Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,373
Mkuu miaka 50 na mmefanya mengi imekujaje tena?
Mi nilifikiri tunaongelea picha tuu?
Mbona unatumia nguvu nyingi kujinadi?
ni mvivu wa kufikiri usimshangae
Mkuu miaka 50 na mmefanya mengi imekujaje tena?
Mi nilifikiri tunaongelea picha tuu?
Mbona unatumia nguvu nyingi kujinadi?
Imetokana na uwepo wa mengi chanya. yapo mengi mazuri ambayo yamefanyika baada ya uhuru,(ndiyo miaka 50) ambayo hata tukipiga picha zake kukuonesha, nafasi haitatosha. hivyo madhaifu machache yasitumike hukumu mengi mazuri.
Aliye kuwa raisi wa Marekani (enzi hizo) Rais John Kennedy, alisema "...ask not what the government can do for you, ask what you can do for your government", Likewise, Usihoji matumizi ya serikali, fanya kazi yako na timiza wajibu wako mahali ulipo, kama ni ajira binafsi, fanya wajibu wako, kama ni kuajiriwa, fanya kwa bidii, maendeleo yako binafsi utayafikia. na maendeleo ya kila mmoja mmoja, ndiyo maendeleo ya taifa zima.Nani atakaetimiza wajibu wake kama wezi unaambiwa ni akina fulani na evidence ipo unaishia kuwakumbatia, je ni mtanzania yupi leo atakaeonyesha uzalendo ktk madudu haya yanayofanywa na serikali waziwazi? Kwa kweli kama kafanya mazuri ni less than 15% the rest hakuna zaidi ya kuzindua miradi ya serikali tena ya msaada huku wakiwa wamevaa manguo yao ya kijani wakati ni issue ya serikali ambayo inajumuisha wasio magamba (ccd)
Hakuna lolo manake maendeleo yaliopo hayaendani na miaka 50 ya uhuru pamoja na rasilimali tulizonazo mimi nafkiri ni bora tusingepata uhuru manake mkoloni mweupe angetujali kuliko huyu mkoloni mweusi ccm ambaye mpaka sasa anaendeleza baadhi maendeleo yaliyoachwa na mkolon mweupe
Hata hayo hasi yapo mengi ila hiyo picha moja ni sample of millions
Za upande chanya ziko nyingi saaaaaaaana hata nashindwa nipost ipi. kwa ujumla miaka 50, tumefanya mengi saaaaana
Harafu dhaifu anasema hajui kwanini watanzania ni masikini.
Kumbe ni fisadi
Ni kweli, Ng'ombe hawezi kujua umuhimu wa mkia wake, mpaka utakapo katika. Like wise, huwezi kujua umuhimu wa uhuru, mpaka utakapo upoteza. Sisi tulio uona ukoloni, hatuwezi kutamani ukoloni. Ila kwa kuwa umezaliwa wakati wa uhuru, huna cha kufananisha. Kwetu ukoloni tunaujua, na uhuru tuna ujua.
"CHUKIA CHAMA, CHUKIA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI, ILA USITAMANI UKOLONI"
mkuu ukoloni unaoukataa,mbona kila kitu kimebinafsishwa.we wawapi?