Waliyoteta Odinga, Upinzani yafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliyoteta Odinga, Upinzani yafichuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Sep 24, 2008.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nimeona tangazo kwenye magazeti ya Mtanzania, Dimba, na Rai kuwa waziri mkuu wa kenya Raila Odinga anategemewa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi mpya wa magazeti ya fisadi Rostam Aziz

  Odinga anaheshimika mno, hapa Tz, huenda hajajua kinachoendelea humu ndani kuhusu huyu fisadi na vyombo vyake dhalimu vinavyopigana kucha kufisha demokrasia hapa Tz

  Ningefurahi sana kama JF itafanya linolowezekana ili mh. Odinga afahamu amealikwa na nani na hili limsadie aepuke kutumiwa kwa hasara ya watanzania
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tufanya kiji-petition kisha kiharakishwe kwa Odinga.Rostam ataitumia ziara hiyo kujipatia sort of "clean" international reputation
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sina hakika kama Raila hamjui RA... nadhani hata RA amekwama baada ya leo Mwanahalisi kuandika habari nzito kumhusu. Bahati mbaya Mwanahalisi halimo katika mtandao, lakini kwa wenye kuweza kutusaidia nyumbani wange scan na kuiweka humu.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Halisi,
  Tina ameshascan na kuiweka hiyo makala JF
   
 5. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Jasusi hiyo habari ipo wapi?
   
 6. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,565
  Trophy Points: 280
  Waliyoteta Odinga, Upinzani yafichuka

  2008-10-05 14:42:10
  Na Muhibu Said

  Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto, `ametoboa` siri ya kikao kati ya viongozi wakuu wa vyama vya CUF, Chadema na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga aliyemaliza ziara nchini hivi karibuni.

  Kwa kile kilichodhaniwa kuwa ni siri lakini sasa siyo siri tena, Odinga katika kikao hicho anadaiwa kuwapa wapinzani mbinu ya namna ya kukishinda katika uchaguzi na kuking`oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, aliwataja viongozi wakuu wa vyama hivyo waliokutana na Odinga katika kikao hicho kuwa ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Zitto mwenyewe.

  Alisema kikao hicho kilichofanyika katika hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam, kilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuhitimisha ratiba ya ziara ya Odinga, ambapo pamoja na mambo mengine alipanga kukutana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.

  Zitto alisema katika kikao hicho, Odinga aliwaeleza kuwa uwezekano wa kuing�oa CCM madarakani upo na mkubwa, lakini kwa namna wapinzani wanavyokwenda hivi sasa nchini, ni ngumu kutekeleza lengo hilo.

  "Ili muweze kuchukua majimbo mengi ya ubunge na kushinda urais, dawa pekee ni kuungana. Msipofanya hivyo, kamwe hamuwezi kuiondoa CCM madarakani."

  Na kwa hali inavyokwenda hapa Tanzania kwa wapinzani, ni ngumu kuiondoa CCM madarakani,`` Zitto alimkariri Odinga akisema.

  Kutokana na hali hiyo, Zitto alisema Odinga aliwataka wapinzani waachane na ubinafsi, badala yake wasimamishe mgombea mmoja anayekubalika katika nafasi zote (urais na ubunge).

  Zitto alisema katika majibu yao, viongozi hao wa upinzani waliunga mkono hoja ya Odinga na wakakubaliana kuimarisha ushirikiano wao na kuunda mikakati kwa lengo la kuishinda CCM.

  Hata hivyo, ushirikiano wa kisiasa kati ya vyama vinne vya upinzani, unaonekana kusambaratika kutokana na tofauti zilizoibuka kabla na baada ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani katika jimbo la Terime, Mkoa wa Mara.

  Hali hiyo ilidhihirika baada ya baadhi ya vyama kuamua kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi huo, huku vingine kila kimoja kikisimamisha mgombea wake, kinyume na makubaliano ya ushirikiano wa kisiasa uliotiwa saini kati ya vyama hivyo mwaka juzi.

  Vyama vilivyotiliana saini makubaliano ya ushirikiano huo ni CUF, Chadema, TLP na NCCR-Mageuzi.

  Hata hivyo, katika uchaguzi wa Tarime, CUF na TLP, vinamuunga mkono mgombea wa Chadema, Charles Mwera wakati NCCR-Mageuzi na Democratic (DP), kila kimoja kimesimamisha mgombea wake.

  Chadema, TLP na CUF, vilianza ushirikiano rasmi bungeni na kuunda kambi rasmi ya upinzani ambayo inatambulika rasmi bungeni.

  Tangu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Zakayo Wangwe kilichotokana na ajali ya gari Julai 28, mwaka huu, katika kijiji cha Pandambili, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, kumekuwa na mvutano wa wazi baina ya viongozi wa kambi ya upinzani.

  Tukio la kipekee lililotokea ni pale mazishi ya Wangwe yalipoahirishwa Julai 31, mwaka huu, kutokana na familia kutaka uchunguzi wa kujitegemea kuhusu ya chanzo cha kifo cha mbunge huyo, hali iliyowagawa viongozi hao kwenye makundi mawili.

  Chadema wamekuwa wakilaumu wenzao kwamba walitaka kutumia msiba huo kupata faida ya kisiasa, lawama ambazo pia zimeelekezwa kwa CCM.

  SOURCE: Nipashe
   
 8. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli; Upinzani wataitoa CCM Madarakani hapo mwaka 2050.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kabwe aseme wazi kuhusu ushahidi uliopatikana tayari huko Tarime kwua kuna mkono wa Odinga, wasi wasi wangu ni kwamba tusipokuwa waangalifu ni kwamba hawa wenzetu yaani majirani, wanaonekana kuwa na agenda ya kutuuzia mifarakano kutoka kwao ili nasi tuanze kupigana wenyewe kwa wenyewe,

  Ingawa misaada kwa vyama vya siasa sio tatizo, lakini ni lazima sometimes tuwe waangalifu!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,565
  Trophy Points: 280

  FMES, kama unao ushahidi huo umwage hapa ukumbini tuujadili.
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi yenye mazingira mazuri ya kisiasa hasa kwa vyama vya upinzani kuliko nchi nyingi duniani, hata hivyo upinzani ndo umekuwa butu uliojaa migogoro ya kila siku. Suala la upinzani kuungana eti ni siri! eti ni suala la kuambiwa na Raila! i back you Mkuu Ladslaus Modest kwamba upinzani utachukua madaraka 2050.

  Concept ya "bottom - up" bado kabisa haijawaingia wapinzani wa Tanzania. Wakajifunze kwa MDC.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu lazima kuna something na hii ishu, kwa sababu jana usiku nimepata dataz straight kutoka huko Tarime, kuhusiana na hii ishu nikaziweka hapa na leo unaona magazeti yanathibitisha kuwepo something kitu ambacho kinanifanya niamini kuwa dataz nilizozipata jana zina ukweli mkubwa sana,

  Ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa tepu maalum zilizomrekodi Rostam na Makamba, wakikutana na Mtikila kabla ya kwenda huko Tarime, ambapo walimpa mikakati na pesa za matumizi kwa safari hiyo ya Tarime hizi zote nimezipata jana toka huko Tarime, ndio maana tulisema kupigwa kwa Mtikila huko ilikuwa ni sawa sawa.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,565
  Trophy Points: 280
  Hata kabla ya Odinga kuwaambia wapinzania umuhimu wa kuungana, Watanzania wengi tu wameshawaambia wapinzani kuhusu umuhimu wa kuungana na hata hapa ukumbini ushahidi wa hilo upo. Hivyo alichosema Odinga siyo siri kwani upinzani umeshaambiwa umuhimu wa hilo katika kila kona ya nchi yetu tatizo ni kwamba ndani ya vyama hivyo bado viongozi wametawaliwa na ubinafsi wa hali ya juu, kila mmoja ana wasi wasi kwamba mara watakapoungana basi atakuwa hana wadhifa mkubwa kama aliokuwa nao sasa hivi.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,565
  Trophy Points: 280
  Kama hii ni kweli basi kazi ipo. Nilishaweka hapa habari kuhusu Mtikila kuwashambulia CHADEMA. Na nikauliza je Mtikila kapewa bulungutu na RA ili awashambulie CHADEMA? Maana miaka yote target ya mashambulizi ya Mtikila ilikuwa ni CCM ghafla tu imebadilika na kuwa CHADEMA. Na ukitilia maanani RA alianika hadharani kwamba Mtikila alienda kuomba michuzi kwa RA, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba Mtikila kishatiliwa kitu kikubwa na RA na CCM ili awashambulie CHADEMA. Kweli siasa ni mchezo mchafu sana.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tikila alipewa zaidi ya zile 3m alizosema rostam hapo awali, na pia ile kesi alioshinda juzi, inawezekana ina masharti ya kuua upinzani kwa faida ya ccm
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi hili suala wanatakiwa kuambiwa na Odinga wakati ndio kilio cha kila siku cha wananchi kule nyumbani na hapa JF?

  Labda watamsikia Odinga kwasababu ni PM.
   
 17. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wapinzani wa Tanzania kuungana na muungano kudumu ni kazi kweli kweli, kwa sababu kila mtu anakwenda na ajenda yake ...hawana "common agenda". Lingine kulinganisha wapinzani njaa wa Tanzania na Kenya vile vile haiwiani, wapinzani wakenya wengi wao ni watu walitosheka kwa namna yao (ukichukulia mfano wa Odinga na wengine), lakini wapinzani wa Tanzania wengi wao nia ni kuganga njaa, kwa hiyo ni rahisi kuyumbisha kwa lolote lihusuyo maslahi yao na familia zao. Swala jingine ni kuwa Tanzania sijaona "Uniting figure" kutoka upinzani mtu ambaye kweli wananchi na wapinzani wenzake watamkubali iwe kwa kujenga hoja, uongozi na maisha yake binafsi.....So kuungana ni swala zuri lakini sisi watanzania naona tuna-challenge kubwa zaidi ya Kenya ikiwa kutika kwa vyama vyenyewe na wananchi kwa ujumla, kwa sababu hata wakiungana wasitarajie matokeo yatakuwa mara moja inahitaji muda na kujitoa kweli kweli.
   
 18. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Labda wakiambiwa na Odinga ndio watauona umuhimu wa kutekeleza suala la kuungana. Lakini mimi naamini katika kitu kinachoitwa "threshold" ama wengine tuite "boiling point", kwamba hapa kwetu haijafikiwa. Nilijifunza katika fizikia kuwa vimiminika mbalimbali huchemka kila kimoja kwa wakati wake, kuendana na hiyo boiling point. Itakapofikia "political boiling point" yetu huko bongo, wala hakuna atakayetutuma tuungane, huo muungano utakuja wenyewe tu naturally. Kule Ukraina kwa kina Yushchenko na Shevchenko kipindi kile, na kule Yugoslavia kwa bw Kostunica wale wananchi walipoingia barabarani kwa wingi hadi majeshi yakawashindwa kutokana na wingi wao, hawakufanya hivyo kutokana na kuhubiriwa au kampeni, ni kwamba walichoka, walifikia mahali wakavuka boiling point, elastic limit au threshold of tolerance. Katika hatua kama hiyo haiwezekani tena kuzuia mabadiliko.

  Huko kwetu labda hatujafikia point hiyo, ama waliyoifikia na wanaoweza kuihisi ni wachache na wanashindwa kuwaambukiza (induce) wengine. Tunasema tuna amani na utulivu? Labda utulivu hauna mwisho (Newton's first law, "unless compelled by some external forces..."), lakini sisi tuna amani na uvumilivu! Uvumilivu una mwisho maana hutumia energy! Hiyo limit of tolerance itakapovukwa ndipo yatakapotokea mabadiliko. Labda pia sisi wa ngozi ngumu tuna threshold kubwa sana ya tolerance, mfano wa punda! Lakini hata punda na uvumilivu wake, ukijisahau tu ukamtwisha mwanae mzigo mbele yake, basi mama punda anazira! Analala chini hatembei tena, hadi umtue mwanae mzigo.

  Threshold of tolerance. Boiling point. Elastic limit. Tujipongeze kwa kuwa na amani na uvumilivu?
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Oct 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Duh,Mwalimu Kithuku nimegundua wewe ni kichwa wa physics.Hata hivyo ni mwanafalsafa kama Albert Einstein
   
 20. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kuungana TZ kusema ukweli tuna hatua ndefu mbele, manake kuna vyama vina muungano (CHADEMA, CUF, TLP na NCCR) ambao wanasema kuwa ikifika uchaguzi wa 2010 upo uwezekano wa kusimamisha mgombea mmoja katika jimbo kwa ajili ya Ubunge na pia ikiwezekana mgombea mmoja wa uRais. Lakini kinachoshangaza wanashindwa hata kuanza sasa, mfano jimbo la Tarime, ilikuwa rahisi kusema CHADEMA wana nguvu pale, na hakuna ubishi tuwaachie CHADEMA. Mfano ungeanza sasa hata kwa viti vya madiwani. Uchaguzi wa madiwani ndio huo unakuja sijui kama kutakuwa na badiliko kwa hawa wakuu.

  Tatizo ni kuwa kiloa mtu anaangalia maslahi, na hii RUZUKU hii itolewayo kwa vyama kutokana na uwakilishi wa wabunge waliopatikana ina faida na hasara kwa hivi vyama. Kwanza tunaanza na ubinafsi, kila mtu anautakaubunge ili apate maslahi, na hivyo kuachiana hakupo. Pili linakuja suala la ruzuku, kila chama kinataka kuwa na wabunge wengi ili kuongeza ruzuku.
   
Loading...