Wana CHADEMA; Tujisahihishe! Kwa hili Tumeteleza

Wana CHADEMA; Tujisahihishe! Kwa hili Tumeteleza

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,199
Reaction score
7,562
Salaam ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya humu JF kwa siku mbili tatu hizi kwa kweli nimeona jambo ambalo sio zuri..

Mara kwa mara makamanda wa CHADEMA, wamekuwa wakinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba "Akili kubwa hujadili mawazo, akili ya kawaida hujadili matukio na akili ndogo hujadili watu".

Kwa kipindi kirefu, vijana wa CHADEMA na wapenda mabadiliko kwa ujumla wamekuwa wakionekana kujikita katika kujadili hoja na mara chache hujikuta wakijadili matukio.Hali hiyo iliwaweka katika nafasi nzuri kiasi kwamba mtu bila kulaumiwa, angeweza kusema "Wana CHADEMA na wapenda mabadiliko katika nchi hii wengi wao ni watu wenye akili kubwa na miongoni mwao wana akili za kawaida".Hili ndilo jambo kubwa lililokuwa linawatofautisha vijana wa CHADEMA dhidi ya timu ya Lumumba ambayo ni jadi yake kujadili watu badala ya hoja. kusema ukweli.ilikuwa ni jambo jepesi sana kuiangalia hoja ya mtu tu na kuweza kujua huyu ni wa Lumumba, au ni kijana mpenda mabadiliko.

Katika siku mbili tatu hizi; Nimeona na sisi wana CHADEMA. tumejikuta tunaanza kujiingiza katika kujadili watu tena kwa kiwango cha juu kabisa na kuachana kabisa na kujadili hoja.Swali langu ni ikiwa tumeamua kuipoteza hadhi yetu ambayo tulikuwa nayo siku zote? Je! ni kitu gani sasa ambacho kitakuwa kinatutofautisha na watu wa lumumba ikiwa na sisi tunataka kuifuata njia yao?Wana CHADEMA natujisahihishe!. Na turudie jadi yetu ambayo watanzania wote wanaijua kwa miaka sasa.Kutupiana maneno huku sio sahihi.

KUHUSU HOJA YA USALITI NDANI YA CHAMA.

​
1. Ifahamike kuwa suala la kuwa na usaliti ndani ya chama si suala geni duniani, hivyo hamna haja ya kupanic sana.

2. Ikiwa kuna wasaliti;; hata kama mtu unawajua, epuka kuwataja hadharani ikiwa wewe sio mtu mwenye mamlaka ya kiitifaki na kisheria kufanya hivyo.

3. Kama kutakuwa na wasaliti ndani ya chama halafu chama kikawa hakina taarifa za kutosha za kitaalam zinazoweza kuwaajibisha wasaliti, hili ni jambo la hatari na wasaliti wanaweza kushinda na wazalendo wa chama wakaonekana ndio tatizo la msingi.(Wasaliti wakawazidi ujanja wazalendo na wazalendo wakawa na haki ya kulaumiwa).

4.Kama chama kina taarifa za kiintelijensia za kutosha juu ya wasaliti na hakiwachukulii hatua za kisheria kwa mujibu wa kanuni za chama,huu ni udhaifu, na matokeo ya hali hiyo, ni watu kutafsiri kwamba kuna chuki binafsi juu ya wale wanaodaiwa ni wasaliti.

5. Ni lazma chama kiunde mfumo wa kitaasisi wa kuwashugulikia wanaoasi chama na vile vile kuwashughulikia wanaotoa hukumu dhidi ya wenzao bila vielelezo, au bila kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

6.Wana chadema wajiepushe na kurushiana maneno kwani kufanya hivyo kunaleta hasira na mtu akiwa na hasira hatumii akili.Kadhalika kurushiana maneno kunampa adui nafasi ya kusoma udhaifu wa ndani na kuendeleza kuchochea mgogoro kwa maslahi yake.

Mwisho, naomba kwenye uzi huu mtu asitaje jina la mtu na kumshutumu kama huna vielelezo,(kwa kuwa hamna ulazima wa kufanya hivyo na kufanya hivyo hakuna faida yeyote) kinyume chake ; ataonekana ni miongoni mwa watu wenye akili ndogo.

Na kuhakishia dr slaa,mbowe hawawezi kukwepa lawama kwenye hili na ndio maana wako kimya.

Kwanini tusiamini hawa vijana na lema kuna watu nyuma yao.
Huu ujinga wao siwezi kukubaliana nao.

Na kwa hili mbowe na slaa hawana sifa ya kuwa viongozi.
 
Tukumbuke kwamba mazoea hujenga tabia, Wenzetu wa lumumba washajizoeza kujadili watu na sasa hii ndio imekuwa tabia yao, Wana chadema wamejizoeza kujadili hoja na hata ikaonekana ndio tabia yao" ni nani basi huyu anayetaka kuivuruga desturi ya watu hawa na kuwafanya waende katika njia ya wale ambao walishapoteza muelekeo na hata wakayapoteza matumaini ya watanzania walio wengi na kujenga matumaini yao kwa CHADEMA? Hatuoni kwamba mbinu za mahasimu wetu ziko katika hatua za awali kufanikiwa hali sisi hatuna habari tunaendelea kurushiana maneno? Tafakari!
 
Na kuhakishia dr slaa,mbowe hawawezi kukwepa lawama kwenye hili na ndio maana wako kimya.

Kwanini tusiamini hawa vijana na lema kuna watu nyuma yao.
Huu ujinga wao siwezi kukubaliana nao.

Na kwa hili mbowe na slaa hawana sifa ya kuwa viongozi.
Mkuu wanaorushiana maneno wapo wengi.Wote wanajijua na ndio maana nimetahadharisha kutoja majina ya watu (kutajana majina hapa hakuna faida kwa chama wala kwa taifa)Tukumbuke humu kuna kila aina ya watu wakiwemo wachonganishi wamo humu humu..Sasa na wewe naona umeamua uanze kujadili watu.Hebu rudia kusoma uzi hadi mwisho.
 
Last edited by a moderator:
Aliyesema watu wasitaje majina ndio yuko mstari wa mbele kutaja majina!!!

Kweli bavicha ni janga kuu...
mchango kama huu kutoka kwa mtu kama wewe ni kitu ambacho nilikitegemea sana.Hongera kwa mchango wako mzuri.
 
Tujiulize ni kwa nini CHADEMA wanapotupiana maneno humu washabiki wakuu ni Lumumba Team? Tufikirieni sana wakuu katika kipindi hiki kabla ya kusema jambo au kuchukua hatua yeyote.

cc Masanilo Bramo Ben Saanane, Yericko Nyerere Molemo Ronal Reagan FUSO OLESAIDIMU Cheche Mtungi Mjuni Lwambo Manyi REMSA at.al karibuni kwa michango yenu.
Mwanzo mwisho unalia lia na Lumumba halafu unataka watu wasitaje majina wewe mbona umetaja majina.

Kama ulikuwa hautaki watu watajwe majina kulikuwa hakuna haja kuleta uzi JF ungepeleka Ufipa mkajadili.

Hivi wewe upo kambi ya nani ya Zitto au Lema.
 
Asante kwa mchango wako mzuri.
 
Mkuu wanaorushiana maneno wapo wengi.Wote wanajijua na ndio maana nimetahadharisha kutoja majina ya watu (kutajana majina hapa hakuna faida kwa chama wala kwa taifa)Tukumbuke humu kuna kila aina ya watu wakiwemo wachonganishi wamo humu humu..Sasa na wewe naona umeamua uanze kujadili watu.Hebu rudia kusoma uzi hadi mwisho.

mkuu umeongea mambo muhimu sana,hakuna haja ya kujibizana mitandaoni, lazima wajue kuwa sisi wanachama tunaakili timamu kwa hiyo tunajua nani mnafiki nani msaliti n.k.Chadema kwa sasa ni taasisi kubwa hao watu hawawezi kosekana,hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi katika swala ambao halina maslahi kwa chama.
 
Na kuhakishia dr slaa,mbowe hawawezi kukwepa lawama kwenye hili na ndio maana wako kimya.

Kwanini tusiamini hawa vijana na lema kuna watu nyuma yao.
Huu ujinga wao siwezi kukubaliana nao.

Na kwa hili mbowe na slaa hawana sifa ya kuwa viongozi.

Ulitaka waongee kitu kama kipi, hebu waongelee kwa niaba ya. . . .
 
Na kuhakishia dr slaa,mbowe hawawezi kukwepa lawama kwenye hili na ndio maana wako kimya.

Kwanini tusiamini hawa vijana na lema kuna watu nyuma yao.
Huu ujinga wao siwezi kukubaliana nao.

Na kwa hili mbowe na slaa hawana sifa ya kuwa viongozi.

Wewe unajua maana ya demokrasia..? Kumbe Mjinga ni mjinga tuu..!!
 
Last edited by a moderator:
Tujiulize ni kwa nini CHADEMA wanapotupiana maneno humu washabiki wakuu ni Lumumba Team? Tufikirieni sana wakuu katika kipindi hiki kabla ya kusema jambo au kuchukua hatua yeyote.

cc Masanilo Bramo Ben Saanane, Yericko Nyerere Molemo Ronal Reagan FUSO OLESAIDIMU Cheche Mtungi Mjuni Lwambo Manyi REMSA at.al karibuni kwa michango yenu.

Mkuu, bahati nzuri sisi wengine hatujaamua ni chama gani tukishangilia, tupo neutral ndo maana tunatwanga kotekote!.

Kwa hili la CDM, kinachowasumbua ni Unafiki ndani ya Chama na Makundi yasiyokuwa na tija. Hakuna sauti moja ndani ya CDM na pia wanahubiri na kusema kila siku kuwa kuna virusi lakini hawachukui hatua kwa virusi "sugu" kama wanavyodai, bali wao wanachukua hatua kwa virusi " hafifu".

CDM wasipojisahihisha mapema, na kuacha majungu, utoto wa kutumia mitandao ya kijamii kushambuliana, basi 2015 watakuwa kama NCCR au CUF!.
 
Ki msingi kwa sasa nikimuona mtu anaendelea kumshambulia kiongozi mmojawapo wa chama humu mtandaoni; huku hana hoja za msingi halafu anatumia verified user au yeye mwenyewe ni kiongozi wa chama. nitamtafsiri tofauti sana kusema ukweli.Tusubirieni vikao vya Chama halafu kama kuna maamuzi yeyote yanafanyika, tutajulishwa ni maamuzi gani na kwa nini. Zaidi ya hapo tutakuwa tumeamua kuingia kwenye mtego kwa hiari yetu wenyewe.
 
betlehem my friend,bado nakubuka mabandiko yako kipindi kile uko lumumba and later on ukajielewa na kuamua kuhamia airtel,niliapa sitakuja kukupa ushirikiano mpk baada ya mwaka mmoja ili niendelee kuchunguza madandiko yako kama bado yana manukato ya lumumba but now naanza kukuelewa kabla hata mwaka haujaisha.

jana kuna uzi niliuleta humu kutoka kwa albert msando na mtu wa kwanza kucoment alikuwa ben na mie bila kupoteza mda nilimuuliza hivi"ben ni sawa kwa viongozi wetu kulumbana kwenye social media" hakunijibu na kwa hili bandiko lako naomba nichukue nafasi hii kuwaomba wenzetu watuelewe kuwa tunakoelekea siko tulikokukusudia,tumeteleza na kwa vile kuteleza sio kuanguka tunaweza jitathimini na kuamka na kuendelea na safari yetu.

ccm kila siku wanasema cdm inakufa,na sie tulivyo wajinga wa akili na ufinyu wa mawazo tumeanza kuomboleza msiba na kupokea rambi rambi toka kwa wageni waalikwa kabla hata maiti hajaitwa maiti,mwenye akili ataelewa nina maana gani ila ujumbe wako nimeupokea na kama ingekuwa posa basi mwanangu wa kwanza ningekupa bila masharti.

"tunakosea njia wakati wa kwenda ila sio wakati wakurudi" TUJISAHIHISHE KWA HILI TUMETELEZA
 
Mkuu, bahati nzuri sisi wengine hatujaamua ni chama gani tukishangilia, tupo neutral ndo maana tunatwanga kotekote!.

Kwa hili la CDM, kinachowasumbua ni Unafiki ndani ya Chama na Makundi yasiyokuwa na tija. Hakuna sauti moja ndani ya CDM na pia wanahubiri na kusema kila siku kuwa kuna virusi lakini hawachukui hatua kwa virusi "sugu" kama wanavyodai, bali wao wanachukua hatua kwa virusi " hafifu".

CDM wasipojisahihisha mapema, na kuacha majungu, utoto wa kutumia mitandao ya kijamii kushambuliana, basi 2015 watakuwa kama NCCR au CUF!.
Ni kweli ni lazma kama kuna virusi, basi virusi vyote viwe scanned lakini kwa utaratibu maalum wa kitaasisi.Sio kila mtu tu anaibuka kokote na kumshambulia yeyote kuwa ni kirusi.Kama mtu ana vielelezo anatakiwa anawapelekea viongozi au analeta mjadala kama concept ya jumla na sio kuleta mjadala wa kumjadili mtu kama mtu.Hii ni hatari sana.
 
Baadhi ya watu waliotoka Nccr na Tlp wana tabia za usugu wa mawazo butu, finyu, mgando na uelewa mdogo wa masuala ya uendeshaji wa shughuli za kisiasa. Chama ni kanuni, sheria na mwongozo. Ikiwa mtu anapata madaraka ya kisiasa na/au mamlaka kwenye chama na akawa hajui chama nini, iko shida sana. Chadema sasa tunatakiwa tuanzishe chuo cha kufundishana siasa na utendaji wa kisiasa, vinginevyo tutapata uzoefu WA KURUDI NYUMA!!
 
Mkuu betlehem, naomba nikuite Kamanda betlehem.
Kwanza naomba nikiri kuwa hii tabia ya kutajana kwenye mitandao kuwa fulani na fulani ni wasaliti, sio tu kwamba nilikuwa naipinga na kuikemea, bali pia ilikuwa inaniogopesha na kunisononesha kwamba inaweza ikavuruga na hatimae kuua tumaini pekee la watanzania, CHADEMA.

Hatimae nimekuja kuielewa na sasa nina support kutaja wasaliti popote hata kama ni kwenye mitandao, nazingatia falsafa ya wenye akili nyembamba kujadili watu, lakini hapa tutawataja wasaliti, si kwa lengo la kuwajadili wao bali kujadili hoja zilizomo katika usaliti wao, therefore, we will be discussing ideas(hoja).

Msaliti ni mtu anayejaribu kuua matumaini ya watanzania, kuna mwanajukwaa aliwahi kutamka kuwa watu wasio na matumaini ni watu wasiokuwa na ndoto, na watu wasio kuwa na ndoto makazi yao ni makaburini. Msaliti ni mtu mbaya mno, ni heri ya adui kuliko msaliti.

Kwa sababu hizo hapo juu, msaliti anatakiwa atajwe popote pale, ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii, umma uelezwe kinagaubaga juu ya usaliti, unafiki na uovu wake, na hatimae chama (CHADEMA)kimtimue. Watanzania wamepoteza viungo vyao, ndugu zao na maisha yao katika safari hii ya ukombozi, leo hii atokee mtu kwa tamaa zake binafsi akwamishe ukombozi, I wont agree, I will stand and fight.
 
Katika hali ya kawaida baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA ambao wanaendekeza kutajana majina kwa kweli si sahihi hata kidogo. Ni udhaifu kuleta mambo ya uzushi kwenye Forum hii badala ya kuitana kwenye vikao ili kuyashughulikia. Naunga mkono hoja ya mleta mada hii maana ni ya busara sana na inalenga kujenga Chama chetu na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom