Wana CHADEMA; Tujisahihishe! Kwa hili Tumeteleza

Wana CHADEMA; Tujisahihishe! Kwa hili Tumeteleza

Mkuu betlehem,
Kitambo sana sijakusikia hapa JF.
This is well noted Mkuu, tunachofanya ni kwenda Sahani moja na hawa Buku 7 Team Lumumba ili kuweza kuiweka sawa record wanayojaribu kuipotosha
 
Last edited by a moderator:
Salaam ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya humu JF kwa siku mbili tatu hizi kwa kweli nimeona jambo ambalo sio zuri..

Mara kwa mara makamanda wa CHADEMA, wamekuwa wakinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba "Akili kubwa hujadili mawazo, akili ya kawaida hujadili matukio na akili ndogo hujadili watu".

Kwa kipindi kirefu, vijana wa CHADEMA na wapenda mabadiliko kwa ujumla wamekuwa wakionekana kujikita katika kujadili hoja na mara chache hujikuta wakijadili matukio.Hali hiyo iliwaweka katika nafasi nzuri kiasi kwamba mtu bila kulaumiwa, angeweza kusema "Wana CHADEMA na wapenda mabadiliko katika nchi hii wengi wao ni watu wenye akili kubwa na miongoni mwao wana akili za kawaida".Hili ndilo jambo kubwa lililokuwa linawatofautisha vijana wa CHADEMA dhidi ya timu ya Lumumba ambayo ni jadi yake kujadili watu badala ya hoja. kusema ukweli.ilikuwa ni jambo jepesi sana kuiangalia hoja ya mtu tu na kuweza kujua huyu ni wa Lumumba, au ni kijana mpenda mabadiliko.

Katika siku mbili tatu hizi; Nimeona na sisi wana CHADEMA. tumejikuta tunaanza kujiingiza katika kujadili watu tena kwa kiwango cha juu kabisa na kuachana kabisa na kujadili hoja.Swali langu ni ikiwa tumeamua kuipoteza hadhi yetu ambayo tulikuwa nayo siku zote? Je! ni kitu gani sasa ambacho kitakuwa kinatutofautisha na watu wa lumumba ikiwa na sisi tunataka kuifuata njia yao?Wana CHADEMA natujisahihishe!. Na turudie jadi yetu ambayo watanzania wote wanaijua kwa miaka sasa.Kutupiana maneno huku sio sahihi.

KUHUSU HOJA YA USALITI NDANI YA CHAMA.

​
1. Ifahamike kuwa suala la kuwa na usaliti ndani ya chama si suala geni duniani, hivyo hamna haja ya kupanic sana.

2. Ikiwa kuna wasaliti;; hata kama mtu unawajua, epuka kuwataja hadharani ikiwa wewe sio mtu mwenye mamlaka ya kiitifaki na kisheria kufanya hivyo.

3. Kama kutakuwa na wasaliti ndani ya chama halafu chama kikawa hakina taarifa za kutosha za kitaalam zinazoweza kuwaajibisha wasaliti, hili ni jambo la hatari na wasaliti wanaweza kushinda na wazalendo wa chama wakaonekana ndio tatizo la msingi.(Wasaliti wakawazidi ujanja wazalendo na wazalendo wakawa na haki ya kulaumiwa).

4.Kama chama kina taarifa za kiintelijensia za kutosha juu ya wasaliti na hakiwachukulii hatua za kisheria kwa mujibu wa kanuni za chama,huu ni udhaifu, na matokeo ya hali hiyo, ni watu kutafsiri kwamba kuna chuki binafsi juu ya wale wanaodaiwa ni wasaliti.

5. Ni lazma chama kiunde mfumo wa kitaasisi wa kuwashugulikia wanaoasi chama na vile vile kuwashughulikia wanaotoa hukumu dhidi ya wenzao bila vielelezo, au bila kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

6.Wana chadema wajiepushe na kurushiana maneno kwani kufanya hivyo kunaleta hasira na mtu akiwa na hasira hatumii akili.Kadhalika kurushiana maneno kunampa adui nafasi ya kusoma udhaifu wa ndani na kuendeleza kuchochea mgogoro kwa maslahi yake.

Mwisho, naomba kwenye uzi huu mtu asitaje jina la mtu na kumshutumu kama huna vielelezo,(kwa kuwa hamna ulazima wa kufanya hivyo na kufanya hivyo hakuna faida yeyote) kinyume chake ; ataonekana ni miongoni mwa watu wenye akili ndogo.


ushauri wako ni mzuri sna isipokuw chadema ci chama cha watz!ni chama cha baba yake lilian,mkileta ujinga mnatimuliwa wotee,chezea mtei ww
 
ushauri wako ni mzuri sna isipokuw chadema ci chama cha watz!ni chama cha baba yake lilian,mkileta ujinga mnatimuliwa wotee,chezea mtei ww
sasa mtei anaingia je kwenye uzi huu? Ok! sawa lakini; uelewa wako umefikia hapo.
 
Mkuu betlehem,
Kitambo sana sijakusikia hapa JF.
This is well noted Mkuu, tunachofanya ni kwenda Sahani moja na hawa Buku 7 Team Lumumba ili kuweza kuiweka sawa record wanayojaribu kuipotosha
Mkuu nilikuwa nimebanwa kidogo ila nipo. Kuna kitu nilikuwa nakiandaa.By kesho au keshokutwa kitakuwepo humu jukwaani.
 
Mkuu Betlehem!!!!

Kwenye hili wamepwaya sana viongozi wakuu mwenyekiti ,katibu na kamati kuu!!!!Hawa ni sehemu ya tatizo na dhambi yao hii itawatafuna wao na chama pia. Wameaminiwa lakini wao kwa hili hawajiamini,viatu vimewapwaya na kama ni mpango wao basi umetumia mbinu sio sahihi,wakati sio sahihi na watekelezaji pia sahihi. Wamefungisha timu katika mchezo muhimu!!!!!!!!

Wanachama ni waoga ,hawana uchungu na hawana mpango mkakati wa kudumu,ni mpaka waendeshwe na viongozi ndio waamke,wanyonge ndani ya chama ila wababe viungani,ni staajabu la mwaka kuandamana kwa vitu vya jirani lakini kwako hata kauli kali hutoi???!!!!Wanachama dhaifu na wamedhihirisha hili!!!!!

Enzi za shule hapa ni kutolewa nje wote hakuna cha monitor wala kiranja kama yupo humo darsani wote shamba kulima mkimaliza kuokota karatasi shule nzima!!!!!

Big disapointment!!!!!
 
Back
Top Bottom