Wamarekani Kuibeba Soka Ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamarekani Kuibeba Soka Ya Tanzania

Discussion in 'Sports' started by Ab-Titchaz, Nov 9, 2008.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #1
  Nov 9, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wamarekani Kuibeba Soka Ya Tanzania


  Na Jessca Nangawe

  MAKAMU wa Rais wa Chama cha Soka Marekani cha The New England Revolution, Craig Tornberg amewasili nchini kwa lengo la kutengeneza mahusiano na ushirikiano katika soka baina ya Tanzania na Marekani.


  Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF, Fredrick Mwakalebela alisema wadau hao wa soka wamekuja nchini kwa lengo la kuendeleza mchezo wa soka pamoja na kubadilishana mambo mbalimbali katika soka ikiwa ni sehemu ya kubadilisha uzoefu.


  Alisema tayari wamekutana na viongozi wa serikali pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ambapo wamekubaliana kushirikiana katika mpango huo kukuza soka ya Tanzania ikiwa ni kupeleka baadhi ya wachezaji wa hapa nchini Marekani kucheza michezo ya kirafiki.


  Mwakalebela alisema baadhi ya viongozi kutoka Wizarani wataondoka nchini Novemba 15 kwenda Marekani lengo likiwa kupata uzoefu na kuangalia viwanja vitakavyotumika katika michezo mbalimbali itakayochezwa huko.


  "Tumekubali kushiriki mpango huu kwani kwetu utakuwa na umuhimu mkubwa kwa kupandisha soka letu na kutakuwa na majaribio kwa wachezaji wetu kabla ya kuon doka kwenda huko vilevile wachezaji wa huko watakuja huku ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika mpira,"Alisema Mwakalebela.


  Naye Craig Tornberg alisema wamekuja Tanzania kwa kutengeneza mahusiano mazuri ya kimichezo na timu za Tanzania na lengo kubwa ni kupanua wigo wa kimichezo kwa nchi za Afrika hasa kwa vijana wenye umri mdogo ili kuwaandaa kuja kuwa wachezaji wakubwa kama zilivyo nchi za Ulaya.


  Timu zitakazoshiriki katika mpango huo ni timu ya taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu pamoja na timu za vijana.

  Mwananchi Read News
   
 2. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mh..!US...na soka wapi na wapi?, anyway karibuni huenda tukapata vijana wakasajili na Gallaxy kwa Becks,'.. bila kusahau 'misaada' yahapa na pale (i guess kwa TFF/Mwakalebela that's his priority number one behind the scenes'..,'
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu walibebe soka lao kwanza kabla ya la Tanzania. Wangesema wanataka 'kutubeba' kwenye Basketball hapo ningeamini.
   
 4. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #4
  Nov 10, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  BAK,

  I think they are more about funding the whole exercise and while doing so
  poach some talent for their Pro League.Hapo nadhani vijana wabongo
  wakiwa ngangari basi 'wataibeba' hiyo soka ya marekani.Basically they wanna
  use our talent to better their league.

  Ni mtazamo wangu.
   
Loading...