Kuanzia jana hata leo hapa mjini Moshi watu wamelazimika kutembea kwa miguu kwani usafiri ni wa shida. Kuna ukosefu wa mafuta hasa petroli. Ninafananisha hii kutembea kwa miguu sawa na maandamano ya kiongozi wa upinzani uganda Kiza Besige ya Walk to Work. Hali hii imesaidia watu kujadili hali nchi ilivyo. wengi wanalaani utawala waserikali ya JK kwamba haifai, watu wanaapizana kuwa hakuna nafasi ya CCM kutawala nchi hii tena.
Leo baadhi ya shule hapa Moshi wanafunzi waliruhusiwa kuondoka shuleni kabla ya muda ili kuepuka tatizo la usafiri.