Wamalawi washitukia Tanzania na maandalizi ya vita!!

Kumbe kuna watanzania wapuuzi kiasi hiki?

Hapo kichapo kwanza mazungumzo baadae, hiyo treaty inawahusu wajerumani na waingereza wenyewe labda waje na ramani iliyochorwa na Mungu, vinginevyo ziwa ni letu sote na kama kuna kiongozi atakubali kuliachia ziwa kwa namna yoyote basi damu ya watanzania itakuwa juu ya kichwa chake na vizazi vyake, hizo sheria za kimataifa hazitumiki kwa wayahudi na wapalestina?

Watanzania bora tufe kuliko kuishi bila ziwa Nyasa.

Ha ha haaa.. Aisee .. Na mie naongezea watanzania bora tufe kuliko kukosa twiga wanaoibiwa... Ha ha haaa.. Ngojea niongeze tena.. Bora tufe kuliko Kuwa wa mgao Wa umeme. Ha ha haaa!!! AKILI nyingine jamani,!!
 
Mimi naona mtazamo wako ndio wa kilevi kwa sababu mtu anakuvamia nyumbani kwako mbele ya mkeo na watoto unamwacha achukue mali zako halafu unasema unampeleka mahakamani, mahakamani my foot.

Yeye alipokuvamia alipitia mahakamani? Yaani wao Malawi wameingia kwenye mipaka yetu wanarusha mpaka ndege ndani ya mipaka yetu hiyo sio kukosa busara, kukosa busara ni kumwambia aache uchokozi vinginevyo tutampiga!!!!!!!!!!!!!!!

Hata kama kuna kosa lililofanyika wakati huo wa kugawa hizi nchi, kwanza lazima kuheshimu mipaka iliyopo then waweke hoja mezani zijadiliwe wakiwa hawajaanza kutuchokonoa.

Na baadaye watasema tusijadili maana kesi ipo mahakamani, so they are making the most of it.
 
Sasa kipi kilianza mkataba wa Heligoland au hii sheria ya kusema mpaka uwe kati kati ya maji?

Na je Mkataba huu unaosema mpaka uwe kati kati ya maji una exceptions kama anazozisema waziri wa Malawi?

I think malawians have taken this personal because of oil and gas...lets wait and see what would come up from the so called wasuluhishi.
 
Principle yangu kwenye masuala ya viwanja ni kuwa, ukiingilia kiwanja changu natumia nguvu yeyote kukuondoa, ili kama ni mahakani uende wewe.
Tuko katika hili tuko pamoja sana.
Hata mimi nilitarajia kwamba hadi wakati huu hakutakuwa na chombo chochote cha utafiti ama cha kijeshi cha nchi ya malawi kinachozagaa zagaa ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania ndani ya ziwa nyasa. Kwahiyo mazungumzo yataendelea huku kila nchi ikiendelea kumiliki nusu kwa nusu hadi hapo suluhu itakapofikiwa.

Kuwaacha wamalawi waendelee kuzurura ndani ya eneo letu ni sawa na kukubali kuporwa eneo letu, sasa sijui tunakwenda kuzungumza nao kitu gani. Kwakuwa wao ndio wanadai kwamba sisi tumewadhulumu eneo lao ilitakiwa tuwafurushe ili wao ndio waende mahakamani au kuomba mazungumzo. Lakini sasahivi ni kama sisi ndio tunawapigia magoti kutaka eneo letu la ziwa nyasa.
 
Last edited by a moderator:
Eneo la NCHI yetu linamuhusu mkulu.. Kila kitu yeye anapiga kimya.. Sasa Kwa hili mkulu unapaswa usemee kitu watz tujue kinachoendelea Na si kila saa wananchi wengine wanapwayukapwayuka tu.. Tunatiana hofu kila kukicha, vita nani asiyeijua.. KamA hujui nenda kawaulize wakazi Wa gongo.. Mtu anapwayuka tu tupigane..!! Tupigane!! Unaijua vita wewe..

Mwenye mamlaka ya kutangaza Azimio la vita, au kitisho Cha vita ni Rais peke yake.. Sasa hawa wengine Sijui nani kawatuma kuropoka.. Huu ni UHAINI..
 
Tukianzisha vita dunia nzima itatucheka. Hii issue lazima ipelekwe kisheria maana hata kama tukishinda vita sio lazima tutakuwa tumepata mpaka kama jamii ya kimataifa haitatambua hivyo.

Wewe hujui,
Vita ndio mpango mzima,
After Vita hata hiyo nusu Ziwa hawapati bali tunalichukua lote, na ikiwezekana tunaichukua nchi nzima ya Malawi na kuifanya Mkoa, angalau southern Tanzania kutakua kumechangamka kidogo kiuchumi.
 
Wewe hujui,
Vita ndio mpango mzima,
After Vita hata hiyo nusu Ziwa hawapati bali tunakichukua lote, na ikiwezekana tunaichukua nchi nzima ya Malawi na kuifanya Mkoa, angalau southern Tanzania kutakua kumechangamka kidogo kiuchumi.


Teh teh teh...mi siogopi vita ila tukichukua kitu kisicho chetu lazima tuwe wababe kama Israel. Vinginevyo itakula kwetu.
 
Lakini jamaa wamesema hawatasitisha cheki kipengele hiki.............[Mussa further said government will not stop exploring oil on the lake as demanded by Tanzania saying “they [Tanzanians] have no powers to do so”.]

Lakini kwenye 'news extract " za leo asubuhi si nimesikia kuwa Malawi "imeufyata" kwa kuziondoa zile ndege zake za utafiti ziwani?
 
Jamaa wanaonekana kuwa na busara sana kuliko viongozi wetu, wanaotaka kujichukulia sheria mkononi. Hivi Membe hajui kuwa kuna international court mpaka yeye achukulie vita kuwa ni suluhisho? anajua kuwa nchi yetu hapa tulipo imefilisika?

Sasa naanza kujua kuwa wapinzani wana akili sana kuliko watawala wetu. Statement ya Malawi inaonekana imetolewa na kongozi mwenye mtazamo mzuri, ile ya Membe na Lowassa ni ya walevi wa virabuni maana kwao kupigana huwa hata bila sababu.


Wewe ni raia wa malawi, tafadhali rudi kwenu Chitipa. Hatuwezi ku surrender hata square Cm moja ya ardhi yeu
 
[h=1]Malawi vows to continue oil-gas exploration on disputed lake Malawi[/h] 2 August 2012 AFP



Malawi vowed Tuesday to press on with oil and gas exploration on Lake Malawi, dismissing a demand by Tanzania, which claims half of the lake, to halt prospecting.
"We categorically put it to them (Tanzania) that as far as we are concerned, the entire lake belongs to Malawi," Patrick Kabambe, principal secretary in the ministry of foreign affairs, said in a statement.
"So our view is that there is no reason to stop the project," he added.
Tanzania has claimed that 50 percent of the lake which forms its border with Malawi is part of its territory.
Tanzanian Foreign Minister Benard Membe last week told domestic media that "exploration activities in the northeast part of the lake should be shelved to pave way for the ongoing discussions to resolve the crisis."
Malawi, a former British colony, and Tanzania, once ruled by Germany, are due to hold talks on the disputed border in the northern Malawian town of Mzuzu on August 20.
Kabambe cited a 1890 agreement between the former colonial powers that stipulates the border between the two countries as lying along the Tanzanian shore of the waters of Lake Malawi.
"Our terms are very clear on this, but we will continue to engage with Tanzania as a good neighbour," Kabambe said.
Mozambique also owns part of the lake.
In September last year, the government of Malawi's late president Bingu wa Mutharika awarded a British firm, Surestream Petroleum, a licence to prospect for oil and gas on the giant lake.
The company has been conducting an environmental impact assessment.
The 29,600 square kilometre lake is Africa's third-largest freshwater lake. In Tanzania, the lake is called Lake Nyasa, which is taken from Malawi's colonial name.


 
NAdhani pamoja na kuwa uchumi wetu unayumba ila hatupo tayari kukaa na kuacha kuilinda mipaka yetu kwa hali na mali. uchumi wetu hali yake ni nzuri ukilinganisha na enzi ya vita ya 1979 na tuliwachakaza vibaya vibaraka wa Amin Dada! Malawi wnadhani tunashindwa, wala hawatusumbui, tuna jeshi kubwa, la kisasa, lenye wataalamu wa fani zote tena ni vijana wenye akili zinazocharge, graduates na hadi PHD holders tena sio zile za kuimba kwaya!

Hawatusumbui ndugu zangu, wao kama hawataki vita wahakikishe wanatusikiliza sisi. Tupo tayari kukaa nao mezani kufikia muafaka wa mustakabali wa suala hili, hapo wakijidai wanakwenda mahakamani pia tutawashinda, wawaulize mambabu zao kwanza mipaka ikoje sio kukurupuka tu.

Sisi ni wakongwe, tena huwa inaniuma ninapoona tumewasaidia sana tena sana majirani zetu wooooote ila wanakuwa na shukrani ya punda, naamini wamesahau umuhimu wa taifa hili, nafahamu tuna matatizo ndani ya nchi kisiasa nk ila haitufanyi tusiungane katika masuala ya kitaifa. Mie ninapenda Malawi wakae na viongozi wetu wakubali kile tulichokubaliana, na Wasitishe shughuli zote za utafiti katika ziwa nyasa mpaka tutakapopata muafaka, kinyume na hapo namuomba Mzee Abrahman Shimbo apange jinsi ya kuwachakaza bila ya huruma tena bila ya msaada toka kokote kwani vifaa vya kisasa tunavyo na jeshi letu sasa ni la kisasa mno!

Vijana tupo tusio na uoga, aseme tu, although najua anao askari w kutosha yeye akitaka reserve army ipo pia ya kutosha.

Its time for our Neighbors to realise that Tanzania is a Mamaland for all Africa, and whoever fights Tanzania will face the whole of Africa. We have a very reputable diplomatic and political history. Malawi we welcome you on the table or meet you at WARZONE!!!!!!!!!:israel:
 
Eneo la NCHI yetu linamuhusu mkulu.. Kila kitu yeye anapiga kimya.. Sasa Kwa hili mkulu unapaswa usemee kitu watz tujue kinachoendelea Na si kila saa wananchi wengine wanapwayukapwayuka tu.. Tunatiana hofu kila kukicha, vita nani asiyeijua.. KamA hujui nenda kawaulize wakazi Wa gongo.. Mtu anapwayuka tu tupigane..!! Tupigane!! Unaijua vita wewe..
Mwenye mamlaka ya kutangaza Azimio la vita, au kitisho Cha vita ni Rais peke yake.. Sasa hawa wengine Sijui nani kawatuma kuropoka.. Huu ni UHAINI..
kuna wanaoamini kuwa Iddi Amin aliamua kuivamia Tanzania si kwa sababu ya kuitaka Kagera bali ku-divert akili ya Waganda kutoka kwenye matatizo ya uchumi ambao ulikuwa umeporomoka kabisa wakati huo. Sasa naanza kuwa na wasiwasi na kinachoendelea maana hizi kauli mala za Mh. Sitta, Membe, Lowassa katika suala nyeti kama hili zilipaswa kutolewa na mtu mmoja tu!
 
Tanzania ni nchi huwezi kufananisha wala kuoanisha na mfano wako. Huwezi kukurupuka kwenda vitani kwa kuwa ndege zinafanya utafiti.

Ingekuwa wanachimba hayo mafuta walau ungekuwa na mahali pa kuanzia. Hivi mbona dhahabu inaibiwa kila kukicha na hatuendi vitani, tunatapeliwa kila leo na viongozi wetu tena mbele ya familia zetu mbona hatuendi vitani, wananchi wananyang'anywa ardhi na wawekezaji ndani ya nchi tena maeneo waliozaliwa mbele ya familia zao na mali zao kuharibiwa au wengine kuuwawa mbona hatuendi vitani.

Ujanja wa zamani huo kutisha watu kwa vita.

Unahitahi kufikiri zaidi ya hapo ulipofikia ndugu yangu. Mipaka ya nchi huwezi ukalinganisha na migodi ya madini. Migodi ya madini ni tatizo tu la usimamizi mbovu na sheria mbovu zilizogubikwa na rushwa ndizo zinatufikisha hapa tulipo, mambo ya ardhi tatizo ni hilohilo la usimamizi mbovu na rushwa na vyote hivi ni mambo ya ndani ambayo hayasogezi mpaka wa nchi. Suala la Malawi linasogeza mpaka wa nchi. Hivi ni busara tusubiri mpaka wapandishe bendera yao ndani ya nchi yetu waanze na kuchimba mafuta ndio tuanze kulalamika au kupambana nao? Au wewe Mmalawi nini mkuu? Narudia kusema hata kama kweli kuna kosa lilifanyika wangedai kabla ya kufanya chochote ndani ya mpaka halali uliopo kwa sasa. Kwa mfano wewe una kiwanja chako unakuta mtu amechimba msingi, unamwambia huyo mtu hiki ni kiwanja changu usiendelee kujenga au nitakuchukulia hatua. Mtu mwingine anasema ungesubiri mpaka apige bati ndio umwulize. Hii inaingia akilini?
 
Jamaaa wanaonekana kuwa na busara sana kuliko viongozi wetu, wanaotaka kujichukulia sheria mkononi. hivi membe hajui kuwa kuna internatinal court mpaka yeye achukulie vita kuwa ni suluhisho? anajua kuwa nchi yetu hapa tulipo imefilisika?? Sasa naanza kujua kuwa wapinzani wana akili sana kuliko watawala wetu. Statement ya malawi inaonekana imetolewa na kongozi mwenye mtazamo mzuri, ile ya membe na lowasa ni ya walevi wa virabuni maana kwao kupigana huwa hata bila sababu.

Mkuu inapokuja katika masuala ya TAIFA letu, wananchi wote tunapashwa kuwa wamoja bila ya kujali itikadi zetu za vyama. Kusema kweli Wamalawi wanashangaza kidogo, hivi ni nchi gani duniani inayopakana na nchi nyingine alafu unakuta ziwa lililo mpakani eti mipaka yake inapitia kando kando (ufukweni) mwa ziwa kwa madhumuni ya kuwapokonya jirani yake umiliki wa sehemu ya ziwa - hii inaingia akilini kweli? Hebu angalia ramani hii ya Wajerumani iliyo letwa humu na mwana JF, inaonekana wazi wazi Ziwa Nyasa limegawanyika nusu kwa nusu, vile vile ziwa Victoria limegawanywa almost nusu kwa nusu between koloni la Kijerumani (Tanganyika) na makoloni ya Uingereza yaani Kenya na Uganda na ukiangalia kwa umakini hapakuwepo mpaka kati ya Kenya na Uganda katika ziwa Victoria.

Nani kasema mipaka ya nchi aiwezi kubadirishwa!!!! Mbona Sudan imegawanywa na kuwa nchi mbili ya kaskasini na kusini? Je iliyo kuwa Yugoslavia kulitokea nini? Hong Kong na Macao zimerudishwa Uchina, mwisho niulize Great lakes zilizo mpakani mwa Canada na Merikani ya kasikazini mipaka yake imekaa vipi, sasa swala hili la Ziwa Nyasa kwa nini nchi zilizo lizunguka zisipewe haki ya kumilika sehemu yake, mbona Msumbiji na Malawi mpaka wake kwenye ziwa Nyasa huko katikati! Why pick on TANZANIA kwa makosa yaliyo fanywa kimaksudi na wakoloni kigeugeu (Waingereza) wakiwa na madhumuni ya kulinda Koloni lao la Nyasaland (Malawi) Tanganyika haikuwa Koloni la Waingereza, walipewa mamlaka na UN kuiongoza kwa muda TU; Hata matamshi haya ya kujiamini yanayo toka Malawi Waingereza wako nyuma yake, si rahisi Wamalawi kuanza kututunishia misuri out of the BLUE.

Kwa hisani ya mwana JF Kobello;4397016]That's an Official map of German East Africa (Tanganyika), after the heligoland treaty.(was produced in 1895).
The map is from the colonial office of Germany. Note the international borders in red

.
il_fullxfull.269120637.jpg
[/QUOTE]

Sasa ramani kama hii ikitolewa Wamalawi watakuwa na kitu gani cha kujitetea, kumbuka Wajerumani hawana hulka ya uzabazabina kama Waingereza, Waigereza mipaka ya Ziwa Nyasa walifanyia usanii wa hali ya juu sana! Naona mgogoro huu ndio utakuwa the begining of the end ya longolongo la Waigereza.
 
Nashauri viongozi wa Tanzaniakama bado haujapata data za kutosha ni vizuri kufunga mdomo ili adui yako asijue udhaifu wako ulipo.Mfano kiongozi unapoongelea mambo ya coordinates je umeshafanya practical na kujua kweli hizo Lat-Long ulizozitaja zipo sehemu gani ndani au katikati au mpakani mwa Tanzania?.Maana haohao Wamalawi watanukuu hotuba yako na hizo hizo Lat-Long kama ushahidi wao na MWISHO UNAKUTA UNAACHIA MAENEO YA NCHI HIVIHIVI KWA AJILI YA UDHAIFU NA KUKURUPUKA KUJIBU HOJA BILA YA KUTAFUTA UKWELI ULIVYO.KWANINI MEMBE ASINGETAFUTA USHAURI KWA PROF.TIBAIJUKA? KWANI HAKUONA JANA MWENZAKE ALICHOKUWA ANAPRESENT UN?WE NEED EVIDENCE BY DATA AND NOT BLABLAH.
 
His Highness,Alhaj Field Marshal Idd Amin Dada, DCO, VCo,nk....The president for Life, alianza kimzaha hivi hivi kwa kudai eneo la kaskazini mwa mto Kagera na sehemu ya nchi yake, halafu akadai na yeye anatake eneo la kaskazini kufika mpaka pwani ya bahari ya Hindi ni lake angalau na yeye awe na bahari. Akapuuzwa kwa maneno maneno, kushtukia tayari ameshanyakua eneo ka kaskazini mwa mto Kagera na kuingia ndani zaidi. Hawa Wamalawi wasipuuzwe, jeshi letu lipelekwe mpakani mara moja, tumeshaumwa na nyoka.....!!

Hivi karibuni ndege ya Uturuki iliingia eneo la Syria na ikatunguliwa, ilikuwa sahihi na Uturuki yenyewe haikulalamika baada ya kuthibitishwa makosa yao. Ndege yo yote toka Malawi ikiingia katika eneo letu itunguliwe tu, mjadala baadae.
 
Back
Top Bottom