Wameshindwa miaka 25 wataweza miaka 5? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wameshindwa miaka 25 wataweza miaka 5?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 16, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Baada ya Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere kusoma alama za nyakati na kuelewa kuwa kwa uwezo wake wa kibinadamu aliweza kuwafikisha Watanzania mahali alipowafikisha aliamua kuachia "ngazi" au kama tulivyoita wakati ule aliamua kung'atuka. Shujaa wangu alitambua kuwa uongozi una kikomo chake cha uwezo wa mwanadamu na vyovyote vile ilivyo alitambua kuwa Tanzania ni lazima itakuja kutawaliwa na watu wengine nje ya yeye mwenyewe.

  Hivyo, akaliandaa Taifa kuwa na viongozi wengine na akamuachia Mzee Ali Hassan Mwinyi kushika usukani. Mwinyi akaingia na Ruksa kwa miaka kumi ya kile ambacho kinajulikana kama ufunguaji wa uchumi wetu kwa sekta binafsi. Hii iliaminika kuwa ingekuwa dawa ya kulileta taifa letu katika mafanikio ya mtu mmoja mmoja. Naye alipomaliza miaka yake kumi akamuachia Mkapa ambaye naye aliingia kwa kubinafsisha taasisi na makampuni mbalimbali yaliyokuwa ya umma kwa nguvu kubwa. Mkapa akawa mtu aliyefungua uchumi wetu kwa wawekezaji wa ng'ambo kwa kiasi kikubwa akisimamia upitishwaji wa baadhi ya sheria mbovu kabisa kuwahi kutungwa na watu huru.

  Alipomaliza naye miaka yake kumi ya majaribio ambayo iliisha kwa mlolongo wa kashfa ambazo hazijawahi kutoka katika taifa hili akamuachia usukani Rais Kikwete ambaye naye aliahidi kuendeleza "mazuri" yaliyofanywa na serikali zilizopita na kuleta mapya kwa kile alichokiita "kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya". Kikwete alipoingia aliingia kwa kujumlisha yale ya Mwinyi (Ruksa) na yale ya Mkapa (Ubinafsishaji) kwa nguvu zaidi lakini akaongeza na ya kwake ambayo ameyasimamia miaka hii mitano inayoisha. Yeye kaja na Uchumi wa Wawekezaji akiamini kabisa kuwa bila ya wawekezaji wa kigeni Tanzania haiwezi kuendelea na hivyo akitumia nadharia ya ruksa (ya Mwinyi) amezidi kufungua sekta na sehemu mbalimbali za uchumi wetu kwa wawekezaji wa kigeni hata katika mambo ambayo ukiyakodolea kwa karibu yanashangaza (kama uchimbaji wa vyoo vya shule!)!

  Kikwete naye kama Mkapa kabla yake amesimamia serikali iliyogubikwa na mlolongo wa kashfa ambazo kuzirudia tena kunaweza kuwa ni kashfa vile vile.

  Miaka ishirini na mitano ya watawala watatu ilitarajiwa ingeweza kufuta na kurekebisha matokeo ya utawala wa Rais mmoja aliyekuwa madarakani kwa karibu miaka 24 hivi. Lakini nusu karne ya watawala watatu mbalimbali wakiwa na faida ya ulimwengu wa kisasa, uliotulia kutoka katika vita baridi, chini ya Afrika iliyo na amani zaidi na mahusiano ya kimataifa ambayo yametengemaa kuliko wakati wowote ule katika historia yetu. Watawala hawa watoto wamekuja na kila mpango na miradi ya "maendeleo" ambayo wameijaribisha. Kuanzia mipango ya "kufufua uchumi" ya miaka ya themanini na mipangao ya MTUKUTA, MKURABITA na MMEM n.k ya miaka ya 2000!.

  Kusema kweli wamejaribu. Wamejaribu kutawala na kufanya yote yaliyo ndani ya uwezo wao. WAmejaribu kurekebisha muundo wa serikali, wamejaribu kupigana na rushwa, wamejaribu kubadilisha elimu ya msingi, sekondari na ya juu, wamejaribu kuleta utawala bora. Naam! Wamejaribu saana kama timu ambayo licha ya jezi nzuri, na makocha wazuri imeendelea kufungwa katika mechi zake mbalimbali hata zile ambazo walitarajiwa angalau kutoka sare. Wamejaribu kuliongoza taifa kwa miaka 25. Na wamefanikiwa katika kujaribu.

  Wamefanikiwa kujaribu kuongeza vitu mbalimbali na ni kweli chini yao idadi ya vitu mbalimbali imeongezeka. Ukiwasikiliza kwa makini utaona wanasifia idadi zaidi kuliko ubora. Kwao wao maendeleo ni kuongezeka kwa idadi. Watasema wameongeza idadi ya vyuo, walimu, shule, majengo, n.k Wameanza kuwa kama Korea ya Kaskazini! Wanajivuna katik akuongeza idadi. Lakini macho yetu yanatufanya tuwe mashuhuda wa kushindwa katika majaribio yao.

  Bado jiji la Dar ni miongoni mwa majini machafu kabisa, bado elimu ya juu ina matatizo makubwa katika ubora na upatikanaji wake, hospitali zetu bado hazijafikia kiwango cha kisasa zikiendelea kuwa mlundikano mkubwa wagonjwa, mipango yetu ya uokoaji bado ni mibovu kabisa kama tulivyoshuhudia juzi mtu aliyekuwa kwenye mtaro kwa masaa ishirini na nne akiojaribiwa kuokolewa kwa njia za enzi za ujima! Katika miaka yao ya robo karne bado kuna watoto wetu vijijini na mijini ambao wanasoma kwa kukalia matofali huku madara yao yakiwa yameezekwa nyasi wakati mtu mmoja anajengenewa jumba analo"stahili" kwa bilioni 3, huku wao wakijigawia bilioni karibu thelathini kila mwaka kwa ajili ya samani na chai huku wakiahidi kuleta bajaji kupeleka mabinti, mama na dada zetu hospitali wakati wa kujifungua!

  Wamejaribu ndugu zangu. Kwa miaka 25 wamejaribu kushindwa na kwa hakika wameonesha jinsi wanavyozidi kushindwa. Kinachoshangaza ni kuwa wanataka miaka mingine mitano ya majaribio mengine makubwa. Yaani wanataka kujaribu kutuahidi kuwa yale ambayo wameshindwa kuyafanya kwa miaka 25 wataweza kuyafanya kwa miaka mitano kwa kutumia viongozi wale wale, wenye sera zile zile wakiongoza na itikadi ile ile ya "majaribio".

  Kumbe swali kubwa ambalo wapiga kura wa Tanzania wanakabiliwa nalo na ndilo kubwa litakalotakiwa kuwaongoza kupiga kura katika uchaguzi huu mkuu ni hili: Je, wanaamini utawala wa CCM uliodumu kwa miaka 25 katika majaribio yaliyoshindwa unaweza kufanikiwa katika miaka mitano? Je, kama wameshindwa kuboresha shule za msingi kwa miaka 25 wataweza kweli kufanya hivyo kwa miaka mitano? Kama wameshindwa kutafuta namna nzuri ya kutoa elimu ya juu kwa miaka 25 ya uliberali wa kiuchumi wataweza kweli kufanya hivyo kwa miaka mingine mitano? Je wananchi wa Dar ambao wanaishi katika mojawapo ya majiji yaliyopangwa vibaya zaidi, machafu na yenye changamoto za kudumu za maji, umeme na usalama kwa miaka 25 kweli wanatarajia kuwa maisha yao yatakuwa tofauti na hali zao kuinuliwa kwa miaka mitano ijayo? Kweli wakazi wa Dar wanaamini chini ya watawala wale wale hospitali ya Mwananyamala, Temeke na Muhimbili zitakuwa bora zaidi miaka mitano ijayo kuliko miaka 25 iliyopita?

  Naam, wapo wanaomini kuwa inawezekana. Naam ni imani tu. Na wengine wataapia kabisa kuwa inawezekana. Lakini msingi wa imani hiyo ni nini isipokuwa njozi kama za Alinacha? Wale wale walioshindwa miaka ishirini na mitano wataweza kweli miaka mitano?
  Waliokataa kufanya marekebisho makubwa ya Katiba miaka ishirini na mitano wataweza kuleta mabadiliko miaka mitano bila mabadiliko makubwa ya Katiba? Walioshindwa kutunga sheria nzuri za uwekezaji na sera nzuri za misaada ya kigeni kwa miaka ishirini na mitano wataweza kweli kuleta mabadiliko katika miaka mitano ijayo?

  Ndugu zangu, tunapoendelea kutafakari ujio wa uchaguzi mkuu ni lazima tujiulize katika dhamira zetu kama tunataka mabadiliko makubwa miaka mitano chini ya uongozi mpya, wenye sera tofauti na za sasa na wenye maono makubwa zaidi au kuendelea kwa kujaribisha watu wale wale ambao tunajua tayari wameshatuonesha kuwa wanashindwa?

  Kama tumekuwa kwenye basi ambalo dereva wake amekuwa akipata ajali za mara kwa mara na kusababisha maafa na majeruhi miaka 25 tuendelee kumchagua dereva yule yule kwa vile ati tumemzoea na kwa vile tayari tunajua kuwa anaweza kupata ajali nyingine au tuamue kumpatia dereva mwingine ambaye anakuja na gari jingine na utaalamu mwingine wa uendeshaji wa gari hilo?

  Katika uchaguzi huu wapo watakaoingia kwenye gari la kwanza kwa vile wamelizoea na wanajua kuwa hata ajali ikitokea wanaweza wasidhurike. Lakini ni majasiri wale wanaotaka kuingia kwenye gari jipya chini ya dereva mpya. Hapo pana tofauti kati ya wenye hofu na majasiri. Kutokana na mazoea wengine watapanda gari la kwanza na hatuwezi kuwashangaa kwani ndilo gari pekee lililokuwepo kijijini kwa muda mrefu, lakini nuru mpya na mwanga mpya umeanza kuangaza, gari jipya lipo kijijini, dereva mpya kashika usukani, anasema twende!

  Waliozoea gari la zamani lenye ajali za mara kwa mara na waende kulipanda kwa furaha, lakini wanaotaka kutafuta njia mbadala wanalazimika kutafuta usafiri mwingine. Kwani, gari lililoshindwa kupanda mlima kwa miaka 25 litaweza vipi kupanda kwa miaka mitano likiwa na dereva yule yule, makonda wale wale na ubovu ule ule? Labda kuna wakati inabidi hata tutumie pikipiki!
   
 2. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Asante M.M Mwanakijiji
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asiye sikia neno mwanakijiji awaambia watanzania ni maskini yeye na familia yake milele
   
 4. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I strongly believe that at this point in this country, we need a president that will not just continue, even with the policies that we have been following in recent years. I think we need a transformational figure. I need–think we need a president who is a generational change. And that's why I'm supporting Dk. Slaa
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Now you are talking...MMKKJ
   
 6. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania is far better off than most African states. In the next 10 years, based on JK plans, if everything works out as planned, we may become among the 30 largest economies in the globe, thus join the G-30 club.
  Vote JK to help us getting there.
  Go CCM
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Miaka 25 wameondoa Landrover vituo vya afya ili wanunue ma VX kwa familia zao. Sisi wanatuahidi wake zetu, dada zetu na mama zetu wajifungulie watoto juu ya baiskeli aina ya guta!
  Miaka 25 wameshindwa kuihudumia reli ya kati iliyomleta mwalimu Nyerere, leo wanataka kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kigoma! bila aibu!
  Miaka 25 bado mwalimu wa shule ya msingi anatoka musoma na Mtwara kuja Dar kufuatilia faili lake ili liende masjala!
  Miaka 25 licha ya kuwa na vyombo vya usalama wameshindwa kukamata wezi waliovunja benki mchana kweupe, tena wanawazawadia nyadhifa, kule kigoma na Muheza watu wanalipa kodi na kuishi kwa dola moja.
  Miaka 25 wameshindwa kuhamia dodoma, bila soni wanaahidi kujenga dubai ya AFRICA kule lake Tanganyika!
  Miaka 25 wanafunzi wanajisaidia katika vichaka, eti wanataka kila mwananfunzi awe na laptop! hata kama choo cha shule kinajengwa kwa msaada wa JICA.

  Kama hatutasema enough is enough, miaka 25 inayokuja watoto wetu watatuandika JF kuwa nasi tulipokea kofia kapelo. Watatusuta kwamba tulimuazima nani akili zetu na je amerudisha! Kama hatutabadilika sisi ni sehemu ya miaka 25 na historria itatuhukumu.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280

  Kwanini unafikiri hizo plans zitafanikiwa miaka mitano ijayo wakati zimeshindwa miaka 25 iliyopita?
   
 9. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Just be patient, dude!!
  We're almost getting there:lol:
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lini tutafika...ishakuwa hadithi ya Bi. kizee na mzigo wa kuni mzito anataka kujitwika...ikawa hawezi kuuinuwa juu, badala ya kupunguza kuni anaendelea kuengeza nyingine zaidi...!
  Ndivyo walivyo CCM...ahadi za miaka mitano iliyopita hazijatekelezwa, wanakuja na mpya...za miaka mitano ijayo...ndiyo mzigo utainuka hivyo? Ni afadhali wananchi wawape wengine tena tuone uwezo wao kwa miaka mitano...hii ndiyo fomula ya ulimwengu mzima
   

  Attached Files:

 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  MMKJ hiyo 25 ni ya viongozi 3, to an avarage of 8.5 yrs/ leader. Inasikitisha kuna wanaoamini 5 mingine maajabu yatatokea, yale yaliyoshindikana 25 yrs ago !!!
   
 12. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  haikufaa rangi chokaa itaweza wapi?
   
 13. n

  nmaduhu Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hata kama ccm tutaipatia miaka mingine 100, bado hali itaendelea kuwa mbovu zaidi, ili tusifike huko tunpaswa kuipumzisha mwaka huu kabla hatujaharibikiwa...
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  tumeshindwa kufika miaka 25 tutaweza kwa miaka mitano? Msingi wa imani hii nini?
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu tutafika lini? Kama 25yrs yameshindikana ni kipi kinakushawishi yatawezekana in 10 years?
   
 16. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Amini nawaambieni mtu ambaye bado anataka kupanda basi la zamani, lazima ni mtu anayefaidika nalo! CCM wametufikisha mahali ambapo hapaelezeki. Sisi tuliona utashi wa kufanya mabadiliko sasa ni vema tujitume na kuyafanya. CCM wamefikia hatua sasa hawajitambui, hawawezi kufanya mabadiliko. Wanahitaji mapumziko ili waone wengine wanafanyaje!!!

  Mimi nawashauri chadema kuongeza kasi kuwaelewesha wananchi haya (kama alivyoyanyambua kaka yangu MKJJ) sambamba na makombora ili wananchi wafunguke!!!

  Kama ni majaribio tumewapa nafasi vya kutosha, sasa basi!!
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Just be patient, dude!!

  We're yet to finish plundering:eek:mg:
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ukiwa umekunywa maji ya bendera ya kijani lazima ufikilie kumpa JK another 5 years of messing arround with our resources
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Ila kuna watu wanaamini kabisa kuwa miaka mitano ijayo itakuwa ni tofauti.. msingi wa imani hii hasa ni nini?
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hatutawapa nafasi ya kuongeza tena miaka kumi natao hilo kosa hatufanyi tena, huo ndio ukweli sasa hivi wote tumepiga kuna wana CCM wanao amini maabadiliko ya kweli mwaka huu hawatoi kura kwa chama chao wengi tuu
   
Loading...