Wameshinda Igunga wameipoteza Tanzania!


Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Messages
2,483
Likes
32
Points
145
Kigarama

Kigarama

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2007
2,483 32 145
CCM wameshinda kura za wapiga kura wa Igunga ila CHADEMA nao wameshinda Imani ya wapiga kura wa Igunga. Lakini vyama vyote viwili fedha waliyoitumia kwenye uchaguzi huo ni kubwa mno kiasi kwamba ni kama vile wameupalilia mchezo wa "aliye nacho" kuongezewa kwenye chaguzi zijazo nchini mwetu.

Igunga ulikuwa ni uchaguzi wa kuijenga upya demokrasia yetu ili iwe tunu kwa taifa zima lakini hilo limeshindikana. Fedha zilizotumika (5bn?) kwenye uchaguzi huo ni nyingi kiasi kwamba zinazidi kwa mbali sana bajeti ya vyama hivyo kwenye wilaya ya Igunga na hata bajeti ya serikali kwenye wilaya hiyo.

Leo hii vyama hivi viwili vinaweza hata kuwekeza milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyama vyao Igunga? Hapa ninachokiona ni kwamba wakiwapo "wenyewe" vyama hivi vitatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya "Ushindi wa chama", lakini papohapo huwa vyama vyao havina fedha vya kujenga chama kama ujenzi huo hauhusishi wakubwa wa vyama hivi. Vurumai ya vyama hivi kutumia fedha zote zile kwenye uchaguzi wa Igunga kumeleta faida gani kwa demokrasia ya Tanzania?

Ni kweli kabisa CCM wameshinda kura na CHADEMA wameshinda Imani ya wana Igunga, lakini wameipoteza misingi ya Demokrasia makini Tanzania! Vyama hivi vimeweka msingi mpya ambao bila fedha hakuna kura!
 

Forum statistics

Threads 1,250,178
Members 481,248
Posts 29,723,306