Wamtaka Obama kugombea Urais Ufaransa

24hrs

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,622
5,952
Nimeshtuka sana na kutikisa kichwa kwa wamarekani wale waliombeza Obama. Sasa France april kuna uchaguzi na wanamtaka kugombea uraisi nchini humo.

Live BBC Mahakama wanaombwa watoe kibali.
 
Ile kazi ya obama aliyotaka kumwachia Hillary Clinton ilipo shindikana naona Obama anatafuta njia nyingine ya kuja kuimalizia yeye!
 
Kuna watu wanapenda O sana kama mleta uzi na BBC hata ile mtandao unaoishia na O unapenda wewe shabiki wa Obama
 
Hizo ni mbinu za kisiasa za kuwaadhoofisha wagombea nchini ufaransa,sidhanikama marekani yenyewe itakubali na cdhan pia kama ufaransa katiba yao inaruhusu
 
Katiba yao inaruhusu raia asiye wa kuzaliwa kuwa raisi? Tena ambaye ametoka kua raisi nchi nyingine?
 
Hicho kikundi cha watu huko ufaransa kinachosema kwamba Obama anaweza kuwa rais wao mzuri hawamaanishi hivyo. Nia yao ni kejeli tu kwamba hao wanaogombania urais wa ufaransa ni takataka tu hawafai.Ni kejeli za kisiasa tu si kweli.Kuna vizuizi vingi sana vitakavyomzuia mtu kama Obama kujaribu kugombea urais si ufaransa tu, hata amerika kwenyewe.
 
Haija wahi kutokea duniani kutoka rais wa nchi moja kwenda kuwa rais wa nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom