Wamachinga wafanyiwe utaratibu wa ku-graduate

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Hili suala la wamachinga linahitaji akili sana na vinginevyo balaa lake huko mbele litakuja juwa ni balaa kubwa sana.

Wamachinga hawa wametoka vijijini na wanapokuja mjini wana attract wenzao wa vijijini na wao waje na ndio maana kila kukicha wanazidi kujaa na Wenzao wakija na wao wanaanza umachinga.

Hii inafanya population yao kuongezeka kila siku, Hivyo hata eneo ukubwa wa wilaya nzima iwe soko lao tu bado haitatosha baada ya muda kwa sababu watakuja mamia kwa mamia kila siku.

Umachinga ni sawa na Mgodi mpya unapoanza, watu hufanya kuitana na baada ya wiki unakuta mgodi una watu zaidi ya laki moja.

Serikali kwa maeneo inayowatengea wamachinga iweke utaratibu wa kuwapa mwaka mmoja mmoja tu baada ya hapo wanagradute na hapo sasa either akatafute frame au arudi kwao huko akawekeze huko.

Ukiwapa mwaka mmoja mmoja watafanya biashara wakijua wana mwaka mmoja tu wa free.

Hii itasaidia ku accomodate wamachinga wapya, utaratibu wa wao kuwa wana graduate unaweza kwa kiasi kusaidia, make kwa sasa hakuna eneo litakalotengwa litakalowatosha hawa.

Huu utaratibu unaweza fanyika kwa kuwachukua kabisa finger print ili aki gradute my be Arusha asije kimbilia Dar tena akatake eneo la bure.

Serikali ikisema tu itenge maeneo yao ya kudumu hayatatosha kamwe na daima, hawa ni wengi sana, njia ya wao kupeana nafasi ya mwaka mmoja mmoja inaweza saidia kwa kiasi fulani hata kama haitamaliza kabisa tatizo.
 
Kilichopo ni kwamba watanzania wengi hatupendi kulipa kodi na tunapenada mserereko aisee ,kuna watu wanamitaji mikubwa ambapo ukimuangalia tu kwa macho ya kawaida unajiuliza huyu kwa nn hataki kutafuta frem , nilipita mbagala nikakuta eti machinga anauza simu tena sim nyingine za gharama tu nikajiuliza na huyu nae ni machinga ?

Siku moja nilikutana na Dada Fulani hivi kwenye vyombo vya usafiri tukawa tunapiga story akajikuta ananieleza kua yeye kule kariakoo ana meza kumi zaidi ya kumi na zote analipia zaidi ya laki na uchafu kwa mwezi kwa watu waliomkodishia hizo meza ,kaweka watu wanajilipa kutokana na mauzo huyu Dada yeye anauza vijora ,

Pia kule kwenye hizo meza huwa wanauza jumla na reja reja , kwamba asubuhi sana ndio wanauza jumla kwa sababu mida hiyo ndio huja watu wa jumla ,

kuna mmoja yeye namfaham ni machinga wa kitambo sana aisee mpaka muda huu anamiliki coster ipo barabarani inàmletea hesabu.
 
Back
Top Bottom