Wametumia mabilioni mangapi kucopy report ya Ernst & Young? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wametumia mabilioni mangapi kucopy report ya Ernst & Young?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  Date::9/6/2008
  Ripoti ya Timu Rais Kikwete kuhusu EPA ni ya Ernst & Young
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  MAPENDEKEZO ya Timu ya Rais Jakaya Kikwete iliyotumia miezi sita kuchunguza watuhumiwa wa ufisadi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hayana tofauti na mapendekezo yaliyotolewa na Kampuni ya Ernst &Young iliyokagua akaunti hiyo.

  Timu hiyo iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika na kutumia mamilioni ya shilingi kuchunguza suala hilo, inaonekana kupoteza muda kwa kushughulikia suala hilo na kutoa mapendekezo yaliyokwishatolewa.

  Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanaliona suala hilo kwa sura mbili, moja ama timu ya Mwanyika imekariri ripoti ya Ernst & Young au Rais Kikwete amefanyia kazi ripoti ya awali na kuweka kando baadhi ya mapendekezo ya timu aliyounda mwenyewe.

  Lakini kubwa wanalosema wachunguzi hao ni kwamba, kama mapendekezo hayo yalikuwapo, likiwamo la kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote, kulikuwa na haja gani kuunda kamati mpya na kutupilia mbali mapendekezo yake.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, pendekezo namba 4.5 la Ernst & Young lililoitaka serikali kuendeleza uchunguzi wa upotevu wa zaidi ya Sh42 bilioni zilizochotwa na makampuni tisa limechukuliwa kama lilivyo.

  Mapendekezo mengine yaliyotolewa na Kampuni ya Ernst & Young ambayo pia ndio yaliyotangazwa na Rais Kikwete ni serikali kuweka utaratibu wa kisheria ikiwamo kukamata mali za watuhumiwa kuhakikisha zaidi ya Sh90 bilioni zilizochotwa na makampuni 13 zinarudishwa.

  Mengine ni kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wa BoT waliohusika katika mchakato huo, kubadili utaratibu wa Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Wizara ya Fedha kuanzisha kitengo maalumu kushughulikia masuala ya EPA, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa akaunti ya EPA na BRELA kuanzisha uchunguzi wa makampuni hayo na kuyafuta kwenye daftari lake.

  Baadhi ya wachambuzi wameelezea kitendo cha tume hiyo kushindwa kuja na mapendekezo mapya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma na ucheleweshwaji wa hatua za serikali kuwashughulikia mafisadi.

  Kwa mujibu wa wachambuzi hao, kushindwa kwa tume hiyo kuleta mapendekezo tofauti na yale yaliyotolewa na Ernst & Young ndiko kulikomfanya rais ashindwe kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa hao.

  Hata hivyo, Kikwete alisema alikubali kuwaongezea muda mafisadi kwa kulinda haki za binadamu na utawala bora na sio kutokana na udhaifu wa tume hiyo.

  Alisema amelazimika kuwaongezea muda watuhumiwa baada ya tume yake kumwambia kuwa, wameshindwa kukamilisha kazi kwa muda kutokana na baadhi ya ushahidi wa makampuni hayo tisa kutakiwa kufuatwa nje ya nchi.

  Kwa mujibu wa Rais, uchunguzi huo ulihusu maeneo mawili, wizi wa Sh90.3 bilioni uliofanywa na makampuni 13, ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati batili na makampuni tisa, ambayo yalilipwa Sh42 bilioni ambazo uhalali wake una mashaka.

  Alisema uchunguzi kuhusu Sh 90.3 umekamilika, lakini ule wa Sh 42 kwa ndani umekamilika, bado nje na kwamba, Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kupata taarifa zaidi za watuhumiwa.

  Rais alisema, Jeshi la Polisi kwa kutumia utaratibu wa kusaidiana na majeshi ya nchi nyingine, lilituma taarifa zaidi katika nchi ambazo wahusika wa makampuni hayo wanaelezwa kuwepo, lakini hadi uchunguzi unamalizika hawakuwa wamepata majibu.

  Alisema, tayari watuhumiwa wengi wa Sh 90.3 bilioni kati ya 133 ambazo uchunguzi wake umekamilika, wamezuiliwa hati zao za kusafiria, magari na nyumba zao zimekamatwa.

  Rais Kikwete alitoa hotuba hiyo wakati wingu likiwa limetanda kwani takwimu za fedha zinapingana. Timu awali ilisema ilikusanya Sh60 bilioni na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikataja Sh64 bilioni, viwango vinavyotofautiana na Sh53.7 alizozitaja Rais Kikwete bungeni.


  Ufisadi katika EPA ulibainika kufuatia ukaguzi wa Kampuni ya Deloitte &Touche ya Afrika Kusini, ambayo iliibua katika malipo ya Sh40 bilioni kwa Kampuni ya Kagoda, lakini ghafla BoT ikasitisha mkataba na kampuni hiyo.

  Baadaye tuhuma hizo ziliibuliwa bungeni, serikali ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kutafuta Kampuni ya Kimataifa ya Ernst &Young, kufanya ukaguzi ambao ulibaini ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika hesabu za mwaka 2005/06 ndani ya BoT.

  Kufuatia ufisadi huo, Januari 9 Rais alitangazia umma kuunda timu chini ya Mwanyika na kuipa miezi sita na kutoa baadhi ya mapendekezo yanayofanana na yale ya Ernst & Young.
   
 2. m

  mgirima Member

  #2
  Sep 7, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na very soon itaundwa Tume nyingine ya kufuatilia utekelezwaji wa mapendekezo ya Tume ya Mwanyika.
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Unda tume kufuatilia tume iliyotumwa kutumikia serikali na wananchi. Huu ni ufujaji wa fedha za wananchi. Jamani wananchi tafsiri yake ni "WENYE NCHI" mbona inakuwa vigumu wao kuelewa. Mimi siku zote nasema ngoja tu itafika siku watataka nchi yao. Huu uhuru wa bendera sasa naona unafika mwisho
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  unamaana wame plagiarize au?
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hapa kinachoendelea ni usanii tu hakuna jipya la maana, ni buy time game watu wanasubiri kwa hamu 2010 ifike issue hii ifukiwe na mchezo wa kutuibia uendelee. Kama mtu unakili timamu utajua wazi kuwa tume ya mwanyika ilikuwa usanii tu na ndicho tunachokiona.
   
Loading...