Wameniibia duka lote la vinywaji

Dogo, Hongera, inauma Sana kuibiwa, tena kila kitu. Anza upya, weka shimo handaki wabaya wako utawakuta wametumbukia humo. Waambie umeweka handaki na ndani yake weka nyoka wa sumu Kali uwaeleze kuwa Kuna nyoka wa sumu Kali.
Furahi sasa umekuwa mtu mkubwa, simaanishi ushirikina bali soma mchezo kwa kina na bandika
Maonyo kwenye ufahamu wa hao wezi. Na badilika kulingana na wao wanavyo cheza mchezo.. Kama ni mbwa weka mbwa, kama ni kuku weka kuku, kama ni camera weka kamera. Kama ni bigula tundika mlangoni.
 
Hizo kufuli za alarm zinapatikana wapi? Vipi bei yake??
Nataka kufungua hardware ila nina la kujifunza kwenye huu uzi!!
 
Hizo kufuli za alarm zinapatikana wapi? Vipi bei yake??
Nataka kufungua hardware ila nina la kujifunza kwenye huu uzi!!
kwan bei mkuu zinaanzia tshs elf 2o tu zinapatikana kkoo
haya ndo ya kisasa ulinzi wa mari zako hapa ni sifuri ni rahisi kuibiwa ndo mana umepata hasara 7bu utategemea KUFURI na kufuri sio mlinzi ukiwa mjuzi haikupi shida dkk 3 tu kushney


haya ndo ya kizamani ulinzi 80% ulijimlisha na hizo lock amazing
 
Elungata Mkuu kwa investment niliyoweka mlinzi alikuwepo sema anasema alikuwa anaogopa kupiga kelele na mara ya pili alikuwa kalala na hao wote walinzi tofauti na hapo hapo nilikuwa na makufuri ya alarm pia.
Embu kwanza anza na huyo mlinzi kumtia ndani wakambinye ipasavyo atasema yote inaonekana anamfahamu mwizi ni nani
 
Angalau frem yangu ina geti la zamani.. Ngoja nitafute hizo kufuli asante mkuu!!
 
hapo hakuna haja ya kumtoa m2kafara huyo mwizi mnamahusino tena ya karibu maana haiingii akilin mtu asie kujua akaja kuiba mali zako zote
 

komamgo Nashukuru sana mkuuu comment yako lakini umeiandika kiana kabisaaa na kiutofauti ila umeeleweka asante sana kaka nashukuru sana kwa hilo na wazo lako roho inauma sio kidogo na ukiangalia nimemwaga hela nyingi sanaaa...wamechukua kila kitu hamna kilichobakia...Asante sana kwa mawazo yako ila ukifafanua zaidi nitashukuru sana
 

Mzimu wa Kolelo Nashukuru sana kwa hili asante sana tena sanaa really appreciate hapo tatizo nilikuwa na geti jipya sio haya ya zamani hilo hapo ni kila kitu kuvunja hawawezi kabisa na ulinzi hapo umekamilika nadhani next step nitafanya hivyo itabidi nijiweke vizuri kwa kuweka tu geti lile la zamani nadhani hiyo ndio idea nzuri
 
Embu kwanza anza na huyo mlinzi kumtia ndani wakambinye ipasavyo atasema yote inaonekana anamfahamu mwizi ni nani

iJamii Nashukuru sana nimejaribu kuomba msaada wa police wamesema hawawezi kunisaidia kwa lolote maana sina ushahidi wowote ila wenyewe ndio wakutafuta na kufanya investigations na sio mimi sema msaada nimekosa kila mahali. ila najuwa lazima mlinzi atakuwa amehusika hapa sio bure lazima atakuwa anajuwa kila kitu kinachoendelea....
 
Angalau frem yangu ina geti la zamani.. Ngoja nitafute hizo kufuli asante mkuu!!

gwankaja Hongera sanaa mkuu weka mapema hizo kufuli ila mimi nilikuwa nalo moja ila nililikuta wamekata wameweka mezani na mpaka leseni ya duka walichukua na yenyewe...
 
Weka mlinzi kutoka makampuni makubwa yaliyosajiliwa. Makampuni haya ukiibiwa ni jukumu lao hivyo wako makini na walinzi wao

truckdriver Asante sana ni wazo zuri sanaa ila kama ni hivyo itakuwa gharama kidogo maana kuna fremu zingine so naona gharama itakuwa kwangu sema itabidi nifikirie...
 
hapo hakuna haja ya kumtoa m2kafara huyo mwizi mnamahusino tena ya karibu maana haiingii akilin mtu asie kujua akaja kuiba mali zako zote

valangati Ni kweli kabisaaa hujakosea unachosema maana hata muuzaji amekuwa na wasiwasi sana na anaogopa sana sema itabidi kuangalia nini cha kufanya maana haiwezekani mtu atoke sehemu nyingine aje kuiba sehemu asiyojuwa.....
 
mkuu ukitaka kutengeneza hilo geti nicheck nikueleze hizo lock nadhani ni msaada mkubwa sana zitakusaidia unatakiwa umuelekeze fundi wakati anatengeneza hilo geti jinsi ya kuweka
ila yote ni katika kujihami tu ila wezi wanambinu nyingi wakiamua
ila ukijidhatiti watakuogopa ukitaka unaweza ukatega UCHAWI
 
Mkuu dagii tafadhali naomba tuwasiliane nitumie number yako ili niweze kupata msaada wa camera na ndio nimeamua hivyo kuweka camera sasa hivi,inauma sanaaa acha tu sina namnaaa
Camera sio kitu mkuu camera sio suluhu,angalau kuweka mlinzi, maana anaekuibia inawezekana ni mtu wa karibu sana, na ameshakuona una kauzembe fulani cha kudhibiti mali zako na ndo maana anarudi kila wakati, ukiweka camera utajidanganya atatafuta njia tofauti kama kuvaa mask nk,
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…