Wana CCM wamtolea uvivu Dkt. Bashiru

Wana CCM wamtolea uvivu Dkt. Bashiru

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,521
Reaction score
96,267
Mjumbe wa NEC mkoa wa Pwani, Haji Juma anasema machache juu ya madhaifu ya Dkt. Bashiru akiwa Katibu Mkuu CCM.

CCM ilikuwa kama nyumba ya udongo iliyopigwa ripu na rangi kwa nje lakini ndani ilikuwa bado ya udongo.

Alibadilika alipo pata madaraka na kuacha alichokiamini na kulinda maslahi yake binafsi na ya aliyemchagua.

Dkt. Bashiru alianza kukidhoofisha chama chetu ndani na kujenga makundi yenye hatari ya ukanda.

Katika uongozi wake vikao vya CCM vilitumika kama rubber stamp tu.

Katika uchaguzi uliopita wagombea wengi walioshinda uchaguzi wa ndani ya CCM walikatwa kwa wingi kuliko wakati wowote tangu CCM ianzishwe.

Robo ya wabunge wote waliopo bungeni hawakushinda chaguzi za ndani ya CCM.

Sasa huo utakatifu wa Dkt. Bashiru unatoka wapi?

Nina mengi sana ya kusema juu ya Dkt. Bashiru.

Screenshot_20210502-131755.jpg
 
Mwaga nyongo mzee kwani ikakaandani ni kama sumu rudia vizuri ukikazia zaidi unamwachia nani hayo mengine.
Alafu usisahau kuchomekea c mbaya kwani hata Nyerere baba wa taifa aliwai kuwaelezea hao watani zake kuwa.. fafanua tu yote.
Wakifunguka siri za ndani ndiyo afya ya walaji wa habari.
 
SEMENI TUUU KWAMBA NYIE MAKANJANJA YA HAPO UFIPANI NDO MNAHANGAIKA BILA KULALA MKIDHANI CHAMA DUME CCM KITABABAIKAA. MNATUNGA PROPAGANDA WENYEWEE HALAFU MNAJIPOST WENYEWEE. MTAPATA TAABU SAAANAA.
MATAGA wewe ukiamka hufatilii habari toka vyanzo vingine ni JF tu? Hii habari mbona ipo kote hata Darmpya wameripoti kwa kumnukuu muhusika! Na huyo katangulizwa tu, wanakuja wengi sana sana kueleza UNYAMA wa JIWE, Polepole na Bashiru.
 
Aisee tutaskia kila aina ya shutuma cha kujiuliza walikuwa wapi tangia mwanzo kuyasema hayo au wanaenda na upepo
 
Tunaposema kuwa Magu alikuwa dhalimu kuna watu walikuwa wanabisha. Aliyoyafanya Magu kwenye demokrasia ya nchi hii ni ushenzi wa hali ya juu. Watu wako kimya lakini yule mtu alikuwa ni shetani mkubwa.
 
Back
Top Bottom