Urais ni Taasisi, cheo cha kijamii, kinaamriwa na jamii nzima na wala siyo mtu mmoja ati mimi ndoto yangu nataka kuwa rais, Jamii haiwezi kunufaika na Lowassa akiwa rais kama vile wengine wanavyofikilia
Tusidanganye wajinga kila siku kwa maneno yale yale!!
Mnufaika wa kwanza kabisa wa urais kiukweli ni familia yake. Ndio maana watu wanatafuta hiyo dili ya uongozi wa juu. Sheria zilizopo zinampa uungu rais wa nchi zetu za kiafrika ndio maana kila mmoja anatamani yule anayempenda ndio awe rais ili wapate pa kutokea na familia zao kirahisi. Hapa hakuna cha utajiri au umaskini ni namna ya kutoka .Mama awe first lady na watoto wawe maprince na maprincess.Kutudanganya kwamba yule anaweza kwa sababu hana fedha au ana fedha ni kutufanya misukule. Tunawasubiri waje tuwachambue kwa hoja.
Lowasa hajaambiwa awe rais bali achukue form. Ndio maana ya kugombea ni ili ashinde yule mwenye hoja na sera nzuri.Mpaka sasa ndoto na hoja ya Lowasa ni maji,Elimu na afya bora kwa wote. Tunasubiri wengine waje na sera na vipao mbele vyao.
Haya mambo ya kushtukizwa tu wagombea ndio yanayotufanya tunawaachia kamati ya watu tisa au kumi walazimishe kwa chuki au mapenzi yao kutupatia rais wa nchi .Matokeo yake anashindwa kufanya maamuzi.
Tunataka sera tuu.Woga wa nini ?Waje wote wenye uwezo tutawasikilize?Kwa nini mtu abebwe na kikundi cha watu wakati hana sera zaidi ya kupinga sera za wenzao?
Hata watoe pesa kama wanavyofanya CCM na makada wake wale wenye akili watasikiliza sera.
Haturudii makosa ya mwaka 2010 ,wananchi walipotoshwa badala ya kusikiliza sera na hoja za wagombea uraisi ili wachague kiongozi bora, waliendekeza nyimbo za kusifiana na mapambo ya CCM .
Dr. Slaa alikua na sera nzuri ya huduma za kijamii na makazi bora kwa wote.Badala ya mgombea wa CCM kuja na sera akaja kwa kupinga hoja za Slaa kwa kusema haiwezekani kwa kejeli nyingi na mifano ya kupotosha.
Imebaki miezi 7 kwa nchi yenye watu makini ni lazima pawe na makundi na watu wanaotajwa kufaa kugombea nafasi ya urais.
Na hakuna mtu atakayejitokeza kugombea urais akakubaliwa na watu wote 100% .Hata akija Yesu atapingwa na kundi lingine.
Kama mpaka sasa pangejua hakuna watu waliotajwa kugombea au kuombwa kugombea basi ningejua hili ni taifa linalosubiri kuzikwa kaburini kwa kuwa taifa la wafu.
Usiwe na shaka atajitokeza unayemkubali wewe ni haki yake ashindane na usiyemkubali. Ndiyo demokrasia ya kweli.