Wana CCM wenzangu ni wakati sasa tutulie na tuache siasa zipite, ni wakati wa kuyaishi tulioyachagua

Matumona

JF-Expert Member
May 30, 2018
313
434
Enyi wana CCM wenzangu ni wakati sasa tutulie na tuache siasa zipite maana ni wakati wa kuyaishi tulioyachagua. Tusianze chuki na kubehi kwa ndugu zetu wa upinzani na kuwaringishia kuwa tumewanyoosha vilivyo kwenye matokeo ya uchaguzi huu wa 2020.

Ni wakati sasa wa kuungana na kuyaishi maisha kwa upendo na mshikamano kama ilivyokuwa jadi yetu Watanzania. Haina maana kumsimanga mwana upinzani kuwa ataisoma namba wakati vitu vifuatavyo tutavionja kwa usawa kabisa ikiwa haijalishi wewe ulichagua chama gani:

1. Sukari 2800 Tsh @ 1kg
2. Unga 1000 Tsh@ 1kg
3. Umeme 230 Tsh @ kWh
4. Nakadharika nakadharika

Hivyo tuache maisha yetu yaendelee na tuishi kwa amani na upendo.
 
Baada ya ccm kupata ushindi wa kishindo matunda yameanza kuonekana.

Bei ya mfuko wa sementi imeshuka kutoka elfu 15 mpk elfu 8 tu. Sukari imeshuka toka 2400 mpk 1100 kwa kila kilo. Unga wa sembe sasa umeshuka toka sh 1500 mpk shilingi 700 kwa kilo.
 
Kweli mod wametekwa na Kijani.
MTU Kama huyu anaandika Upupu na bado yupo Active tu.
 
Back
Top Bottom