Wamuua dereva wakidai kaiba nyama - Wagawana nyama, wateketeza gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamuua dereva wakidai kaiba nyama - Wagawana nyama, wateketeza gari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Cynic, Jan 16, 2009.

 1. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  This is lawlessness/lack of civil order of highest order. Where is our moral obligation ( at least in layman's terms)?
  ____________________________________________

  Date::1/15/2009 - Wamuua dereva wakidai kaiba nyama - WAGAWANA NYAMA, WATEKETEZA GARI

  Frederick Katulanda, Mwanza

  SI jambo jipya kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi na kumuadhibu, hata kumuua, mtu wanayemtuhumu kwa wizi, lakini wakazi wa Buhongwa jijini Mwanza walienda mbali zaidi walipogawana mali waliyodai iliibiwa na baadaye kuliteketeza gari la mtuhumiwa.

  Walikuwa wamefanikisha mtego wao wa wizi wa ng'ombe uliomnasa dereva wa taksi anayejulikana kwa jina la Johnson Chacha, ambaye anadaiwa kuiba nyama ambayo ilikutwa kwenye gari lake na kusababisha wananchi hao kuamua kutoa kipigo hicho cha kikatili kilichokatisha maisha yake.

  Lakini hawakuishia hapo, wananchi hao wagawana kitoweo hicho na baadaye kuliteketeza gari lake kwa moto kabla ya kulikata vipande vipande na kila mtu kuondoka na sehemu yake, wengi wakionekana kuwa na nia ya kuuza kama chuma chakavu.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:30 jana alfajiri katika eneo la Mtaa wa Shibai, ulio kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana - kama mita 400 kutoka kizuizi cha Polisi cha barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga.

  Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walipata taarifa ya simu ya mkononi usiku wa saa 9: 38 kutoka kijiji cha Idetemya, kata ya Usagara wilayani Misungwi, ikiwajulisha kuwa kulikuwa na wizi wa ng’ombe na hivyo wakaandaa mtego.

  "Tuliweka mtego eneo hili kwa vile tunajua kuwa kila siku wezi wanapoiba, hukipitia eneo hili kukwepa kizuizi cha polisi. Na ilipofika majira ya saa 11:45 gari hilo lilifika

  ndani kukiwa na dereva huyo na wenzake wawili, walipojaribu kupita walikuta

  tumepanga mawe na ndipo walipogeuza gari kutaka kurudi, lakini tulipambana na

  kuwashinda nguvu," alieleza mmoja wa wananchi waliopambana nao.

  "Walipogundua wamevamiwa na wananchi walitoka ndani ya gari na kuanza kukimbia wote na dereva wa taksi aliingia mtaroni na kupita katika kalvati la maji kutoka upande wa pili, lakini alionekana na alipotakiwa ajisalimishe, alionyesha ukaidi na ndipo alipomshambulia kwa mapanga na marungu hadi kufa."

  Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Jamal Rwambow amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa gari hilo aina ya Toyota Chaser limetambulika kuwa na namba za usajiri T 706 ABY na linakisiwa kuwa lilikuwa likiegeshwa maeneo ya Butimba Mkuyuni.

  "Baada ya wananchi kulipekuwa, walikuta likiwa na nyama ya ng’ombe katika

  buti lake, lakini vibao vya namba IBRSPJBO-48 900772 inayodaiwa kuwa ya pikipiki iliyokuwa haijapata usajili hapa nchini," alieleza Kamanda Rwambow.

  Polisi waliofika eneo la tuikio alfajiri kwa ajili ya kutwaa mwili wa marehemu pamoja na vielelezo vingine katika eneo la tukio, walikuta wananchi wakiwa wanakata gari hilo vipande kwa ajili ya kuviuza kama chuma chakavu na walipotaka nyama iliyokamtwa katika gari hilo, walizidiwa nguvu na wananchi na kufanikiwa kutwaa kiasi kidogo cha nyama huku kingine wakigawana wananchi.

  Mmiliki wa ng'ombe aliyeibwa, William Luchemba, 50, mkazi wa kijiji cha Idetemya, alisema ingawa hakubaliani na kitendo cha kumuua mtuhumiwa, amefarijika na kubainika kwa wezi hao kwa kuwa limekuwa ni tatizo kubwa.

  Alisema siku hiyo waliiba ng'ombe wawili, lakini mmoja alikutwa akiwa amefungwa kamba kichakani.
   
Loading...