Andiko lako laonesha unawapenda waarabu hadi unatamani uanze kulia. Hongera sana!
Maneno yapi hapo yanaonyesha nawapenda Waarabu?
Najaribu kusema ukweli kwa kadri nielewavyo, full stop
Nathamini weus wangu. Hao Waarabu au wazungu naona ni binadam wenzetu tuliotokea kukaa nao hapa dunian. Sisi na wao wote tuko sawa. Tunatofautiana katika rangi, lakini,na vitu vingine kama imani
Unaonekana unawapenda wazungu kindakindaki, na utakuwa mkristo wew inavyoonekana. Na hili si kosa lako. Haya mambo yalianza zamani. Ukikutana na mweusi mwenzako asiye mkristo utakuwa una fikia hata kumhujumu, kisa sio mkristo. Utamkaribisha na kumhudumia vizuri mzungu. Lakin utamnyanyapaa mweusi mwenzako kisa imani yake. Ni kama mwislam mweusi anavyoweza kumuona mweusi asiye mwislam kama kitu kilichopotea.
Huu ukristo na uislam tuliletewa na wazungu na Waarabu. Kabla hawajaleta hizi dini tulikuwa na dini zetu. Walipofika kwa ushawishi na kwa nguvu mara nyingine, walitubadilisha dini zetu. Wakawa wanasema zile ni za kishenzi, sio dini na nk. Babu na bibi zetu walilishwa kasumba hiyo kwa miaka mingi mpaka ikazoeleka. Uongo ukirudiwa rudiwa unakuwa ukweli.
Maeneo makubwa afrika yaliyo kaliwa muda mrefu na wazungu ndo kuna wakristo weng. Na kulikokaliwa muda mrefu na Waarabu ndo kuna waislamu wengi. Kama wew ni mkristo usiwachukie Waarabu na waislamu weusi kwa maana saa hizi wew ungekuwa mwislam kama Waarabu wangekuwa wamepata kutuama Maeneo utokako kwa miaka mingi. Na hata kwa mwislam ndo hivyo hivyo usiwachukie wazungu au wakristo weusi Kwasababu wew sio mkristo sana sana ni Kwasababu maeneo utokako wazungu hawa kuweka makazi kwa kipindi kirefu
Hii imetugawanya mazima katika makundi mawili Makubwa. Kabla ya hapo naona vilikuwa vikundi vya kikabila au kieneo na namna yao ya kusali.
Kwa kiasi kikubwa Wachina na wajapan wana dini zao, yaani sio wakristo na si waislamu na wazungu na Waarabu wanaishi nao poa tu. Muulize mzungu, je, kati ya Mchina au mjapan asiye mkristo na mweusi mkristo yupi wa maana? Atakujibu kuwa ni Mchina au mjapan na 'upagani' wake. Hivyo hivyo kwa mwarabu
Kuwa mkristo au mwislam au kuwashobokea wazungu au waislamu hakukufanyi wa maana. Zaid zaid inatudhalilisha na kutufanya tunyonyeke zaidi..
Mpaka hapo tutakapo jifunza kuwa hapa duniani kila mtu na lwake ndio tutaheshimika