tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,134
- 280
Katika harakati za kujisafisha ili kuleta mvuto kwa wananchi, baadhi ya vigogo katika Chama Cha Mapinduzi wamepewa siku 90 kujiengua. Swali ninalojiuliza ni kwamba wameambiwa waondoke katika chama au ni katika nyadhifa mbalimbali walizonazo? Kama ni kujiengua katika chama ni chama gani kitakachokubali wajiunge nacho? Ngoja tusubiri kwani siku zinahesabika.