Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Kuna vitu vingine vinafanywa na serikali na CCM na serikali yake hadi vinatia aibu. Kila mtu anajua wakati wa uchaguzi wa Chadema Lissu Vs Mbowe, serikali na CCM walifanya kila wawezalo ili Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa Chadema, ikashindikana.
Kisha wakaanza kuwatumia wafuasi wa Mbowe ndani ya Chadema, G55, kumpa Lissu wakati mgumu, ikashindikana.
Wakaamua kumfungulia Lissu kesi ya kubambikiza ya uhaini. Bado wanaona haitoshi.
Sasa wameamua kumtumia Msajiri wa Vyama vya siasa kuimaliza Chadema.
Hivi kwa nini kuwe na nguvu zote hizi dhidi ya Chadema? Tatizo hasa hapa ni nini, Lissu au Chadema?
Kwa nini CCM na serikali wanaona kwamba kuwa na upinzani ulio na nguvu nchini ni jambo baya lisilovumilika? Mnaogopa nini, kwamba CCM ikiondolewa madarakani madhambi yenu yakafichuliwa wengi mtaishia jela?