( 49) Chadema(96) NCCR-Mageuzi (1), kituo namba mbili ofisi ya mtendaji kata ya Makorongoni Urais CCM (81) Chadema(81) ,CUF(2) UPDP(1)Ubunge CCM(78)Chadema(108) na NCCR-mageuzi (5)​
hakika hamna anayekubali hasa ukizingatia mama mbega hajashinda hata kituo kimoja na hapo juu inaonyesha mama mbega alikuwa akiachwa mbali na msigwa ndio maana mwisho wanairinga wanasema japo CHadema imeshinda ila maatokeo bado yamechakachuliwa
 
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
4,413
Likes
417
Points
180
Gsana

Gsana

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
4,413 417 180
Unajua mi nilipata ugumu wapi,ukiangalia kura za vituoni zilikuwa ndogo mno je elfu 17+ zinatoka wapi? Anyway mshindi amepatikana ata kama watazidiana kura 1. Chadema oye!
 
Mchizi

Mchizi

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
1,034
Likes
1,616
Points
280
Mchizi

Mchizi

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2009
1,034 1,616 280
Haya ni matokeo ya vituo hewa ambavyo ndiyo vinampa jk ushindi
 

Forum statistics

Threads 1,238,902
Members 476,226
Posts 29,336,127