Wamalawi washitukia Tanzania na maandalizi ya vita!!

Mimi sielewi huu ubishi kuhusu mpaka kwenye hilo ziwa unatokea wapi. Malawi wananukuu hiyo Heligoland Treaty, Tanzania nayo wananukuu Heligoland Treaty hiyo hiyo!

Kuna mikataba mingapi ya Heligoland?

Hata kama hiyo Heligoland Treaty inaipa Malawi hilo Ziwa bado nitapinga, mantiki haikubali Tanzania kutokuwa na sehemu ya maji ya hilo Ziwa, kutakuwa hakuna tofauti kati ya ule Mkataba wa Sultan wa Zanziba na Germany EA ambapo Sultan alitawala hadi eneo la maili 10 ya Pwani ya Tanganyika !
 
Mkuu hapa hatuendi kwa dunia inasemaje ama sivyo Uingereza haingekuwa Falklands.
Msuli ni muhimu.
Iraq ilivamia kuwait si uliona moto wake haya mambo ya kiCCM tuyaache CCM inafikiri inabishana na CHADEMA inajisahau kwamba hata malawi wanamiliki Jeshi Na Ndege za kivita CCM chonde chonde Msijisahau
 
ww hujui unachokiongea ,they have to stop exploring oil first then tukae mezani.vinginevyo kichapo tu .
Ombeni sana Mungu msichapwe! Do you know who is behind Malawi on this saga? Uwezo wa adui yako haupimwi kwa macho bali kwa kuchapana. So usijidanganye kwamba una jeshi zuri sana kuishinda Malawi, just kwa kuiangalia malawi kwa mwonekano wa nje.

Nafikiri Membe angeonekana mwenye busara sana kama angeagiza malawi itoe ndege zake za kutafiti mafuta hadi hapa mazungumzo yatakapokamilika.

Na angeongeza kwamba iwapo Malawi isingefanya hivyo, Tanzania ingekuwa tayari kuipeleka kwenye court ya kimataifa ya arbitration or else. Lakini kuanza moja kwa moja kutaja habari za vita, ni ukosefu wa busara na hekima.

Unataja habari za vita ilihali hujui uwezo wa adui yako? Hamjiulizi ni kwa vipi Marekani inasita kupigana na korea kaskazini au iran kwa miaka yote hii? Vita si kitu rahisi na cha kukurupuka kama wengi wetu wanavyoweza kudhani.
 
Mkuu CCM inafikiri ni kama kupambana na CHADEMA au vyama vingine vya Upinzani ambavyo havina Jeshi Wanafikiri MALAWI ni chama cha siasa kwi! kwi! kwi! kwi! teh! teh! teh!
 
Mess

Usidanganyike na wanayoandika kwenye magazeti. Kitendo cha kuipa kampuni tenda ya kuexplore ziwa lote ilhali wakijua kuwa hakuna definitive agreement kuhusu mpaka ni act of aggression. Kwa lugha ya kiutuuzima hapo ndio kusema kuwa Malawi washatangaza vita, kwa sababu Tanzania nayo ikianza exploration nini kitafuata?

Ndio maana nikasema serikali ya tanzania katika mkakati wa kuinua wananchi kiuchumi inatakiwa kuwawezesha wavuvi wa ziwa Nyasa kupata boats za kisasa zitakazowawezesha kuingia mpaka katikati ya ziwa kuvua samaki.

Atakayewabughudhi ametangaza vita rasmi, wamalawi wanataka Tanzania ionekana ndiyo iliyoanzisha vita kwa kuwafukuza wawekezaji wao.
 
Last edited by a moderator:
Sasa kipi kilianza mkataba wa Heligoland au hii sheria ya kusema mpaka uwe kati kati ya maji?

Na je Mkataba huu unaosema mpaka uwe kati kati ya maji una exceptions kama anazozisema waziri wa Malawi?
 
Lakini jamaa wamesema hawatasitisha cheki kipengele hiki.............[Mussa further said government will not stop exploring oil on the lake as demanded by Tanzania saying “they [Tanzanians] have no powers to do so”.]
.....hawatasitisha pande yao hili halina shida bali wakiendelea na process hizo hata upande unao milikiwa na Tanzania huo ni ukorofi na kichapo ndiyo suluhisho haya ya mahakamani wataenda wao baada ya sote kuonja joto la jiwe washike adabu zao hawa haya mambo ya kugombana gombana hayana maana lakini yanapohitajika ni nji murua pia kuweka mambo sawa ili tuheshimiane siyo kusumbuana
 
ZeMarcopolo

Naam; wewe umesema kweli sasa waTz tunataka Malawi waseme tunataka vita mara mbili .....hilo walilolifanya si kauri tosha ya kutaka kupigana hivi inaingiaje akili mtu mwaname aje akutomase tomase harafu unasema njoo tukae tuzungumze una maana gani. Ala mi nakufyatua kwanza harafu tutaulizana nikikuzidi nguvu
 
Last edited by a moderator:
WaMalawi wana busara sio kuwa wanataka vita bali wao wanataka haki yao tu. Kuwasemanga ovyo si sawa hata kama ni vita vya maneno. WaTanzania wanajulikana kwa porojo na vita vya maneno unlike majirani zetu in EAC wao ngumi mkononi. mTanzania hadi kurusha ngumi inamaanisha vita vya maneno imeshindikana. So wamefanya jambo la kiungwana na busara kusitisha utafiti wao ili kujenga amani na udugu uliopo.

Mgogoro wa ziwa nyasa haujaaza leo.ulikuwepo hata kipindi cha rais banda na Nyerere. Enzi hizo malawi pia walijaribu kulitwaa ziwa hilo kwa nguvu lakini baadae waliweza kusalimu amri kutokana na kipondo walichokipata kutoka kwa wanajeshi wa Tz. Malawi wanaelewa kuwa mgogoro huu ni wa enzi na enzi.

Wangekuwa watu wa busara kabla ya kuanza kufanya utafiti wao wangeumaliza kwanza mgogoro. Kitendo cha malawi kuingia kwenye ziwa ambalo wanajuwa kuwa linamgogoro bila kuumaliza kwanza mgogoro ni cha kibabe hata kama wanadai lahaki hakikubaliki hapa ni sawa na kuivamia tz. Risasi ndio dawa yake
 
Mimi naona mtazamo wako ndio wa kilevi kwa sababu mtu anakuvamia nyumbani kwako mbele ya mkeo na watoto unamwacha achukue mali zako halafu unasema unampeleka mahakamani, mahakamani my foot.

Yeye alipokuvamia alipitia mahakamani? Yaani wao Malawi wameingia kwenye mipaka yetu wanarusha mpaka ndege ndani ya mipaka yetu hiyo sio kukosa busara, kukosa busara ni kumwambia aache uchokozi vinginevyo tutampiga!!!!!!!!!!!!!!!

Hata kama kuna kosa lililofanyika wakati huo wa kugawa hizi nchi, kwanza lazima kuheshimu mipaka iliyopo then waweke hoja mezani zijadiliwe wakiwa hawajaanza kutuchokonoa.
Tanzania ni nchi huwezi kufananisha wala kuoanisha na mfano wako. Huwezi kukurupuka kwenda vitani kwa kuwa ndege zinafanya utafiti.

Ingekuwa wanachimba hayo mafuta walau ungekuwa na mahali pa kuanzia. Hivi mbona dhahabu inaibiwa kila kukicha na hatuendi vitani, tunatapeliwa kila leo na viongozi wetu tena mbele ya familia zetu mbona hatuendi vitani, wananchi wananyang'anywa ardhi na wawekezaji ndani ya nchi tena maeneo waliozaliwa mbele ya familia zao na mali zao kuharibiwa au wengine kuuwawa mbona hatuendi vitani.

Ujanja wa zamani huo kutisha watu kwa vita.
 
Bandugu tusichukulie ishu ya vita kirahisi. tumeshajiunga na International societies kibao ambazo zinatufunga,hatuwezi kuamua wenyewe tena mpaka hiyo matter ifikishwe kwa level ya kimataifa, unless we agree with Malawians mutually. Vita si poa kabisa
 
Iraq ilivamia kuwait si uliona moto wake haya mambo ya kiCCM tuyaache CCM inafikiri inabishana na CHADEMA inajisahau kwamba hata malawi wanamiliki Jeshi Na Ndege za kivita CCM chonde chonde Msijisahau
Basi tuwatume nyie mkacheze dansi pengine wataacha chokochoko.
 
Bandugu tusichukulie ishu ya vita kirahisi. tumeshajiunga na International societies kibao ambazo zinatufunga,hatuwezi kuamua wenyewe tena mpaka hiyo matter ifikishwe kwa level ya kimataifa, unless we agree with Malawians mutually. Vita si poa kabisa

Askari wameajiliwa na kulipwa mshahara mzuri pamoja na posho nzuri,vifaa vya kijeshi vinanunuliwa kwa ajili ya kazi ya vita.leo hii j banda katutafutia hiyo kazi hamtaki ifanyeke basi hakuna haja ya kutumia kodi za wanachi kwa ajili ya kulihudumia jeshi na ni bora kutokuwa na jeshi.
 
Tukianzisha vita dunia nzima itatucheka. Hii issue lazima ipelekwe kisheria maana hata kama tukishinda vita sio lazima tutakuwa tumepata mpaka kama jamii ya kimataifa haitatambua hivyo.

Pamoja na kwamba ninaunga mkono njia za kidiplomasia zaidi katika kumaliza utata wa mgogoro wa mpaka kati yetu na malawi lakini pia mimi mtazamo wangu ni kuwa JWTZ kuhakikisha kwamba inalinda mipaka yetu ndani ya ziwa nyasa kama serikali inavyotambua kwamba ni katikati ya ziwa.

Sasa ikitokea mtu yeyote, chombo chochote, ama kampuni yoyote inayofanya utafiti ama shughuli yoyote iwe ya kiuchumi ama kijamii ndani ya ziwa nyasa imevuka/wamevuka mpaka na kuingia ndani ya eneo la Tanzania inabidi idhibitiwe/wadhibitiwe.

Kwa kufanya hivyo sidhani kwamba tutakuwa tumetangaza ama kuanzisha vita, hapo tutakuwa tunalinda mipaka yetu na sidhani kama kuna mtu ama jumuiya ya kimataifa itatushangaa ama kutucheka.
 
Ombeni sana Mungu msichapwe! Do you know who is behind Malawi on this saga? Uwezo wa adui yako haupimwi kwa macho bali kwa kuchapana. So usijidanganye kwamba una jeshi zuri sana kuishinda Malawi, just kwa kuiangalia malawi kwa mwonekano wa nje.

Nafikiri Membe angeonekana mwenye busara sana kama angeagiza malawi itoe ndege zake za kutafiti mafuta hadi hapa mazungumzo yatakapokamilika.

Na angeongeza kwamba iwapo Malawi isingefanya hivyo, Tanzania ingekuwa tayari kuipeleka kwenye court ya kimataifa ya arbitration or else. Lakini kuanza moja kwa moja kutaja habari za vita, ni ukosefu wa busara na hekima.

Unataja habari za vita ilihali hujui uwezo wa adui yako? Hamjiulizi ni kwa vipi Marekani inasita kupigana na korea kaskazini au iran kwa miaka yote hii? Vita si kitu rahisi na cha kukurupuka kama wengi wetu wanavyoweza kudhani.
Lukolo hujui kwamba mkwara nao huwa una sehemu yake katika kukabiliana na adui yako.
Sisi wengine tulibahatika kupitia mifumo yetu ya kijadi katika kuwafunda vijana wa kiume tunajua na kutambua umuhimu wa kupiga mkwara, hata kama unajitambua wewe ni dhaifu. Unapiga mkwara kwanza halafu unamuangalia adui yako anauchukuliaje.

Kwahiyo alichofanya waziri membe mimi namuunga mkono mia kwa mia. Kwani naamini kwamba kuingia vitani ni hatua kubwa ambayo haihitaji tamko la waziri wa mambo ya nje, hiyo inakuja baada ya viongozi na makamanda wa vikosi vya ulinzi kufanya intelijensia ya kutosha kufahamu uwezo wa adui yetu na kuangalia uwezo wetu wa kukabiliana nae. Hapo ndipo humshauri amiri jeshi mkuu naye hutoa tamko la kutangaza vita ama vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom