Wamezuia wajibu wetu wa Kikatiba, lakini hawawezi kuzuia fikra zetu

Wamezuia wajibu wetu wa Kikatiba, lakini hawawezi kuzuia fikra zetu

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
519
Reaction score
1,463
Leo hii, vijana nguvu kuu ya taifa, chemchemi ya matumaini tumezuiliwa kutimiza wajibu wetu wa kikatiba. Tumezuiwa kuzungumza, kuuliza, kushiriki, na hata kufikiri kwa uhuru tuliozaliwa nao. Swali linabaki: Nchi hii ni ya nani?

Kwa nini tunaishi kama wageni katika ardhi tuliyoirithi kwa damu na machozi ya wazalendo waliotutangulia? Kwa nini kila sauti ya hoja inaitwa uasi, kila swali linachukuliwa kama tishio, na kila ndoto ya mabadiliko inakanyagwa na buti la mamlaka isiyo sikivu?

Serikali ni nani, jamani? Ni kiumbe gani hiki ambacho kimejichukulia nafasi ya Mungu katika maisha ya wananchi? Government is supposed to be a servant of the people, not their master. Lakini Tanzania ya leo, imegeuka maabara ya majaribio ya hofu. Kila kijana anafundishwa kukaa kimya, kila msomi anaambiwa apige magoti mbele ya ujinga wenye cheo.

Hivi kweli, tunapaswa kuishi kama watumwa wa mfumo tulioujenga sisi wenyewe? Constitution siyo karatasi tupu ni mkataba wa damu kati ya wananchi na dola. When the state begins to silence its youth, it is not protecting peace it is suffocating the future.

Angalia vijana mitaani: wenye akili wanaogopa kusema, wenye elimu wananyamazishwa, na wajinga wenye ukaribu wa kisiasa wanapewa majukwaa. This is intellectual genocide the systematic killing of critical thought.

Tanzania inahitaji uamsho. Not a rebellion of violence, but a rebellion of consciousness. Lazima tuamke. Lazima tuhoji. Lazima tukumbuke kuwa serikali si mungu, ni muundo wa kijamii uliopo kutuongoza, si kututawala.

Hatutaki heshima isiyo na haki. Tunataka haki itakayozaa heshima ya kweli. Tunataka taifa linalowapa vijana nafasi ya kufikiri, kuhoji, na kujenga. Tunataka nchi inayosikiliza, siyo inayotisha.

Kwa sababu, mwisho wa siku power belongs to the people, not to the thrones built on their silence.
 
Samuya ametuharibia sana nchi yetu, 9 dec tukomae tumalizane naye & genge lake la wahuni wachache!
 
Back
Top Bottom