Wamarekani mwaka 2020 wataamua hivi kwa Rais wao Trump, ila sijajua Waafrika nao kwa mwaka 2020 wataamua vipi kwa Marais wao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,734
2,000
Imegundulika ya kwamba kwa jinsi Wamarekani walivyokuwa na Hasira na Chuki za ' Kutukuka ' kabisa kwa Rais wao Donald Trump ambaye walikuwa na ' Matumaini ' nae makubwa sana baada ya kuonekana atakuwa ni ' Tiba ' ya mambo mengi ya Kipuuzi yaliyokuwepo hapo sasa kama pakitokea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 basi Wamarekani 57% si tu hawatampigia ' Kura ' bali hawatapoteza pia muda wao ' adhimu ' kwenda Kujipanga Mstarini Kumchagua.

Huyu ni Rais wa Marekani ila sijajua kwa Marais wengine hasa wa hapa Barani Afrika na Wao mwaka 2020 watakosa Kura asilimia ngapi kutoka kwa wale waliowachagua na walio na hasira nao kweli kweli ambapo inasemekana wengine kwa jinsi walivyochoka wana hamu hata Uchaguzi Mkuu uwe leo.

Bora Mimi hapa nilipo nchini Nicaragua kwa jinsi Rais wetu huyu ambaye kabla hajawa Rais hivi alikuwa ni Mchapakazi mzuri mno katika Nafasi zote za Uongozi alizoshika hivyo Wananchi wa hapa wamesema kuwa kwa Maendeleo haya ya haraka aliyoyafanya ya Kujenga Miundombinu, Hospitalini kuna Dawa zote, Maji yanapatika Nicaragua nzima, Elimu ni bure na hata Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanapewa Mikopo wote, Kodi inakusanywa na inatumika vyema, Mfumuko wa Bei hakuna kabisa, Wananchi wana raha, amani na furaha, nchi imemaliza Madeni yake yote na WB na IMF, Shule zote Wanafunzi wanakaa katika Dawati moja moja na kila Mwanafunzi anamiliki Laptop yake, Mazao yanauzwa vizuri na Wakulima wote wana furaha na Serikali ya hapa inawajali kama ambavyo hata Yesu Kristo na Mtume Mohammed wanawajali ' Wapendwa ' wao na Ujambazi na Mauwaji nayo pia yameisha na hayapo kabisa hivyo watampa Kura zake zote 100%.

Karibuni sana Nicaragua Wapendwa!

Nawasilisha.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,405
2,000
Huyu Trump wa Bongo akijitahidi sana atapata asilimia 20 ya kura zote panapo Tume Huru.

Mijini hakubaliki, vijijini hauziki!!

Ile kete yake ya kujinadi kuwa anapambana na ufisadi sasa nayo imeingoa doa la wazi hata vipofu nao sasa wamegundua na hii ni kutokana na yeye kutaka kumuondoa SIEIJI.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,044
2,000
Huku Africa na hasa hasa hapa Tanzania.. Rais "uchaguliwa" kwa "matokeo" ya uchaguzi unaoshirikisha idadi yoyote ya waliojipanga kupiga kura..
Wawe 1/4 au 1/8 au hata 1/12 ya waliojiandikisha au raia wa nchi husika bado tu mshindi atapatikana na hafla za kusimikwa zitafanyika tu..!!
 
Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
599
1,000
Imegundulika ya kwamba kwa jinsi Wamarekani walivyokuwa na Hasira na Chuki za ' Kutukuka ' kabisa kwa Rais wao Donald Trump ambaye walikuwa na ' Matumaini ' nae makubwa sana baada ya kuonekana atakuwa ni ' Tiba ' ya mambo mengi ya Kipuuzi yaliyokuwepo hapo sasa kama pakitokea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 basi Wamarekani 57% si tu hawatampigia ' Kura ' bali hawatapoteza pia muda wao ' adhimu ' kwenda Kujipanga Mstarini Kumchagua.

Huyu ni Rais wa Marekani ila sijajua kwa Marais wengine hasa wa hapa Barani Afrika na Wao mwaka 2020 watakosa Kura asilimia ngapi kutoka kwa wale waliowachagua na walio na hasira nao kweli kweli ambapo inasemekana wengine kwa jinsi walivyochoka wana hamu hata Uchaguzi Mkuu uwe leo.
mkuu kwani waafrica wote wanauchaguzi mkuu 2020???sema wananchi wa Venezuela wataamuaje 2020???
 
Timm Wu

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
506
1,000
CCM imekufa, hawashindi chaguzi bali wanapindua matokeo halali ya viongozi waliochaguliwa...imagine Shwain wa Zanzibar naye anajiona Rais eti
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,042
2,000
CNN walisema hatashinda, wameendelea kuwa na ugomvi nae hadi leo. watu wakasema kwenye uchaguzi mdogo uliopita watapoteza viti vingi sana, amevuka. Marekani na sisi tuko tofauti sana.

Nimesukiliza BBC wanasema viongozi wa maziwa makuu wamekutana Ethiopia kujadili matokeo ya urais Congo, pale ukimuuliza kila mshiriki ni nani yupo madarakani kihalali hakuna atakaenyosha mkono kwa ujasiri. Pale kilichohuswa ni maslahi ya watu.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,734
2,000
mkuu kwani waafrica wote wanauchaguzi mkuu 2020???sema wananchi wa Venezuela wataamuaje 2020???
' Sindano ' hii haikuhusu hivyo kaa Kimya iwaingie inaowahusu. Nchi ninazozijua ni Kisiwani Puerto Rico na hapa Nicaragua nilipo.
 
Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
599
1,000
Wamarekani si watu wa kuwaamini,watamrudisha tu Trump
hahahahahaaaaa, hadi huko nicaragua mmchoka???mm huku Puerto Rico nimesanda,kijana wangu mmoja anasema akipata kibali anajiunga,amekata tamaa kiasi kwmba anaona hana cha kupoteza
 
Charles Dotter

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,199
2,000
mkuu ya USA waachie wenyewe, we endelea kutabiri ya tz

trump 2016-make america great again

trump 2020-make america safe again
 
Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,665
2,000
Huyu Trump wa Bongo akijitahidi sana atapata asilimia 20 ya kura zote panapo Tume Huru.

Mijini hakubaliki, vijijini hauziki!!

Ile kete yake ya kujinadi kuwa anapambana na ufisadi sasa nayo imeingoa doa la wazi hata vipofu nao sasa wamegundua na hii ni kutokana na yeye kutaka kumuondoa SIEIJI.
Tume huru ni mali ya ccm usijifanye kusahau
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom