Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,488
- 908
Chadema tuongeeni kidogo
Ndugu zangu wanaChadema tumepoteza kabisa welekeo!
Mtu mjinga, asiye na akili, akifeli kwenye jambo lake lolote atatafuta kisingizio. Na mara zote hurushia lawama kwa wengine. Chadema tumefeli! Kwenye uchaguzi huu 2020 tumefeli.
Kwamba tuliibiwa, kwamba tulikosa fedha, kwamba tulizidiwa na masababu yote hayo lakini output ni failure! Tusitafute mchawi nje, sisi wenyewe ndani. Lazima kujitafakari upya. Tatizo ni kiongozi mkuu wa chama.
Kuna damu changa yenye akili inayo chemka, wapewe usukani. Hii tabia ya kung’ang’ania madarakani hata kama boti limezama mwanaume bado uko tu na usukani ukidhani mashetani wataibuka kukuibua ni uzembe wa mawazo.
Mbowe kwenye chama hiki ni jabali, mpiganaji, sio milima miwili au mitatu amevuka na amevusha wengi. Heshima yake lazima ilindwe. Lakini ndio tutakuwa na akili zilezile za kudhani wewe ni bora zaidi na hakuna wa kuongoza chama zaidi yako.
Mimi nampa mbowe miezi mitatu hadi april 2021, atangaze kujiondoa CHADEMA apishe watu wengine na maono mengine na mwelekeo mpya. Hayo ya kusubiri eti mpaka 2024 mbali sana, utabadilishaje mwenyekiti wa chama wakati mna elekea kwenye uchaguzi?
Si ndio ujinga wenyewe huo wa kufelishana, tunajifelisha wenyewe kwa katiba, wenzetu mapema mwenyekiti wao wanamthibitisha mara baada ya uchaguzi ila Chadema tunangojea tume karibia.
Nikisema hivi utaona mjinga anapost we mataga! Hoja kama hizi kila anayetoa hoja makini mnamshambulia. Ni mtu mwenye uchungu na chama anapoona kuna kwa ujinga ulio wazi kabisa, asipopisha mtaniona natoka mzima mzima kumpigia kampeni Rais Magufuli katiba ibadilishwe aongezewe muda na hakuna atakayepinga CHADEMA kwa sababu kama mbowe tunasema ni bora kwenye chama aendelee sasa kwanini tusiseme Magufuli ni bora na aendelee! Miaka mingapi mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA?
Mtei alikuwa mwenyekiti kwa miaka sita(6) tu (1992-1998) Bob Makani akawa mwenyekiti tena miaka sita tu (1998-2004) kisha Mbowe akachukua kijiti hadi leo miaka sasa ngapi 22 tunakwenda yupo tu. Sasa kwanini Rais Magufuli asipewe mingine kumi? Kuna ubaya gani? Kama tabia ndio hii ya kuamini kwamba huyu ni bora kuliko wengine.
Mimi sidhani kama ishu ya Rais Magufuli kuongezewa muda CHADEMA tutaipinga, tutaanzia wapi kupinga! Wakati tuko kwenye boti hilo hilo!
Mjue tunahitaji chama makini, mbaya zaidi siku hizi tumekuwa Wizara ya Afya, yaani tunajichora kupita kawaida. Akili ya kiongozi mkuu wa chama ikishachoka hakuna ujenzi wa chama wala mbinu mpya, zile alizokuwa nazo zote zimegonga mwamba na kabakia kurukia maneno na matamshi ambayo baadae anachoreka!